Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,488
- 13,608
Leo nimegundua kuwa Mzee Edward Lowassa ni mstaarabu sana. Warusi wanatumia neno kachestveni ( high quality a person).
Kama kila tusi analotukanwa mtu lingekuwa linaleta kovu mwilini, Mzee huyu asingekuwa anatazamika kwa sasa.
Ukimya wake kila anaposhambuliwa ni kitabu tosha kabisa chenye kurasa zinazozungumzia uvumilivu na ustaarabu anaopaswa kuwanao mwanadamu mwenye kujifahamu.
Pengine Mzee afikirie juu ya kuandika kitabu kuhusu maisha yake ya kisiasa, vizazi vijavyo vya wanasiasa vitabakiwa na kumbukumbu elimishi.
Watoto wake waanze kufikiria juu ya utamaduni huo, zile kumbukizi (legacy) za kina Malcom X na Martin Luther na wanaharakati wengine, bado zipo hai kwa sababu ya ukweli kwamba maandishi huwa hayafi.
Unapokaa kimya na kutii mamlaka hata kama unaona upungufu mwingi ndani ya hizo mamlaka, ni kuendelea kuitunza amani ya rohoni.
Wanasiasa mjifunze kwamba kupayukapayuka kunaweza kukupunguzia heshima mbele ya jamii.