Lema 'pasua kichwa' CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lema 'pasua kichwa' CHADEMA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by issenye, Jun 18, 2011.

 1. i

  issenye JF-Expert Member

  #1
  Jun 18, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 1,146
  Likes Received: 988
  Trophy Points: 280
  Lema 'pasua kichwa' CHADEMA[/h] * Kauli zake zadaiwa kuudhi wenzake
  * Mbunge adai zinakidhalilisha chama
  * Ashangaa baadhi kumwona kama shujaa
  * Ataka chama kimuwajibishe, vinginevyo...

  NA STEPHEN BALIGEYA, DODOMA

  KAULI za majigambo zinazotolewa na mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema (CHADEMA), kwamba ataendelea kuhamasisha maandamano usiku na mchana, zimemweka kitanzani. Hatua hiyo inatokana na baadhi ya wabunge wa CHADEMA, kudai kuwa kauli na matendo ya Lema yamekuwa yakikidhalilisha chama hicho mbele ya umma.

  Akizungumza kwa sharti la kutotajwa jina, mbunge mmoja wa CHADEMA, amesema kuwa anakusudia kuwasilisha malalamiko ndani ya chama hicho juu ya kauli hizo. Hata hivyo, amesema anatarajia kupata wakati mgumu wakati wa kuwasilisha hoja, hivyo kutokana na viongozi wa juu kukaa kimya bila kumchukulia Lema hatua za kumrekebisha. "Ni mtu anayeshangaza sana, taswira yetu mbele ya jamii imechafuka, lakini jambo la kusikitisha viongozi wa juu wako kimya na wengine wanamchukulia kama shujaa," alisema mbunge huyo.

  Ameongeza kuwa ni ngumu kwa viongozi na wabunge wa CHADEMA kujivua lawama za kuwa chama kisichojali maendeleo ya Watanzania na badala yake kuhamasisha fujo. "Kweli unaamua kuropoka mbele ya umma kwamba tutaandamana usiku na mchana, mpaka kieleweke, hivi tujiulize anataka kieleweke kitu gani wakati uchaguzi umekamilika?" alihoji.

  Pia, ameeleza kushangazwa kwake na baadhi ya wabunge wenzake wa chama hicho kujigamba mbele ya Bunge kuwa vyama vingine navyo viitishe maandamano kama vitapata watu. "Huu ni upofu wa kisiasa, hivi unaweza kusema CCM wakiamua kufanya maandamano hawapati watu, na je, unataka kusema CUF wakiandamana hawapati watu? Waache kujidanganya," aliongeza.

  Alisema iwapo vyama vingine vitakuwa na sera ya maandamano kama Chadema inavyotaka iwe, hakuna shaka nchi itakosa mwenyewe, kwani lazima kila mwananchi ana mapenzi na chama fulani, hivyo kusema hawatapata watu ni hadaa tupu.

  "Hivi kama sisi tuna watu wengi kiasi hicho, tulishindwa nini kupata viti 50 ikilinganishwa na vile ilivyopata CCM? Pamoja na udhaifu tunaozungumzia, lakini ukweli unabaki kuwa CCM ndiyo chama chenye watu wengi na siku kikiamua kujibu mapigo patakuwa hapatoshi.

  "Unajua siku ile tunajadili Muswada wa Katiba hapa Dodoma, aliamua kwenda kuhamasisha wanafunzi wa UDOM na kuwapa sh. 5,000 kila aliyekubali kuungana na fujo zake," aliongeza mbunge huyo.

  Alisema pamoja na Mkuu wa Mkoa Dodoma, Dk. James Msekela, kueleza wanafunzi kuwa anajua mgomo na fujo zao yupo mwanasiasa (mbunge) nyuma, Lema alijitokeza papo hapo na kusema yeye ndiye aliyewafuata.

  Kwa maelezo hayo, mbunge huyo anasema imefikia hatua watu wenye akili timamu wanaona kwamba, CHADEMA kinaongozwa na watu wasio na uchungu na Watanzania kutokana na matendo yanayoendelea.

  "Tumekuwa tukiwasema viongozi wa CCM ambao kila kukicha wanakemeana, lakini kwetu hata kumuonya Lema juu ya kauli zake tumeshindwa na badala yake heshima ya chama inazidi kushuka," alisema.

  Juzi jioni akichangia kwenye bajeti ya serikali kwa mwaka 2011/12, Lema alisema CHADEMA kitaendelea kuandamana usiku na mchana ili mradi taa ziwekwe barabarani.

  "Tena nataka niwaambie kuwa mimi ndiye niliyezuia maiti Tarime wasizikwe na mwenzangu Tundu Lissu akaja kupigilia msumari wa mwisho," alijigamba Lema.

  Mbunge wa Mwibara, Alphaxard Lugola, alisema mbunge huyo amezoea kuzuia maiti wasizikwe, hivyo kuna siku atazuia hata maiti za watu wengine ambazo hazijatokana na vurugu kama za Tarime.

  "Lema, kuna siku ukimaliza kugombea maiti wa Nyamongo, utagombea maiti wanaotokana na vifo vya kawaida, kwani itakuwa mazoea hivyo kuwa vigumu kuacha," alisema Lugola.

  Source: UHURU
   
 2. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #2
  Jun 18, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,344
  Likes Received: 3,111
  Trophy Points: 280
  Kama source ni uhuru(uhuni) basi no comment kwani vijarida km uhuru vipo kwa maslahi ya mafisadi.......hongera uhuru kwa kuandika habari za kupunguza ukali wa maisha ya watz na hongera kwa kuendelea kuhubiri maisha bora kwa kila mtz kwa vitendo................lakini nashauri kijarida hiki kijiunge na vijarida vingine vya udaku km risasi,
   
 3. C

  Campana JF-Expert Member

  #3
  Jun 18, 2011
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 207
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Hii porojo inanikumbusha hadithi za sungura na kaka fisi. Hata chekechea atajua jitu kubwa zima limekaa na kuitunga, maana haiingii akilini kabisa.
   
