Leo Ijumaa, Agosti 7 nitazungumzia siasa zinazoendelea nchini channel 10 saa 4 usiku, karibuni

Hamprey Polepole anasema yeye anasimamia Katiba ya Warioba ambayo kimsingi inasimamia misingi ya Mtanzania, lakini anajitambulisha kuwa yeye ni Mwanachama wa CCM, chama ambacho kimeikataa KATIBA ya Warioba. Jambo la ajabu ni kwamba anawashangaa Umoja wa Katiba ya Wananchi ( ya Warioba) UKAWA kumpokea mtu mmoja (LOWASA) ambae anatokea Chama kinachokataa Katiba ya Warioba (CCM).

Ukisoma hiyo logic unaweza kujiuliza, yeye ni msafi lakini ni mwanachama wa Waovu, lakini anachukia wasafi kupokea Muovu.

Toa maoni yako
 
Ndo maana ka-advertise sana leo watu wamcheki channel 10 kumbe alikuwa ya moyoni ya kuhukumu wengine. We ni nani hata uhukumu wengine, ni nani aliemsafi miongoni mwa waliopo ccm au hata huko ukawa, watz tuache unafiki tuwe wazalendo wa kweli.

Mbona magufuli tuhuma zake umesita kuzizungumzia
 
Inasikitisha sana kuona ukabila na undugu kama huu Tz...1. Mwenyekiti Chadema taifa- Mh FreemanMbowe (mchaga,kilimanjaro)2. Mkurugenzi wa fedha na uwekezaji - NduguAnthony Komu (mchaga,kilimanjaro)3. Mwenyekiti Bodi ya wadhamini ya chama -Mh. Philemon Ndesamburo (mchaga,kilimanjaro)4. Mkurugenzi wa Rasilimali wa chama- NduguSuzan Lymo (mchag,Kilimanjaro)5. Mkurugenzi wa Bunge na Halmashauri -NduguJohn Mrema (mchaga, kilimanjaro)6. Naibu katibu Mkuu wa chama - JohnMnyika ( mpare wa kilimanjaro mwenye maskani yake Dar)7. Mwenyekiti wa Wanawake Halima Mdee (Mpare wa Kilimanjaro mwenye maskani yake Dar es Salaam)8. Makamu mwenyekiti wa Wazee Susan Lymo (mchaga wa Kilimanjaro)9. Walinzi wote wa Mbowe (wachaga wa Kilimanjaro)10. Asilimia 98 ya madereva wa Chama wachaga wa KilimanjaroAsilimia 80 ya wabunge wa kuteuliwa wa Chadema wanatoka Kilimanjaro naArusha,wakiongozwa na Mrs wa Mbowe wa pili Joyce-Mukya, Grace Kihwelu, Suzan Lymo, Lucy Ndesamburo Owenya, Cecilia Pareso, Rebecca Mngodo na Rose Kamili.11:Tundu Lisu MB na dada yake wa kuzaliwa MBwa kuteuliwa,12:Dk Wilbroad Slaa katibu mkewe wa ndoa Mbwa kuteuliwa13:Mbowe Mwenyekiti Mkewe mdogo Mb waKuteuliwa16:Ndesamburo Mb mwanawe wa kuzaa MBkuteuliwa16:Mtei Mlezi wa chama mkwewe MboweMwenyekiti wa Chama,Hii familia inataka iongoze watu zaidi ya milioni44 haitakuja kutokea katika historia ya TanzaniaNdio wanafamilia hawahawa waliomtengenezea zengwe la kumfukuza Mh Zitto Kabwe katika chama hiki cha kifamilia baada ya kuona anakubalika ndani ya chama hicho na anauwezo wa kuwa mwenyekiti endapo angechuana na Mbowe lakini si mchaga wala mtu was kaskazini.Hapo ndipo vikao vya kifamilia vikaanza na kuamua kumtimua Zitto.Wanafamilia hawa ndio wamemuuzia chama chao Edward Lowassa kwa kiasi cha Billion 10 ili agombee urais kupitia chama hiki! Dr Slaa alipohoji akaambiwa wewe sio mwanafamilia hivyo tulikustili kwa muda tu. Ndipo slaa akagundua kuwa sio chama bali ni SACCOS na kuamua kujiengua.Mwl Nyerere aliwahi kusema, nanukuu " Mtu anayeonekana anapenda sana kwenda ikulu hafai hata kidogo ni wa kukwepa kama Ukoma".NDG watanzania huyu Lowassa anavyopenda sana kwenda ikulu tumkwepe. Hizo bilioni 10 alizonunulia chama anataka akazirudishe kwa kutuibia sisi wananchi. ZINDUKA!Kama amenunua chama akipewa nchi siataiuza kurudisha gharama zake......!!!!?
vipi mdini mkubwa wewe mwaka huu mtamjua mamvi kuwa yeye ndo aliwaweka hapo mlipo! si mliona 2010 alivyokaa kando mambo yalivyokuwa magumu!
 
nakukubali maana ulisema akuchngulia fisadi utasimama kidete kuwambia watanzania ukweli kuwa wasimchague, kazi imeanza tuko wote ,endelea kusimamia msimamo wako siasa za kinafiki zimechosha,
mimi binafsi kwa kupinga ufisadi nakukubali maana najua utalichana baba lao waziwazi hata lilipo

Mbona team escrow wote wamepita?
Au ile sio tuhuma?
Achani double standard,hakuna msafi ccm
 
Safi sanaaa, sema wewe sijui kwanini? yaani ulivyo mkweli hutakiwi kukaa ccm, hauendani nao kabisaaaaa. Labda ccm ile ya zamani ya akina Nyerere sio hii ya sasa. Karibu CHADEMA mkuu tulete ukombozi wa kifikra, kiuchumi katika nchi hii
Jamaa mkweli sana kamanda mpaka wewe umekiri.
 
Ndo maana ka-advertise sana leo watu wamcheki channel 10 kumbe alikuwa ya moyoni ya kuhukumu wengine. We ni nani hata uhukumu wengine, ni nani aliemsafi miongoni mwa waliopo ccm au hata huko ukawa, watz tuache unafiki tuwe wazalendo wa kweli.

Mbona magufuli tuhuma zake umesita kuzizungumzia

Amzungumzie makomeo asilipwe ela yake hizi siasa yeye ni mccm lazima asimame na maccm wenzake
 
vipi mdini mkubwa wewe mwaka huu mtamjua mamvi kuwa yeye ndo aliwaweka hapo mlipo! si mliona 20110 aluvyokaa kando mambo yalivyokuwa magumu!
Naona banana zinafanya kazi kichwani mwaka 20110 utafika wewe ni viroba vyako.
 
Usikariri kwa uongo aliokupa Lowasa siku ile, ifuatilie report ya Richmond utauona udhibitisho wa uhusika wa Lowassa kulazimisha mkataba ule apewe Richmond,Lowassa aliingilia mpaka kwenye tender.

Subiri kampeni zianze,utaufahamu ukweli.

Kilaza tulia. Kama ni uongo mbona tiss haija mkamata azibitishe ni kwa vip amemtuhumu kikwete ndo alikataa kuvunja mkataba? Na kama tume ya mwakyembe ina ushaidi kwanini haikumuita na kumuhoji alafu ije ituambie alichosema lowasa?? Na ni kwanini hamkushtaki kama mramba?? Ccm kwishneyyyyy.
 
Polepole leo umepita kushoto kabisaa mdogo wangu. Ngoja tukukumbushe mwaka 2005 tuliambiwa na Ccm wenyewe kuwa Dk. Salmin kuwa alihusika na mauaji ya Karume hivyo hizo zikawa ni tuhuma tosha kwa kiongozi. Swali langu mbona alipoteuliwa kuwa mjumbe wa tume ya mabadiriko ya katiba hukupinga na badala yake mkafanya kazi na tukaikubali Rasimu yenu? Hivyo tuhuma pekee ktk siasa haitoshi kuitwa mchafu.
 
mkuu tunakukubali sana kwa uzalendo wako ila wakumbushe ccm kuwa kunasiku watashindwa kukatiza mitaani na maana tuna machungu nao zaidi ya uchungu anao pata mwanamke wakati wakujifungua wasiwaze goli la mkono kabisa litaharibu nji yetu italipuka vifuwa vya wanchi vinamabomu na sumu mbaya ya pesa za sandarusi walizo gawana kama za mama yao au baba yao!!:embarassed2:
Mpaka wafuasi wa Chadema wamekiri basi jamaa yupo vizuri.
 
Makufuli anatuhumiwa kuhonga nyumba za serekali kwa mahawara wake ..hilo hajasema....ameingiza serekali hasara ya zaid ya bilion 56 ...Polepole haoni hilo ...lowasa amesema mwenyewe ..kuwa richmond ....alitaka kuvunja mkataba mkuu wa kaya ambaye ni mwenyekiti wa ccm akagoma ...nan ni fisadi hapo????

Huyu jamaa naona anaongea mambo ya kufikirika ukichukua issue ya ufisadi padlocks hafai make tuhuma zinamuangukia personality kama yeye kwa kumuuzia ndugu yake ambae alikua hajaajiriwa na alikua bado anasoma.

Alimtafutia kazi ya part-time akampa Nyumba kwa dhamana ya hiyo kazi.
 
Zile nyumba za serikali zilizouzwa nani alikuwa,wazir Leo wafanyakazi wa taasisi nyeti kama majaji wanapanga mitaani kivuko hivyo kinachoenda Bagamoyo masaa matatu uanona sawa

Lowassa angekuwa mzalendo angeipangisha hata serikali kwenye jumba lake la Singapore angalau tuwe na ubalozi.kama alivyopangisha nyumba zake za masaki.nawashangaa mnamkomalia magufulo kauza nyumba wakati mnunuzi wa hizo nyumba ni fisadi Lowassa lakini kwa kuwa nyie ni NYUMBU hamuwezi kuliona hilo.
 
Mpaka wafuasi wa Chadema wamekiri basi jamaa yupo vizuri.

Naona unajitekenya ucheke hovyohovyo kwa kelele nyingi ili majirani waone kwenu kuna ushindi ,sherehe na furahaaa kubwa.... kumbe ni msukule anatafuna chawa na kucheka. Nenda kaombew kanisani utapona
 
Leo tarehe 7 Agosti siku ya Ijumaa saa 4 hadi 5 usiku nitakuwa katika Televisheni ya Channel 10 kipindi cha Mada Moto. Huko nitazungumzia yanayoendelea kujiri katika siasa za Tanzania.

Nitasema vitu kadhaa visivyo vyepesi, lengo likiwa ni kusaidia umma wa watanzania kuujua ukweli na hatimaye wafanye uamuzi sahihi Oktoba. Ninaomba sana uhimilivu wenu ambayo pia ni ishara ya ukomavu wa siasa za ufuasi na uumini, zile zinazojenga umoja wa Taifa letu.

Naomba "share" na wajulishe watu wengi zaidi.

========================


Nami namwuliza Pole pole maswali haya anijibu:
1. Serikali iliwafikisha Mramba na Yona mahakamani kwa ubadhirifu na matumizi mabaya ya madaraka. Kwa nini haikumfikisha Lowasa mahakamani kwa kosa la ufisadi kama analo?
2. Kwa nini Lowasa hajafikishwa kwenye baraza la maadili kama wanavyohojiwa kina Chenge kama kweli hana maadili?
3. Unasemaje kuhusu Magufuli anayetuhumiwa kuuza nyumba za serikali?
4. Una uhakika gani kwamba rasimu ya Warioba itarudishwa kwenye utawala wa ccm chini ya Magufuli na siyo utawala wa Ukawa chini ya Lowasa?
NB. Leo ulikuwa unafanya kampeni ya ccm kabisa.Wananchi wa leo hatudanganyiki,mwulize Lipumba.
 
Wachambizi wa siasa wengi wamekuwa wazee wa fursa kuanzia akina naba na lepo lepo wote ni wachumia tumbo wa ccm na ni makada watachambua nini
 
Pole pole tuhuma sio hatia kaka Angu nilikua nakuheshim sana lakini kuanzia Leo nakuona kama takataka njaa itakuua ww kijana mwenzangu...unamzungumzia lowassa mbona humtaji magufuli? Ccm imekataa katiba ya warioba Leo unauponda ukawa unataka hyo katiba ya wananchi iletwe na nani?lipumba wa pili hyu
 
Si haki kumtuhumu mtu raia na kumhukumu kiasi hiki bila ushahidi. Pole pole haujathibitisha uchafu wa Lowasa. Hujaonyesha usafi wa Magufuli na CCM. Ulitegemewa ueleze matatizo ya nchi na wananchi sio umbea kama huo. Maisha kwa ujumla yameanguka. Nani mwenye uwezo wa kuyainua? Umepoteza rasilimali muda na airtime. BAHATI Mbaya wananchi waneshaamua kuwabadilisha ni ngumu. Time ll tell.
 
Back
Top Bottom