Lema wenzo la mafiga matatu ya Chadema

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,883
6,884
000000001chademaleo.jpg

Pichani Mjumbe wa Kamati kuu ya CHADEMA Aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema (Katikati) akisindikizwa na wanachama wa chama hicho alipokuwa akiingia katika uwanja wa Shule ya Msingi Tabata jijini Dar es Salaam jana kwa ajili ya mkutano wa hadhara.

Lema ni kati ya watu maarufu mwenye mvuto kwa wananchi kwa kujenga hoja zenye kuakisi ukweli na uhalisi ya maisha wanayoishi wananchi na matatizo yanayowakumba kutokana na mfumo wa utawala tulio nao wa kurithishana na kuriadhiana.

Chama kinahitaji watu kama akina Lema, maana wanahitajika watu wa aina mbalimbali ili kujenga nyumba imara. Matofali, saruji, mbao, kokoto, misumari, vyuma, mabati, na mengineyo ndiyo yanayofanya nyumba inapojengwa ikamilike, vinginevyo kimoja tu nyumba haitajengeka ikakamilika.​
 
Namkubali kamanda Lema Ni Jembe walidhani wamemmaliza kumbe anawamaliza ccm, wana haki ya kujuta kwanini walimpoka ubunge. wake A-Town
 
Namkubali kamanda Lema Ni Jembe walidhani wamemmaliza kumbe anawamaliza ccm, wana haki ya kujuta kwanini walimpoka ubunge. wake A-Town

Bora angebaki bungeni wangelala usingizi, lakini sasa ona Nape anavyohaha kumfuata Lema kila kona?
 
Back
Top Bottom