Lengo lake huyu dada ni nini?

Seneta Wa Mtwiz

JF-Expert Member
Sep 23, 2013
3,601
4,087
WASH'KAJI EEEEEEEH!

TUSIKILIZANE KIDOGO.

KUTOKANA NA PILIKA ZA MAISHA HAPA MJINI,
NIMELAZIMIKA KUHAMIA HUKU PANDE ZA GOBA_JUU,
HAPA KWENYE MABANDA YA MKAA,
KARIBU NA MNARA WA AIRTEL,
UKIINGILIA NJIA YA TANKI_BOVU.

SASA KUMBE HII NYUMBA NILIYOPANGA KUNA MASISTA DUU WA CHUO KAMA 6 HIVI,
I SEE WANA NYODO NA MASHAUZI KICHIZI!

YAANI ILE SIKU YA KUHAMIA NAINGIA TU NA GUTTA LANGU LA KUKODI NIKAWASALIMIA,
INGAWA HAKUNA ALIYEITIKIA SALAM YANGU,
NIKAPIGA KIMYA NIKAANZA KUSHUSHA MIZIGO YANGU,
AMBAYO NI LILE GODORO LANGU, MKEKA, TOCHI YA BATI, STULI 1 NA
MFUKO WANGU WA KIROBA NILIMOZIWEKA NGUO ZANGU.

GHAFLA WALE WADADA WAKAANGALIANA,
KISHA
KIKAANGUSHWA BONGE LA KICHEKO
"Hee.Heeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeh!
Nainjiiiiiiiiiiiiiiiiiiii!

Ngoja nisogee pembeni kuepuka Kunguni miye!"

DAAAAAAAAAAAAAAAH!!!

NIKAJUA HAPA 1 KWA 1 WANANICHEKA MIMI NA HILI GODORO LANGU JEMBAMBA,
NINALOLITEGEMEA LA FUTI 2½,
NIKAKOSA RAHA KINOUMAH!

KWA UNYONGE,
NIKAINGIZA VITU VYANGU NDANI,
NIKARUDISHA GUTTA YA MWENYEWE.

****
KUTOKANA NA NYODO, KEBEHI, DHARAU NA MAJIVUNO YA HAWA WAPANGAJI WENZANGU AMBAO WOTE NI WADADA TU,
TENA MASISTA DUU WA CHUO FLANI HAPA MJINI,
NI
NGUMU SANA KUINTERACT NAO,
LBDA KWA SALAMU TU,
AMBAYO NAYO NI LAZIMA NIJIPENDEKEZE KUWASALIMIA,
NA KUITIKIA KWAO NI KWA MAGUMASHI MNO.
_____
SASA HAPA JIRANI KUNA NYUMBA 1 MPYA MATATA SANA,
INA KILA KITU,
IMEMALIZIWA KUJENGWA SIKU ZA HIVI KARIBUNI TU,
WENYEWE BADO HAWAJAHAMIA,
ILA KIMWONEKANO NIKAHISI YAWEZA KUWA NI YA KIGOGO FLANI WA SERIKALI KUU.

SIKU 1 MIYE NA USHAMBA WANGU NIKAWA NALISHANGAA GETI KALI LA ILE NYUMBA,
GHAFLA
LIKAFUNGULIWA,
AKATOKEA DADA MMOJA PINI MWENYE FIGA MATATA KAMA YA #Agness_Masogange
NA SURA YAKE KAMA YA YULE BINTI WA #Rais_Kagame WA RWANDA.

NIKAMSALIMIA KWA WOGA HUKU NIKIONDOKA,
YULE DADA AKAITIKIA,
KISHA AKANIAMBIA
"Samahani kwa usumbufu brother,
Naomba unielekeze wapi naweza kupata kijana wa kunisaidia kupunguza majani yaliyoota humu uani
nataka nihamie hapa kwangu Kesho,
Coz nyumba za kupanga nishachoka miye hapa mjini."

NIKAMUULIZA,
"Kwani hayo majani ni mengi sana?"

