ThinkPad X250 ina mfumo wa kutambua battery halisi (genuine Lenovo) kupitia chip ndogo ya ndani, na ikibaini umeweka battery fake au iliyochoka sana, inakataa kuicharge na inatoa hiyo error ya Genuine Lenovo Battery Not Attached.
Kwa uzoefu wangu, kuna mambo machache unaweza kujaribu:
1. Jaribu BIOS update, mara nyingine firmware mpya inaweza kuruhusu kutambua battery, hasa kama ulikuwa umeweka replacement.
2. Fanya power reset, toa battery zote (internal na external), ondoa charger, kisha bonyeza power button sekunde 30. Baada ya hapo rudisha battery uwashe tena.
3. Suluhisho la uhakika, badilisha battery na original Lenovo battery yenye FRU number sahihi. ThinkPad ina battery mbili (internal 3-cell na external 3 au 6-cell), hivyo hakikisha unapata battery zinazolingana na model ya X250. Hapo ndiyo utapata tena muda mrefu wa kukaa na chaji.