Nimwambie ukweli wife au niendelee kushikilia msimamo wangu?

ni huyo mm

Member
Apr 28, 2022
25
79
Hakika Ngoma ikivuma Sana inapasuka waswahili walinena, Leo ni siku mbaya sana ktk maisha yangu nahisi uwezo wangu wa kufikiri umefika mwisho.

Ishu ipo hivi jana nilikuwa na mchepuko wangu kwenye gari na unajua Tena wawili wakiwepo watatu wao huwa ni shetani. Sasa bas tukaanza kushikana(ashakumsi matusi)kitendo kilichopelekea mchepuko asahau chupi yake kwenye gari,(hapa sijui ni kusudi au bahati mbaya)lakini baada ya kuachana alinisms kuwa amesahau kufuli lake na mm niliona msg lakini nikajipa moyo nitaliweka sehemu salama tukikutana nimpatia(big mistake)

Fila na Hila Ila siku zote havikai pamoja sikio la fila nilikisia jicho la hila ujifanya halijaona(maji na maziwa vikatengana bwana)

Nilitoka kazini nimechoka nikala na wife akaniambia nikalale kidogo(mwanzo wa tatizo)

Nilikumbuka kuhusu chupi ya mchepuko niliyoweka kwenye gari na nilichofanya ni kulock gari na kuweka funguo kwenye mto(Kumbe nilipitiwa na usingiz mzito Hali iliyopelekea funguo uonekane na wife na kwenda kwenye gari.

Basi bwana akaja mgeni wife akaniamsha nikaongea na mgeni baada ya kumaliza ndio nikapata mshtuko kuona funguo kwenye kochi badala ya kitandani.

Nilizuga zuga pale nikadaka funguo kwenda kucheki mazingira kwenye gari kama sir god kaamua kunistiri au ndo amenibeba sasa amenichoka kaniachia mwenyewe mabalaa yangu niangaike nayo.

Ha haulaaaaa!!!nilikuta Ile chupi wife kaitandika juu ya Siti ya dereva daaaaa nikabaki kwenye gari kama nusu Saa hivi akili ikiwa imestack.

Bas bwana nikaazimia kupindua kesi nikaingia ndani nikamwita wife nikamuangushia zigo.

Nikamwambia Kuna mwanaume amenipa hiyo chupi nimpe yeye coz huyo mwanaume anasema ameshatoka na wife kitambo kabla mm sijamuoa (uongo mtupu)
Sasa bas wife alikuja kwa unyenyekevu uku machoz yakimtoka na kusema maneno mawili tu"'dii muogope Mungu ipo siku utakufa" baada ya kusema hivyo akatoka akaniacha room.

Hakika haya maneno yamekuwa mkuki moyoni na roho inavuja damu na inanisuta nyingine inaniambia nimuombe radhi wife na nimueleze ukweli na nyingine inasema ndo nitaharibu kabisa!

Naombeni msaada wenu wa mawazo wadau kipi ni Bora au nitumie Njia gan sahihi ya kusolve hii ishu peacefully na nibaki na amani ya moyo.
 
Back
Top Bottom