Lema: Dhambi ya CCM ni kubwa imekaribia kwenye mauti

Tunajua upinzani unatamani sana cku moja wao wawe watawala, lakini sio kwa mbinu hii ya Lema.

Kama ccm ina dhambi sana utakatifu wa Chadema ni upi?
 
Ninapojiuliza hili andiko la dhambi kubwa ni uoga limeandikwa kwenye kitabu gani hicho ili niamini unabii
 
Lema ni msanii na tapeli la kisiasa.
Lema huyu huyu alituambia kumtukana na kumuita Lowassa fisadi,ni baraka kwa Mungu,leo wapo wote
Sitashangaa kesho nikimsikia Lema amejiunga na ccm
 
Hakika kibanzi ni kwa mwenzio chako hakipo

Ama kweli siasa ni sayansi ambayo haitaji experiment nikusema tu wadanganyika ndio wasiojitambua

Najiuzulu siasa natumikia watanzania alafu anaingia makinikia

Mwembeyanga watajwa mapapa leo safi
 
Nampongeza waziri mkuu kupiga marufuku viroba mapema maana tushaaza kutambua sura halisi za vijana na akili pia hakuna wa kumdanganya tena awadanganye hao hao
 
Haya yapo yatakuja tokea ccm kuachia ngazi lakini bado muda wake kitakuja chama cha upinzani kweli ambacho sio cha watu dizain ya hawa wapigaji hata chadema itafikia kitajichuja na kubaki walio safi - hivi bado kinakusanya ili baadae wajichuje wamakandokando watatafuta tu sehem nyingine wananchi wanahitaji viongozi safi hata kama ni upinzani sio wamakandokando hivi sasa wameshaelimika watu, hoja ukituhumiwa fisadi eti ushahidi au mahakamani katika siasa hakuna haja ya ushahidi wa kuona kwa macho ni vitendo vyako tu ndo unatosheleza kukuhukumu kuwa ni......
 
ccm wasome kitabu kinachoitwa ",MAMBO YA NYAKATI" watajifunza mengi.....huyo rais wa wanyonge wa chato anawaingiza kingi maana anaharibu uchumi wa nchi km mugabe
 
Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amesema kuwa kitu cha msingi ambacho wananchi wanatakiwa wajue ni kwamba Chama cha Mapinduzi (CCM) kimefika mwisho huku akisema mshahara wa dhambi ni mauti na Chama hicho kina dhambi kubwa sana iliyokaribia mauti.

Lema ameyasema hayo Jumapili hii katika uwanja wa Shule ya Msingi Mhandu mkoani Mwanza ambako Mbowe alikuwa anahutubia mkutano wa hadhara wa kampeni za udiwani katika uchaguzi mdogo utakaofanyika Novemba 26,2017.

“Tundu Lissu yuko hospitali ana uguza majeraha ya risasi si kwasababu alifumaniwa, si kwasababu ni mwizi ni kwasababu ya kupigani haki zenu, dhambi kubwa kuliko dhambi zote duniani ni uoga na sasa kitu cha msingi sana mjue tu kwamba CCM imefika mwisho. Mmesikia Zimbabwe waliompindua Rais Mugabe sio Wapinzani aliokuwa ana wapiga mabomu ni Wanajeshi aliwavalisha yeye vyeo, walewale machinga waliokuwa wanamshangilia Mugabe leo wameandamana kusema Mugabe toka, nitamshukuru Mungu sana siku nikiona hiyo siku inafika mahali hapa, mshahara wa dhambi ni mauti na dhambi ya CCM ni kubwa sana imekaribia kwenye mauti kwasababu leo yupo Mwenyekiti wetu hapa na Katibu wetu Mkuu yuko mahali hapa na Lazaro Nyalandu yuko hapa,” alisema Lema.

“Ila niwaombe watu wa Kata hii, ukiibiwa kura unaenda nyumbani mwanaume una mwambia mke wako tumeibiwa kura mama mtafutie sketi huyo baba kama ambavyo Katiba inaruhusu kuzuia uhalifu wa aina yoyote kwa mwananchi yoyote ndivyo ambavyo Katiba ina ruhusu kulinda kura zako viongozi wameandaa mawakala wazuri sana kwahiyo ukishaa piga kura kaa mita 100.”

Source: Bongo5
Huo ni uchochezi asubiri kuitwa akafafanue vizuri hiyo kauli yake
 
Naona bangi zinaanza kumzidi, tangu lini Lissu ndo sera ya chadema
 
Eti wabaki mita 100?, mgambo wa ccm wataua mtu. wale hufanya kazi bila weledi.
 
Waache kuvunja sheria makusudi ili waone kama kutakuwa na la kuwaongelea.
 
Back
Top Bottom