Lema: Rais akiendelea kufikiri yeye ni Mungu basi Mungu atasitisha maisha yake kabla ya 2020

Status
Not open for further replies.
mbona Lowasssa mlisema anaumwa atakufa?leo jamaa kamsema BWANA YULE imekuwa kosa.

swissme
Nashangaa! Waliokuwa wanasema hadharani kuwa Lowassa hamalizi wiki mbili ATAKUFA tena mbele ya ngosha walikuwa sahihi lakini Lema tena hajasema atakufa kasema atachukua maisha yake imekuwa nongwa.
Kwani kuchukua maisha Mungu ni kosa? Sii Mungu atakuwa kampenda zaidi?
Mtu anayeombewa kwa Mungu amchukue kosa liko wapi wakati Mungu atakuwa katimiza wajibu wake?
Lema angesema Alshabab watachukua maisha yake huo ndio uhaini nami ningeshangaa kama leo hii angekuwa uraiani
 
Namuunga mkono lema 200%

swissme
 
Jamani mbunge wangu lema punguza ukali kdg,watanzania tunajua vizuri tuna rais wa namna gani lakini tutulie 2020 sio mbali,ila kama wacha Mungu tuzidi tu kumuombea rais ili maamuzi na kauli zake ziwe zinaongozwa na Mungu mwenye hekima.
 
Si bure kimtokacho mtu mdomoni mwake ndicho kilicho ujaza moyo wake, pengine huyu jamaa kuna consipiracy juu ya maisha ya mh Rais anayo ijua. Maneno haya ya fanyiwe kazi kutokana na uzito wake!

Na washawasha!
 
Lema alishawafanya watu wa arusha mazezeta acha aseme lolote atakalo wamshangilie sisi tunasonga mbele
 
Jamani mbunge wangu lema punguza ukali kdg,watanzania tunajua vizuri tuna rais wa namna gani lakini tutulie 2020 sio mbali,ila kama wacha Mungu tuzidi tu kumuombea rais ili maamuzi na kauli zake ziwe zinaongozwa na Mungu mwenye hekima.
Inaudhi sana, mtu anatibua jambo ambalo watu kwa miaka mitano wamehangaika nalo nje ya utaratibu wa serikali halafu analeta majanga na huyo msimamizi mkuu badala hata ya kukaa kimya anampigia simu kunpongeza tena anaomba kuongea na mtu mwingine nje ya mfumo wa utawala kumwambia RC kafanya jambo safi sana.
Nilivyo chukia naona kama Lema katumia lugha nyepesi na ya upole kama Askofu
 
Bonge la mbunge huyo,we love him more!...muacheni mbunge wetu na vijimaneno vyenu vya barazani
 
Kifupi hii ni sawa na zile hadithi tulizokuwa tunahadithiana enzi za utoto,za YULE ZIMWI AKASEMA..wakati zimwi hujawaahi kuliona,,au Tembo AKASEMA...wakati unajua wazi tembo haongei..inshot uhai wa mtu mungu anapanga yeye mwenyewe kwa muda wake,ingekuwa hivo basi boko haram,isis n.k wangeshakufa wote,Lema kachemka
 
Pamoja na yoote ila ni hatua mbaya kufikia kuombea kifo hata kwa kiongozi wa nchi,tutulize jazba kidogo jamani !
 
Ikitokea Mapigo ya moyo ya Pombe yaka siamama kabla ya 2020, Lema una kesi ya kujibu.
Ebu ngoja niishie hapa.....
 
Mh. Lema anapaswa kufahama kuwa kama inavyoweza tokea mzazi katili na wa hovyo kuzaa mtu makini na wa kutegemewa ndivyo ilivyotokea kwa ccm. Japo wenyewe wana mengi ya hovyo hayawezi kuhusiswa na JPM na utendaji wake uliotukuka. Wananchi wengi tunamuombea asafishe uchafu uliopo ambao hata ccm waliufumbia macho. Hivyo hayo maombi yake tunayafuta kwa nguvu za Mungu na akirudia tena aangalie asijefika yeye maana Mungu hadhihakiwi.
Faida ya Lema ni ndogo mno ukilinganisha na ya mh. JPM.
Binafsi nimekasirishwa na kauli hiyo.
 
Tutamuamini vipi kuwa Rais hatafika 2020...wakati aliishasema atakayemzomwa Lowasa kwakuwa ni fisadi atapata neema za Mungu ila yeye ndio alikuwa wa kwanza kumsafisha...
 
Ukijitwalia utukufu badala, Mungu atayafupisha maisha yako.Mfano mfalme Herode alipojiona yeye ni Mungu na watu kumsifia hivyo, kwamba sauti Ya Mungu alikufa, kwa kuliwa na chango, kwa wasomaji wa Biblia. Lema amenukuu hapo ingawa hajaelezea kinabaubaga!
Basi siku moja iliyoazimiwa, Herode akajivika mavazi ya kifalme, akaketi katika kiti cha enzi, akatoa hotuba mbele yao.
22 Watu wakapiga kelele, wakisema, Ni sauti ya Mungu, si sauti ya mwanadamu.
23 Mara malaika wa Bwana akampiga, kwa sababu hakumpa Mungu utukufu; akaliwa na chango, akatokwa na roho. (Matendo Ya Mitume 12:21-23)
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom