Nchi Kavu
JF-Expert Member
- Sep 11, 2010
- 4,289
- 2,472
Leo kuna jamaa mmoja huko whatsapp ameonyesha mshangao wa ajabu kutokana na yale yaliyotokea siku ya Jumatano na Alhamisi (yaani clip zilizoonyesha kilichodhaniwa au kuthibitishwa ni wizi wa kura). Na kwa kuwa bado mitandao haijafunguliwa, inawezekana alipenya penya kama wengine tulivyopenya penya, ila yeye alipenya too late. Leo ndio anashuhudia maclip clip ya 'wizi wa kura'.
Jana nikiwa na bi mkubwa kwake anasema ccm imeshinda kwa kishindo mno na hakukuwa na wizi wowote. Kifupi huwezi kumbadili mtazamo wake. Bahati mbaya zaidi au nzuri yeye anapata tbc 1 tu. Hajalipia kisimbuzi. Tbc ni mashamsham tu na kusifu mwenendo wa uchaguzi.
Kwa haya mawili; kuzuia mitandao ya kijamii na kupatikana tbc tu kwa asilimia kubwa kama televisheni ya bure ni kete muhimu sana kwa ccm ambapo wameteka angalau %90 ya watanzania wote kuamini kuwa uchaguzi ulikuwa supa na jpm alistahili ushindi ule wa maporomoko.
Kuzuiwa kwa mitandao ya kijamii ndio ilikuwa kete muhimu zaidi kwa kuwa huko hakuna uhakiki. Kila mmoja ni mwandishi, ripota na mhariri. Sasa kama huyu ndugu yangu anayeishi kwenye ulimwengu wa kidijitali baada ya mitandao kufungwa tu naye akawa gizani, ni vipi kwa wale kina kayumba ambao mitandao na tv ni anasa kwao?
Hakika wamefanikiwa. Tatizo lake kufanikiwa huko ni kama mtu aliyekuwa ameoza jino kisha akaenda kulingo'a baada ya kuchomwa sindano ya ganzi. Sasa ganzi inaanza kuondoka. Maumivu yapo njiani.