Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,894
- 20,375
Wadau, amani iwe kwenu. Eid Mubarak.
Salum Mwalimu, mtangazaji wa zamani wa Channel Ten hajaenda CHADEMA kwa bahati mbaya. Ulikuwa ni mkakati wa chama hicho kusimika mapembe yake Zenji ili kuwa na wafuasi wengi na hatimaye kufanikiwa kupata wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na wabunge kutoka visiwani humo. Ilitegemewa kuwa Salum Mwalimu atatumia muda wake mwingi kukijenga chama visiwani humo.
Hata hivyo, cha kushangaza ni kwamba Salum Mwalimu ameshindwa kabisa kufanya siasa Zanzbiar. Inadaiwa pia kuwa Salum Mwalimu hana hata nyumba ya kuishi visiwani na kwamba kuteuliwa kwake kuwa Naibu Katibu Mkuu Visiwani ilikuwa ni kutimiza tu takwa la katiba ya chama hicho.
Inadaiwa kuwa Salum Mwalimu hajawahi kufanya harakati zozote za kisiasa visiwani Zanzibar isipokuwa tu pale alipoanbatana na viongozi waandamizi wa chama chake. Kwa maana nyingine ni kwamba Salum Malimu ni Mgeni katika mazingira ya Zenji. Wa kuja.
Kinyume chake, Salum Mwalimu ametumia muda mwingi kufanya siasa Tanzania Bara na inadaiwa kuwa anaandaliwa na Lowasa ili aje kuwa Katibu Mkuu wa chama hicho mwaka 2018 ambapo inatarajiwa kuwa Lowasa atakuwa Mwenyekiti wa CHADEMA.
Kwa hali hiyo, ili CHADEMA ifanikiwe angalau kuwa na mwenyekiti wa Shehia visiwani humo, hawana budi kufanya marekebisho ya safu yao ya uongozi ili kumpata Naibu Katibu Mkuu ambaye ni mkaazi wa Zanzibar.