Leo kidogo nikamatike na Wife kwa uongo wa kizembe kabisa

mkuu piga konyagi kubwa kabisa ukifika home uwe top top..hamna discussion asubuhi mpige miti ya hatari..kesi hamna
 
Sijui kwa nin Akili Yangu inazidi kupingana na huu ujinga anaotuaminisha huyu jamaa.
 
Tutafute hela wanaume wenzangu,tuache kutegemea hela za wake zetu.... Ni aibu kuu mwanaume kumuogopa mke wake kwa viwango vya aina ya mleta mada.
 
Salaam Wakuu.

Daaah Ha ha ha ha, ngoja nicheke Kwanza. Uongo sio mzuri wakuu ha ha ha ha.
Uandishi wangu sio mzuri ila tuvumiliane.

Ilikuwa hivi mwezi Kama Mmoja uliopita Mimi na wife tulipata ka plot tukakapenda Sasa tukakubaliana na mmiliki ambae alikuwa mkoa B, pale eneo la tukio aliwakilishwa na Ndugu yake. Sasa baada ya kukubaliana bei Tshs 1500000 tukaachana kwa kukubaliana kuwa nitawalipa baada ya Kama siku 3 hivi.

Kweli Mzee mzima baada ya siku tatu nikawa nimekamilisha Mzigo Sasa si unajua Tena mishe za kibaharia, Mzee. Nikatumia Mzigo wote sikulipia ile plot, wife kuniuliza vipi? Nikamwambia nishalipia tayari Mambo yote yapo kwenye mstari kwahiyo wife Usijali Kabisa nakulove balaa wife na mbwembwe nyingine kibaoooo.

Sasa siku zinazidi kwenda Mimi Sina habari namwambia tu yule Ndugu wa muuzaji aliye mkoa B kuwa nitakukamilishia muda si Mrefu pesa ipo.

Ebanaaa eee Sasa leo wife kakatiza maeneo ya hako ka plot mara paaah anakuta watu wanapimiana mahatua na kuoneshana mipaka. Si kawapandishia kuwa nyie vima niaje hapa kwenye Mali za watu? Mnatafuta Nini? Hiki kiwanja Ni changu. Jamaa wakasema wametumwa na muuzaji aliye mkoa B. Heee wakamlukia hewani Ndugu wa muuzaji kumuhoji hii imekaaje? Akasema Mimi sijapewa hela. Kumlukia mwenye plot nae anasema hajapewa hela hivyo anauza kiwanja kwa mwingine. Huku Mimi nishamwambia wife kiwanja shalipia kitaaambo, huwa akiniuliza maandishi yako wapi, Kila siku namwambia nimesahau Ofisini.

Sasa nipo Ofisini nakaribia kuingia kwenye Kikao mara Simu ya mtoto mzuri (wife) hii hapa. Napokea kwa mbwembwe nambie mtoto mzuri, umenimiss?..." Wewe kiwanja ulisema ushalipia mbona nimekuta watu wanapimiana na mpaka mwenye kiwanja na Ndugu yake wanasema hawajapata pesa? Wewe hebu nieleze Vizuri au hukulipia ulinidanganya? ( Na wife kitu ambacho huwa hapendi Ni uongo )

Mnnnnnh, nikasepa fasta pembeni ya waheshimiwa. Nikasema wife mi nishalipia Mbona kitambo? Akasema mmnh mbona wote wanakataa au matapeli? Sasa hawa watu waliopo hapa nakuja nao kwako na wewe mtafute yule Ndugu wa mwenye plot halafu uniambie sehemu ya kukutana ili tuone Nani tapeli.


Mnnnnnh nikaona Mzee mzima naenda kuumbuka hapa na mbaya zaidi naenda kuharibu ndoa na mtoto mkaleeee, ha ha ha ha daaah.

Nikasema litakalokuwa na liwe nikamuibukia hewani yule Ndugu wa mmiliki wa plot ( Ni Mzee wa makamo kidogo huwa ananiheshimu Sana) Mzee naomba Tuonane fastaaa. Bila Shida Mzee akakubali. Nikatoka nduki eneo la Kikao Kama nimefumaniwa.

Nikakutana na Mzee ikabidi nimchane tu , " Mzee nilimdanganya wife kuwa nishanunua kiwanja Sasa Leo kule mwenye plot katuma mtu mwingine wife kawafuma na anataka Tuonane wote Sasa Mzee Wangu nisaidie kiume hapo maana mtiti wa wife naujua akifika hapa"" sitaki tuonane nae Saizi.

Huku wife anapiga Simu kinomaaaa, mko wapiiiiiii? Mimi nazuga tu ngoja ndio namtafuta yule Mzee.

Sasa mara Simu inaita balaa nikaacha kupokea, Sasa wife kwa akili ya kijasusi akahisi something is fishyyyy. Mara text zikaanza kumiminika Kama Ak 47. ( Hapa mabaharia mnanielewa mwanamke akihisi unamdanganya halafu hupokei Simu hizo text zinavyoanza kumiminika)

Ikabidi nifanye Kama sisikiii nikakomaa kumpanga Mzee. Mzee akasomeka ikabidi amuibukie hewani mwenye plot kumpa mchongo ulivyo mwenye nyumba akakubali ila akataka alipwe 2000000. Hapo hapo ili aachie uwanja maana anasema wife kamuwakia kinyamaa.

Baada ya kukata Simu Mzee akasema Jamaa kapanda Sana, Mimi nitakupa kiwanja kingine. Sasa nikawaza huu muda wa mpaka kwenda plot nyingine halafu wife kakaba Koo. Daaah halafu Siri ya kambi isije vuja.

Sasa ikabidi nichague, wife ananiamini kinoma either nikutane nao halafu baadae tambembeleza najua atakaa sawa tu Ila litakuwa doa la kizembe Sana. Kisa laki 5?

Daaah kwa kulia na kusaga meno ikabidi nimtumie mmiliki huo mpunga nae amwambie wife kuwa hela ilitumwa kwa Kaka yake wa huko huko ila alichelewa kumpa baada ya kuingiza Katika business zake.

Daaah na Mzee nae akampoza wife kwa hiyo story. Wife akapoa ikabidi aachane na wale Jamaa.

Daaah nikatuma text ya udhuru wa Kikao saizi nimepoa mahali jioniiii hivi ndo niibuke kilingeni nikute injini imepoa.


Wadau uongo huu wa kizembe hivi ha ha ha ha sio.
Inaonekana wewe ni tapeli. Au unatabia isiyofaa
 
Back
Top Bottom