AKATABASAM' KISHA AKASEMA,
"Mmmmmmmmmh!
Tusiandikia mate Wakati wino upo,
Ingia uje ujionee."
_______
BILA KUJALI
NIKAMWAMBIA YULE DADA,
KWA KUWA JEMBE LIPO MIYE NAWEZA KUIFANYA HII KAZI, NIKACHUKUA JEMBE NIKAZILIMA NYASI ZOTE,
KISHA NIKACHUKUA UFAGIO NIKAFAGIA VIZURI,
NIKAZIZOA ZILE NYASI NIKAENDA KUZITUPA DAMPO.
____
YULE DADA HAKUAMINI JINSI NILIVYOJIONGEZA KUFANYA KAZI YA ZIADA,
ALISHANGAA SANA,
AKANIULIZA NINAPOISHI,
NIKAMWONESHA ILE NYUMBA FUPI YA KIZAMANI NILIPOPANGA.

AKASEMA

"sasa Miye' ningeomba Kama una nafasi twende Ukanisaidie kuhamisha baadhi ya vitu vichache vilivyobakia kule Sinza,
Kisha tutajumlisha malipo ya kazi Zote mbili."

KWA KUWA NA_HUSTLE DAILY SINA ISHU YOYOTE KITAA,
NIKAONA HII NI DILI YA KUPATA HATA BUKU 5 KWA LEO,
NIKAMKUBALIA.
_____
YULE DADA AKAWASHA GARI YAKE AINA YA @Toyota_Probox_Van
AKANIASHIRIA NIINGIE UPANDE WA PILI,
AKAITOA UANI,
AKASHUKA KWENDA KUFUNGA GETI,
AKAREJEA GARINI,
SAFARI IKAANZA.

KWA KUWA NI MARA YA KWANZA KUONANA,
AKAJITAMBULISHA KWA JINA,
NA KAZI YAKE NI MHASIBU WA KAMPUNI FLANI YA MAFUTA KUBWA SANA HAPA NCHINI.

TUKIWA NJIANI KUNA SEHEMU ALIINGIA,
AKA_PARK GARI AKASHUKA HARAKA AKAINGIA MINI_SUPER_MARKET YA KARIBU KUCHECK MAHITAJI FLANI MIYE NIKIWA NAMSUBIRIA NDANI YA GARI.

KUMBE PALE ALIPO_PARK NI NJIANI,
HIVYO MADEREVA KIBAO WAKAANZA KUPIGA HONI KWA JAZBA KUOMBA NJIA,
NA WENGINE WAKASHUKA NA KULISOGELEA HILI GARI WAKIWA WAMEPANIKI VIBAYA!

FASTA!
NIKAHAMIA KITI CHA DEREVE NIKARUDI REVASI,
NIKAWASHA INDIKETA YA KULIA,
NIKAINGIA SHELI ILIYOPO KARIBU UPANDE WA PILI WA BARABARA,
NIKA_PARK PEMBENI HUKU YULE DADA AKIWA AMEPIGWA NA BUTWAA KWA MBALI!

AKAVUKA BARABARA KWA HAMAKI SANA,
AKAJA PALE SHELI AKANIKUMBATIA HUKU AKINISHUKURU SANA,
MAANA'KE ILIKUWA BADO KIDOGO KILE KITENDO CHA YE' KUPARK NJIANI KISABABISHE AJALI KUBWA SANA.

TULIPOPANDA KWENYE GARI,
AKAKATAA KATAKATA KUENDESHA,
HUKU MAPIGO YAKE YA MOYO YAKIENDA KASI SANA,
AKAWA ANATAFUTA NAMBA YA SIMU YA NDUGU YAKE GANI SIJUI
NA KUMWOMBA AJE AENDESHE GARI COZ YEYE MWENYEWE YUKO OFF_MOOD,

NIKAMHURUMIA SANA JINSI ALIVYOPANIKI,
NIKAMWAMBIA "Samahani hivi kwa hii Licesnce yangu Class "C" inaweza kuwa na tatizo lolote mbele ya trafic police?
(HUKU NAMWONESHA ILE LESENI YANGU).

