Lema azidi kumbana Mulongo

Lema azidi kumbana Mulongo

rosemarie

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2011
Posts
6,887
Reaction score
3,446
Arusha. Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema amewatumia salamu Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo na Mkuu wa Wilaya ya Arusha, John Mongela akiwataka wasithubutu kuvuruga uchaguzi wa kata nne utakaofanyika mwezi ujao.

Uchaguzi mdogo wa kata nne za wilaya za Arusha umepangwa kufanyika Juni 16, mwaka huu.

Akihutubia mkutano wa hadhara kwenye Uwanja wa Ngarenaro, Arusha Lema alisema yeye na wafuasi hawatakubali kuona wakipokonywa haki yao ya kuchagua viongozi wanaowataka kwenye uchaguzi huo.

Amemtunishia misuli Mkuu wa Mkoa ikiwa siku chache baada ya kuachiwa kwa dhamana baada ya kupandishwa kizimbani kwa tuhuma za uchochezi.

Mbunge huyo anatuhumiwa kuwahamasisha wanafunzi wa Chuo cha Uhasibu Arusha kumzomea Mulongo wakati alipokwenda kuwatuliza walipotishia kuandamana baada ya kifo cha mwanafunzi mwenzao, Henry Kago, wiki iliyopita. "Ninawatahadharisha viongozi hawa wasithubutu kutumia vyombo vya dola kwa nia ya kukipa ushindi Chama cha Mapinduzi (CCM) kwenye kata hizo. Waache uchaguzi ufanyike kwa amani.

"Tutahakikisha tunapiga kampeni usiku na mchana na pia tutalinda kura zetu siku ya uchaguzi ili tusipokonywe," alisema.
Hata hivyo, Mkuu wa Mkoa na Mkuu wa Wilaya walipotafutwa kuzungumzia madai hayo ya Lema hawakupatikana na walipopigiwa simu, ziliita bila ya kupokewa na hata walipotumiwa ujumbe mfupi wa maandishi (sms) hawakujibu.

Lema alisema ataripoti bungeni Jumatatu ijayo lakini atarejea Arusha kabla ya kuanza kwa kampeni za uchaguzi huo mdogo zilizopangwa kuanza Mei 15 na kumalizika Juni 15, mwaka huu.

"Niko tayari kuachia posho za bungeni katika muda huo ili nishiriki kwenye kampeni za uchaguzi huu," alisema Lema.
Joto la uchaguzi huo limeanza kupanda katika Jiji la Arusha katika Kata nne za Themi, Kaloleni, Elerai na Kimandolu na watu wapatao 60 wamechukua fomu ili kuwania kupitishwa na Chadema kugombea nafasi hizo.

Hata hivyo, amelalamikia kutoitishwa kwa uchaguzi mdogo wa Kata ya Sombetini ambayo pia haina diwani baada ya Mawazo Alphonce kupitia CCM kujitoa na kujiunga na Chadema na ameapa kupigania kuitishwa kwa uchaguzi wa Sombetini pia katika kipindi hicho.
 
Duuu..! Huyu mtoto mbona msumbufu sana..? Nina imani soon atakuwa rais wa Arusha..!
 
Lema, jembe la Ukweli tupo nyuma yako ktk hili.
 
Cha msingi ni kufanya uchaguzi wa haki na amani, tabia ya wakuu wa mikoa na wilaya kutumia jeshi la polisi kisiasa au kama ni lao iachwe mara moja dhana ya polisi ni kulinda watu na mali zao na si kuvunja amani bila shaka muda wake umefika.
 
hivi uyu msengerema mkuu wa mkoa ajahamishwa tu
 
Subiri tu anaendelee na tabia yake. Morani wa Kimasai huwa hawajaribishwi. hufanya kweli
 
Style yetu ile ile tu,unapiga Kura kisha unarudia hatua 10 nyuma na kulinda Kura,vurugu wataanzisha wao sie ni haki tu wakishinda kwa haki wapeni haki yao na tukishinda kwa haki pia tupewe haki yetu
 
Style yetu ile ile tu,unapiga Kura kisha unarudia hatua 10 nyuma na kulinda Kura,vurugu wataanzisha wao sie ni haki tu wakishinda kwa haki wapeni haki yao na tukishinda kwa haki pia tupewe haki yetu

huo ndo utaratibu wa uchaguzi? Baada ya kupiga kura unatakiwa uondoke kituo cha kupigia kura. Ila wakati wa kutangaza matokeo unaruhusiwa kuhudhuria.
 
Tamisemi wabanwe kuhusu uchaguzi kata ya sombetini.kwa nini iachwe?mbona magamba wamekuwa watu wa vituko na uvunjaji katiba ya nchi?
 
Safi sana Kamanda Lema! Tupo pamoja! Wape vidonge vyao vilaza hao
 
huo ndo utaratibu wa uchaguzi? Baada ya kupiga kura unatakiwa uondoke kituo cha kupigia kura. Ila wakati wa kutangaza matokeo unaruhusiwa kuhudhuria.

unachoandika hapa ni nini?akili yako imekaa kuropoka tu...hatua 100 ndio utaratibu...haina maujanja hii...usiwe kama akil zimekazwa sana hadi unafikiria posho ya Lumumba kila sekunde
cc : CCM original
 
Last edited by a moderator:
tuondoke twende wapi? wacmamizi wa uchaguzi wanatoka tume huru? ama tume iliyochaguliwa na Rais pendwa? tutaondoka eneo la uchaguzi as usual na kama askari watatuamru kupotea kabisa mpk mda wa kuhesabu Kura pia tutaonyesha ushirikiano ila home hatuendi kwani mda wakuhesabu Kura tunaujua na haki ya mpiga Kura tunaijua
 
ahamishwe apelekwe wapi? Mnamwogopa sana CHADEMA jinsi anavyowanyoosha? Atabaki Arusha aweke Asusha yenye amani.

APELEKWE BAGAMOYO/PWANI WAKANYWE WOTE CHAI
 
kamanda nakuaminia sana unaweza kwa sababu mambo ya ukweli unayatamka kwa ukweli wake na siyo kwa kuuma maneno
 
Back
Top Bottom