 4. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #4
  Jun 18, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,344
  Likes Received: 3,111
  Trophy Points: 280
  ***&&&&^^^%%%$$$#$#@###$%$%^^^^ zao........mi nachukia sana uhuru gazeti na redio kwani wapo kwa ajili ya mafisadi.....wakumbuke watz wa sasa sio sawa na mafisadi wa leo wanaowatumikia.......bila mafisadi uhuru lisingekuwepo mitaani kwani hakuna anayenunua.........fedha za epa/kagoda/meremeta na uchafu mwingine wooote ndiyo habari hizi za kiuchumnguzi tunazopewa na kijarida hiki
   
 5. k

  kazuramimba Senior Member

  #5
  Jun 18, 2011
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 107
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  heri mmeliona hilo huyu jamaa ni MUNGIKI amezoea fujo anataka nchi yetu iwekama somalia. Nashindwa kuelewa huyu mungiki akipewa nchi itakuwaje nadhani atakuwa dictetor mbaya kuliko Adolf hitler.Nadhani CHADEMA wanasafari ndefu sana ya kuchukua nchi hii na mavurugu yao.Shida yao inchi isitawalike tumewashtukiaaa.!
   
 6. p

  paul p raia Member

  #6
  Jun 18, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 43
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  UHURU na ukweli kuhusu CDM!!!
   
 7. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #7
  Jun 18, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,344
  Likes Received: 3,111
  Trophy Points: 280
  Kama tz ingekuwa inahofu yanayotokea somalia na alshababu basi wasomali km bashe wangekuwa walisha fukuzwa ccm na tz............hao mafisadi wanawadanganya nanyi mnadanganyika..........ila kwa kuwa huwezi kudanganya watu wote wakati wote isipokuwa unaweza kudanganya baadhi ya watu wakati fulani basi wewe ni mmoja wa hao baadhi lakini watz wa sasa sio wale wa danganyika tena.......................

   
 8. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #8
  Jun 18, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Uhuru siyo reliable source ya information Mkuu, Potezea hiyo.
   
 9. P

  PR Member

  #9
  Jun 18, 2011
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Najua watu wasiotaka kuambiwa ukweli watakataa lakini huu ndio ukweli wenyewe. Wote wanaweza kuhamasisha maandamano ila wanachozidiana kwa hili ni jee hayo maandamano yana tija yoyote au ni kujitafutia umaarufu?
   
 10. F

  FRANK MICHAEL Senior Member

  #10
  Jun 18, 2011
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 150
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Tena wana jf mfahamu hayo ni mawazo ya mwahariri kumfurahisha nape na mafisadi wenzake wanajua itajenga uhasama ndani ya chadema chutu poleni sana mafisadi
   
 11. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #11
  Jun 18, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,344
  Likes Received: 3,111
  Trophy Points: 280
  Km maandamano yana tihja au hayana nakupa assignment......nenda kawaulize ivory coast baada ya hapo nenda tunisia, nenda misri, nenda yemen halafu njoo na jibu sio kuuliza maswali yasiyokuwa ya msingi............

   
 12. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #12
  Jun 18, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Lema anaboa men!!
   
 13. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #13
  Jun 18, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,344
  Likes Received: 3,111
  Trophy Points: 280
  Hey!...na wewe umetokea wapi tena na avatar yako hiyo?....

   
 14. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #14
  Jun 18, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Avatar yangu haikuhusu! Concentrate na issue za Lema
   
 15. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #15
  Jun 18, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,344
  Likes Received: 3,111
  Trophy Points: 280
  Ungekuwa unashaurika ningekushauri uibadili......anyway kwa kuwa watoto hawatembelei hapa basi nakushauri uiache tu...

   
 16. S

  SEAL Team 6 JF-Expert Member

  #16
  Jun 18, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 655
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  UHURU- Hivi hili gazeti bado lipo !!!, kwa mara ya mwisho lilichapishwa lina?
   
 17. Baba V

  Baba V JF-Expert Member

  #17
  Jun 18, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 19,507
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 160
  Si lazima amfurahishe kila mtu lakini cha msingi ni mwiba kwa wasioitakia mema nchi hii. ki ufupi namkubali sana kwa ujasiri wake. Nchi hii tunmezidi kwa ukondoo. big up Lema
   
 18. Kurunzi

  Kurunzi JF-Expert Member

  #18
  Jun 18, 2011
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 4,003
  Likes Received: 325
  Trophy Points: 180
  Binafsi naweza kusema Lema kweli ni mwanaharakati jasiri mpambanaji lakini asipojiangalia vizuri siku za usoni sifa hizo nzuri zitabadilika kuwa udhaifu wake mkubwa asipotumia busara alipozua miili kuzikwa sio tatizo lakini sio busara kujisifu kwa kufanya hivyo kusema mimi ndiyo nilizuia miili kuzikwa ah busara inapungua lakn anamuda wa kujirekebisha
   
 19. mwanapolo

  mwanapolo Senior Member

  #19
  Jun 18, 2011
  Joined: Mar 29, 2011
  Messages: 194
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Lema tumemchagua wenyewe sababu ni mpambanaji. Wote mnao mlalamikia ina onyesha amewashika pabaya na sio mkazi wa Arusha
   
 20. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #20
  Jun 18, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,671
  Trophy Points: 280
  Namjua vizuri Lema ni pumba sana, upeo wake wa ufahamu ni mdogo sana, ni mtu wa Controversy kila wakati sijui huyo ubunge kaupataje
   
Loading...