Leo Ijumaa, Agosti 7 nitazungumzia siasa zinazoendelea nchini channel 10 saa 4 usiku, karibuni

Humphrey Polepole,

..Magufuli ana tuhuma za kuuza nyumba ya serikali nchi nzima kwa bei ya hasara.

..kuna wanaomtetea kwamba ni uamuzi wa baraza la mawaziri. lakini tatizo linakuja kwamba hata yeye mwenyewe alijiuzia nyumba hizo na baadhi tunaambiwa aliuza kwa ndugu zake.

..sasa hebu tuambie huyu unaanza vipi kumsafisha? wewe kama mwana-ccm umemkubali mgombea huyu? je, kama mwana-ccm una moral authority ya kumnyooshea kidole Lowassa ambaye amesema richmond ilikuwa amri ya mamlaka ya juu yake, na hakuna mahali popote ilipobainika kwamba Lowassa amefaidika binafsi na richmond?

Hvi aliye weka sahihi kwenye mkataba wa richmond ni nani? Kama aliweka lowasa basi yeye ndo anapaswa kubeba msalaba maana yeye kaona mkataba mbovu na bado karidhia kuweka dole gumba lake, hakuna kiongozi hapa kama wakina,luanjo wamempeleka mjini hataweza kua mkuu wa kaya, bye bye lowasa ikulu ndo basi tena kwako
 
Last edited by a moderator:
Tuna tatizo kubwa sana kwenye mfumo wetu wa haki kama taifa!!Ni kweli kuwa kiongozi wetu akituhumiwa anapaswa kukaa pembeni kama alivyofanya Lowasa,ingawa Magufuli hakufanya hivyo.Anakaa pembeni ili kutoa nafasi ya kuthibitishwa au kukanushwa kwa tuhuma hisika baada ya uchunguzi.Sasa bwana Polepole anasema Lowasa alikuwa mtuhumiwa tangu 1995 lakini aliteuliwa kuwa waziri na Nyerere akiwepo na ikaridhiwa,2008 akajiuzulu lakini miaka 7 baadae tuhuma hazijathibitishwa wala kukanushwa!!!!!Haki yake mtuhumiwa huyu ya kuhukumiwa au kuwekwa huru dhidi ya tuhuma husika ingebidi akae pembeni mpaka lini?????
 
leo tarehe 7 agosti siku ya ijumaa saa 4 hadi 5 usiku nitakuwa katika televisheni ya channel 10 kipindi cha mada moto. Huko nitazungumzia yanayoendelea kujiri katika siasa za tanzania.

nitasema vitu kadhaa visivyo vyepesi, lengo likiwa ni kusaidia umma wa watanzania kuujua ukweli na hatimaye wafanye uamuzi sahihi oktoba. Ninaomba sana uhimilivu wenu ambayo pia ni ishara ya ukomavu wa siasa za ufuasi na uumini, zile zinazojenga umoja wa taifa letu.

naomba "share" na wajulishe watu wengi zaidi.

========================


jamaa kapwaya sana leo, too biased
 
Hongera PolePole Umenena vyema kabisa bahati mbaya tu umekutana na washabiki maandazi ambao wao wanapenda wasikie vitu vinavyowafurahisha tu
 
Inasikitisha sana kuona ukabila na undugu kama huu Tz...1. Mwenyekiti Chadema taifa- Mh FreemanMbowe (mchaga,kilimanjaro)2. Mkurugenzi wa fedha na uwekezaji - NduguAnthony Komu (mchaga,kilimanjaro)3. Mwenyekiti Bodi ya wadhamini ya chama -Mh. Philemon Ndesamburo (mchaga,kilimanjaro)4. Mkurugenzi wa Rasilimali wa chama- NduguSuzan Lymo (mchag,Kilimanjaro)5. Mkurugenzi wa Bunge na Halmashauri -NduguJohn Mrema (mchaga, kilimanjaro)6. Naibu katibu Mkuu wa chama - JohnMnyika ( mpare wa kilimanjaro mwenye maskani yake Dar)7. Mwenyekiti wa Wanawake Halima Mdee (Mpare wa Kilimanjaro mwenye maskani yake Dar es Salaam)8. Makamu mwenyekiti wa Wazee Susan Lymo (mchaga wa Kilimanjaro)9. Walinzi wote wa Mbowe (wachaga wa Kilimanjaro)10. Asilimia 98 ya madereva wa Chama wachaga wa KilimanjaroAsilimia 80 ya wabunge wa kuteuliwa wa Chadema wanatoka Kilimanjaro naArusha,wakiongozwa na Mrs wa Mbowe wa pili Joyce-Mukya, Grace Kihwelu, Suzan Lymo, Lucy Ndesamburo Owenya, Cecilia Pareso, Rebecca Mngodo na Rose Kamili.11:Tundu Lisu MB na dada yake wa kuzaliwa MBwa kuteuliwa,12:Dk Wilbroad Slaa katibu mkewe wa ndoa Mbwa kuteuliwa13:Mbowe Mwenyekiti Mkewe mdogo Mb waKuteuliwa16:Ndesamburo Mb mwanawe wa kuzaa MBkuteuliwa16:Mtei Mlezi wa chama mkwewe MboweMwenyekiti wa Chama,Hii familia inataka iongoze watu zaidi ya milioni44 haitakuja kutokea katika historia ya TanzaniaNdio wanafamilia hawahawa waliomtengenezea zengwe la kumfukuza Mh Zitto Kabwe katika chama hiki cha kifamilia baada ya kuona anakubalika ndani ya chama hicho na anauwezo wa kuwa mwenyekiti endapo angechuana na Mbowe lakini si mchaga wala mtu was kaskazini.Hapo ndipo vikao vya kifamilia vikaanza na kuamua kumtimua Zitto.Wanafamilia hawa ndio wamemuuzia chama chao Edward Lowassa kwa kiasi cha Billion 10 ili agombee urais kupitia chama hiki! Dr Slaa alipohoji akaambiwa wewe sio mwanafamilia hivyo tulikustili kwa muda tu. Ndipo slaa akagundua kuwa sio chama bali ni SACCOS na kuamua kujiengua.Mwl Nyerere aliwahi kusema, nanukuu " Mtu anayeonekana anapenda sana kwenda ikulu hafai hata kidogo ni wa kukwepa kama Ukoma".NDG watanzania huyu Lowassa anavyopenda sana kwenda ikulu tumkwepe. Hizo bilioni 10 alizonunulia chama anataka akazirudishe kwa kutuibia sisi wananchi. ZINDUKA!Kama amenunua chama akipewa nchi siataiuza kurudisha gharama zake......!!!!?

Hii ilishapitwa na wakati. Katafuteni nyingine. Hatuna muda na hii tena. Imechujaaaaa.
 
Watu wa UKAWA hovyo sana yaani mtukiongea kinyume na mioyo yenu baasi mnamkashifu sana. Lowassa si msafi jamani tuelewe hilo.

Lowassa si msafi wewe ni msafi! Mbona kila siku unaoga na kusukutua? Na kule msalani huendi au! Wewe ni mahakama?

Ebu niambie kwenye ile list alitajwa rais wa JMT JAKAYA KIKWETE vipi mlimsafisha lini?

Pole pole namkubali sana lakini leo kachemsha siasa hawezi.
 
Polepole H my class mate alisema ili UKAWA idumu Rais asiwe Dr slaa wala Prof Lipumba na ikawa hivyo Je UKAWA imekufa?

Umesahau jambo moja,alisema pia japo yeye ni mwanaCCM lakin CCM wakiteua mgombea wa urais FISADI basi atampinga mgombea huyo kwa uwezo wake wote.

Bahati mbaya mgombea huyo FISADI hagombei CCM bali sasa anagombea UKAWA
 
Naona nae kanunuliwa.Iweje anaitetea Ccm,wakati waliikataa katiba waliyoipendekeza.Kama Lowasa ni fisadi mbona hapelekwi mahakamani.Naona kuna nguvi kubwa sana inatumika kuzuia ukawa.Ila Mabadiliko yakitaka kutokea,hayawezi kuzuiliwa kamwe. Poor u Polepole.Umejishushia heshma sana.
 
Huyu alitabiri ili ccm ibaki salama ni lazima lowasa na membe wakatwe ikawa hivyo na upinzani akawbeza Dr na leprofsa akaomba aje MTU ccm ili washinde sasa kinachomtatiza alidhani atakuja ngeleja au duwani badala yake likaja buludoza mashine ya uhakika ndio maana amepata presha

Sijui alitaka aje muhongo au yule mzee aliyepewa kichapo kule tanga! Ukimwondoa el nani mwingine ndani ya ccm mbadala wa dr slaa!
 