HAKUNIJIBU KITU, AKANIPISHA KWENYE KITI CHA DEREVA NA KUNIOMBA NIENDESHE.
NA
HAPOHAPO AKAMSITISHA YULE NDUGU YAKE ALIYEMUITA.


**
MAMA YAAAAANGUUUUUU!!!!

NIKA_APPLY ILE DRIVING STYLE ALIYOKUWA AKIITUMIA @Brother_B KULE MTWARA TUKIWA KATIKA MBIO KALI ZA KWENYE VUMBI!

NIKAIWASHA NDINGA,
NIKAINGIA BARABARANI
NA KUANZA KUIPA FIMBO MATATA SANA
HUKU NIKIZIOVATEKI AMBULANCE NA TATA ZA JESHI NA KUZIACHA ZIMEDUWAA MIDOMO WAZI!

SOON TUKAFIKA SINZA,
TUKABEBA VITU VYAKE TUKAVIWEKA KWENYE GARI,
NIKAGEUZA NDINGA TUKASEPA KURUDI GOBA!
______

TUMEFIKA PALE,
BAADA YA KUSHUSHA VITU VYOTE,
KITU CHA KWANZA YULE DADA
KUNIULIZA JINA.

NIKAMWAMBIA
"Miye Naitwa @Seneta_Wa_Mtwiz."

AKASEMA
"What?!?!?!?!
We' nd'o yule @Seneta_Wa_Mtwiz wa JF, FB & Insta??"

NIKAITIKIA KWA AIBU KIDOGO.

AKINIANGALIA KWA MAKINI SANA,
KISHA AKASEMA,
"I am really overwhelmed,
Naomba namba yako ya simu kwanza seneta,
Then naomba tuwasiliane mida please!"

AKANIPA ELFU 50 KISHA NIKASEPA.
___

SASA JIONI HII KANI_TEXT ASEMA,
"Excuse me seneta,
Nipo Kwenye maandalizi ya kupika dinner,
So niambie mapema wapendelea chakula gani coz kufikia saa tatu everything will be ok.

NIKAPIGA KIMYA.
MARA IKAINGIA MESEJI INGINE,

" Hellow Boy,
Utakula ugali, wali, au tambi?
Au
Nikuandalie chips kama wanaume wa
Dar_es_Salaam?

Tell me @Seneta."

NIKAMWAMBIA,
"Subiri kidogo,
Nitakujibu."

KISHA AKANITUMIA SMS TENA

"I am eagerly waiting for you seneta,
Au kama umechoka kutembea niruhusu nije hapo kwako kukuchukua Basi,
Coz kwenye gari mafuta yapo ya kutosha.
Tell me boy!"

AKATUMA TENA,
Nijibu Basi,
I wish ningekuandikia Kimakonde ili unielewe vema!"

KISHA KANITUMIA 100,000/=
KWA AirtelMoney.
_________________
SASA NAJIULIZA,
HUYU DADA NIA YAKE NI NINI??
 
Napaya wasiwasi kama habari hii ni ya kweli. Ila kama ni kweli, bado kuna mengi sana yanayoweza kuwa nia ya huyo dada. Labda amekupenda sababu huwa anaona mada zako kwenye social networks kama alivodai ama pengine kakuona kama ni mtu ambae utaweza kumsaidia tatizo lake fulani kutokana na hali yako ya ku-socialize.
 
Ha haaaa,,mwanangu unasimulia step by step hadi livyoshuka na kufungua geti...we noma...
 
Sasa hujaenda kula unatuuliza huyu dada nia yake ni nini? Sasa sie tutabiri? Wewe nenda kula msosi kisha akikupa na yale mambo yetu kula kisha lala hapo hapo, kukikucha kula morning glory kisha mwambie akuachie lakimoja unashida nayo alafu muulize nia yake ni nini. Baada ya hapo sasa njoo hapa tujadili nia yake kama yafaa au la
 
Hahahahahahaaaa mwisho wa habari umenichekesha bin kunifurahisha hehehehehehee
 
12479118_1035675046509978_1286653182_n.jpg

KUMBE NI WEWE HAYA NENDA KALE CHAKULA
hakukuwa na ulazima wa kufanya hivi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom