Teknolojia ni Yetu sote
JF-Expert Member
- Apr 28, 2020
- 1,221
- 2,425
Kila mwaka ifikapo tarehe 17 July Duniani watu huweza kusherekea siku ya Emoji Duniani. Emoji ni ishara inayoelezea kwa Namna gani mtu anajisikia Kwa wakati huo.
Emojis Kwa mara ya kwanza iligunduliwa mwaka 1999 na jamaa anaitwa Shigetaka Kurita, ni mjapani ambaye aliamua kuunda Emoji ili kuweza kurahisisha watu katika kueleza hisia aliyonayo kupitia mfumo wa kidigitali.
Kwa mara ya kwanza aliweza kutoa emoji zenye ishara 176 pekee, na ziliweza kushika Kasi Nchini Japan kabla ya kusambaa Duniani kote. Mpaka kufikia Desemba 2024 jumla ya emoji zote Duniani zilikua 3,790.
Hesabu hii inajumuisha Emoji zote kuanzia za bendera, solo emoji , jinsia nk. mwaka zinaweza kuongezeka emoji 164 mpaka kufikia Desemba 2025 tutakua na jumla ya emoji 3954. Emojis ni zaidi ya hisia inayomtambulisha binadamu.
Ebu tuambie emoji gani unapenda sana kuzitumia kwenye simu yako !!