Leo nilipoteza muda ili niangalie uchambuzi wa Humphey Polepole lkn hakuwa polepole niliemjua katika ubora wake,uchambuzi wake ulijielekeza kwenye chuki zake dhidi ya mgombea fulani,alikuwa bias sana
 
Eti,.,.''kiongozi wa taifa anapaswa awe juu ya tuhuma. Anayetuhumiwa hafai kuwa kiongozi'',.,.,.,. !!!!! Kusema huu msemo ndani ya hicho chama,.,.,. unaonekana wazi kwamba na wewe ni mwendawazimu-kwa kiasi fulani!!!!!! :smile-big:
 
Hamprey Polepole anasema yeye anasimamia Katiba ya Warioba ambayo kimsingi inasimamia misingi ya Mtanzania, lakini anajitambulisha kuwa yeye ni Mwanachama wa CCM, chama ambacho kimeikataa KATIBA ya Warioba. Jambo la ajabu ni kwamba anawashangaa Umoja wa Katiba ya Wananchi ( ya Warioba) UKAWA kumpokea mtu mmoja (LOWASA) ambae anatokea Chama kinachokataa Katiba ya Warioba (CCM).

Ukisoma hiyo logic unaweza kujiuliza, yeye ni msafi lakini ni mwanachama wa Waovu, lakini anachukia wasafi kupokea Muovu.

Toa maoni yako

well said..mkuu
uko level za juu sana kifikra
 
Safi sanaaa, sema wewe sijui kwanini? yaani ulivyo mkweli hutakiwi kukaa ccm, hauendani nao kabisaaaaa. Labda ccm ile ya zamani ya akina Nyerere sio hii ya sasa. Karibu CHADEMA mkuu tulete ukombozi wa kifikra, kiuchumi katika nchi hii
Umekubaliana na ukweli wake vizuri sana.
 
Hvi aliye weka sahihi kwenye mkataba wa richmond ni nani? Kama aliweka lowasa basi yeye ndo anapaswa kubeba msalaba maana yeye kaona mkataba mbovu na bado karidhia kuweka dole gumba lake, hakuna kiongozi hapa kama wakina,luanjo wamempeleka mjini hataweza kua mkuu wa kaya, bye bye lowasa ikulu ndo basi tena kwako

Fungua akili yako uelewe. Mkata unatengenezwa na wizara husika. Sahihi inakuwa sio moja. Ipo ya rais, mwanasheria mkuu , waziri husika na ndo inakuja ya waziri mkuu. Acha kuwa kilaza. Wote wamerizia na mamlaka kuu ambago ni ya rais imesema mkataba usainiwe je wew kama waziri mkuu unaewajibika kwa bis wako rais utafanyaje?? Jiongeze kilaza wew
 
Hvi aliye weka sahihi kwenye mkataba wa richmond ni nani? Kama aliweka lowasa basi yeye ndo anapaswa kubeba msalaba maana yeye kaona mkataba mbovu na bado karidhia kuweka dole gumba lake, hakuna kiongozi hapa kama wakina,luanjo wamempeleka mjini hataweza kua mkuu wa kaya, bye bye lowasa ikulu ndo basi tena kwako

Usikariri kwa uongo aliokupa Lowasa siku ile, ifuatilie report ya Richmond utauona udhibitisho wa uhusika wa Lowassa kulazimisha mkataba ule apewe Richmond,Lowassa aliingilia mpaka kwenye tender.

Subiri kampeni zianze,utaufahamu ukweli.
 
yeye si alituhumiwa watanzania tukasimama naye na tume sasa hawafai kwa katiba ile da kweli njaa noma ikianza panda kichwani tuhuma za makufuli nazo zinafaa awe raisi kujitoa ufahamu nako ni kipaji

.
Hii njaa ya pole pole ni kweli imepanda kichwani maani inesababisha hata nywele zisiote ilhali bado yeye ni kijana mdogo.
aombe Mungu tu kwamba leo alipokuwa anatoa huo upuuzi wake aliouita uchambuzi alikua studini kama ingelikuwa jukwaani mbele ya hadhara angepopolewa mawe kama mtikila alivyopopolewa kule Tarime akiutumikia mshahara wa mbwa aliolipwa na ccm.
.
 
Back
Top Bottom