Lema: Dhambi ya CCM ni kubwa imekaribia kwenye mauti

Lema: Dhambi ya CCM ni kubwa imekaribia kwenye mauti

Rosh Hashannah

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2017
Posts
3,415
Reaction score
2,044
Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amesema kuwa kitu cha msingi ambacho wananchi wanatakiwa wajue ni kwamba Chama cha Mapinduzi (CCM) kimefika mwisho huku akisema mshahara wa dhambi ni mauti na Chama hicho kina dhambi kubwa sana iliyokaribia mauti.



Lema ameyasema hayo Jumapili hii katika uwanja wa Shule ya Msingi Mhandu mkoani Mwanza ambako Mbowe alikuwa anahutubia mkutano wa hadhara wa kampeni za udiwani katika uchaguzi mdogo utakaofanyika Novemba 26,2017.

“Tundu Lissu yuko hospitali ana uguza majeraha ya risasi si kwasababu alifumaniwa, si kwasababu ni mwizi ni kwasababu ya kupigani haki zenu, dhambi kubwa kuliko dhambi zote duniani ni uoga na sasa kitu cha msingi sana mjue tu kwamba CCM imefika mwisho. Mmesikia Zimbabwe waliompindua Rais Mugabe sio Wapinzani aliokuwa ana wapiga mabomu ni Wanajeshi aliwavalisha yeye vyeo, walewale machinga waliokuwa wanamshangilia Mugabe leo wameandamana kusema Mugabe toka, nitamshukuru Mungu sana siku nikiona hiyo siku inafika mahali hapa, mshahara wa dhambi ni mauti na dhambi ya CCM ni kubwa sana imekaribia kwenye mauti kwasababu leo yupo Mwenyekiti wetu hapa na Katibu wetu Mkuu yuko mahali hapa na Lazaro Nyalandu yuko hapa,” alisema Lema.

“Ila niwaombe watu wa Kata hii, ukiibiwa kura unaenda nyumbani mwanaume una mwambia mke wako tumeibiwa kura mama mtafutie sketi huyo baba kama ambavyo Katiba inaruhusu kuzuia uhalifu wa aina yoyote kwa mwananchi yoyote ndivyo ambavyo Katiba ina ruhusu kulinda kura zako viongozi wameandaa mawakala wazuri sana kwahiyo ukishaa piga kura kaa mita 100.”

Source: Bongo5
 
Kila siku verbal diarrhea ya huyu jamaa ni bora jana!
He sounds logical and intellect when he shuts his mouth!
 
Vijana wapenda haki ktk nchi hii , hawaitaki ccm na wanaichimbia kaburi ambalo liko karibu kukamilika ili mazishi ya ccm yafanyike na wala haita sikika tena, wala kwenye vitabu vya historia haita itajika hilo jina ccm kuonekana.
 
Vijana wapenda haki ktk nchi hii , hawaitaki ccm na wanaichimbia kaburi ambalo liko karibu kukamilika ili mazishi ya ccm yafanyike na wala haita sikika tena, wala kwenye vitabu vya historia haita itajika hilo jina ccm kuonekana.
Kwa kuwategemea Nyalandu, Lowassa na Sumaye, watu waliomaliza carrier yao ya kisiasa, mnachekesha tu watu walio na huzuni !
 
lema.jpg


Mbunge wa Jiji la Arusha Godbless Lema amewafahamisha wananchi amesema kitu cha msingi ambacho wananchi wanatakiwa wajue ni kwamba chama cha mapinduzi (ccm) kimefika mwisho na kusisitiza kuwa mshahara wa dhambi ni mauti na chama hicho kina dhambi iliyokaribia mauti
 
Ila kweli mshahara wa dhambi ni mauti, hasa inapokuwa mojawapo ya dhambi hizo ni kumwaga damu za watu.
 
Jana kule Mwanza kuna mbunge wa UPINZANI kaongea mambo yaliyowazi kabisa kuwa ni ya kuchonganisha raia na serikali.

Vyombo vya dola kwa nini mtu huyo hajafikishwa mahakamani hadi wakati huu?!

Mtu anayehamasisha watu waipindue serikali na anatamani sana hilo litukie-anaachajwe uraiani hadi wakati huu?!

Naamini mda si mrefu atawajibishwa kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi!Waropokaji hao kwao ni gerezani.
 
Kuleta maendeleo kumewashinda mmebaki kukamata wanaowakosoa kwa kuwapa ukweli mchungu
 
Hahah..waanze na king mbowe kwanza ndio tutaamini maneno yao..wamtoe kwenye kiti..
Lema bwana huwa habalehi tu katika siasa pamoja na kumtukana kote lowasa kisha kumpigia kampeni awe rais.
 
Ukweli hauzuiliki kwa nguvu za dola, hivyo vyombo vya dola vimeshindwa kesi zote hadi wamechoka sasa.
 
Back
Top Bottom