Juzi nilileta thread humu JF kuhusu huo mradi nakauliza Lema, naye anahusika sikupata jibu sahihi..
Leo ndio nimepata jibu, hivi huo mradi ni wa Chadema au CCM? huo mradi ni kwa manufaa ya wana Arusha.
Nashangaa Lema kujipa majukumu ya Shekh Yahaya utabiri
Juzi nilileta thread humu JF kuhusu huo mradi nakauliza Lema, naye anahusika sikupata jibu sahihi..
Leo ndio nimepata jibu, hivi huo mradi ni wa Chadema au CCM? huo mradi ni kwa manufaa ya wana Arusha.
Nashangaa Lema kujipa majukumu ya Shekh Yahaya utabiri
Usifike huko Mh. Lema ni mjumbe halali wa Baraza la madiwani, anayofursa ya kwenda kuhoji huko kwenye vikao vyao
Hata kuamia Vijiji vya Ujamaa ilikuwa nia njema kabisa ya Mwl. Nyerere, lakini implementation yake ilileta madhara makubwa sana kwa wananchi hata kupelekea wengine kuliwa na simba. Huyu anayejiita Meya naona hakujifunza kitu kupitia mradi ule wa Vijiji vya Ujamaa. Wananchi lazima washirikishwe na waandaliwe, wao si maboga unayoweza kuyabeba tu na kuyapeleka unapotaka wewe pasi na ridhaa yao wenyewe.Mh. Lema kubali maendeleo yaje kwa faida ya wengi; hizo guest house za Kaloleni zina tija kidogo sana kwa uchumi wa jiji letu la Arusha
Tunahitaji maendeleo lakini pia utaratibu ufuatwe, safi Mbunge wetu Arusha,
Lakini, kuna muwekezaji wa ndani kama nimemnusa ktk huu mradi, yule mzee mamvi!
Mh. Lema kubali maendeleo yaje kwa faida ya wengi; hizo guest house za Kaloleni zina tija kidogo sana kwa uchumi wa jiji letu la Arusha
Gurtu,Tazama hapo kwenye red: mradi wenye manufaa kwa wana Arusha! Ni manufaa gani? Hivi kwa akili yako unaweza kusema kuwa ni jambo la maendeleo kwa mfano; mwekezaji anapopewa ardhi ambayo ilikuwa yako bila wewe kuulizwa na mwisho wa yote mwekezaji ajitafutie faida yake? Kuna mwekezaji gani kutoka wa kigeni aliyekuja kuwekeza hapa TZ na mwisho tukafaidika Watanzania?
Hii nchi kama tunategemea kuijenga kwa nguvu za uwekezaji kutoka nje, je, yatakuwa maendeleo kweli ya Watanzania? Chukua mfano mdogo, mwekezaji anawekeza kijiji kwako katika mradi unaozalisha faida ya Bilioni moja kwa mwaka. Katika kijiji hicho pato la wananchi wake ni miioni 50 kwa mwaka. Jumlisha pato la mwekezaji na wanakijiji unapaata bilioni moja na milioni hamsini kwa mwaka. Pato la kijiji hicho kwa mwaka (ukijumlisha na la mwekezaji) kwa mwaka litakuwa juu kuliko la baadhi ya mikoa katika nchi hii. Je, kiwango cha maisha ya wananchi yataendana na pato hilo?
Usidanganyike na uwekezaji ambao hauzingatii kuinua maisha ya wananchi kama ambavyo sasa hivi unafanyika Tanzania. Hakuna nchi inayofanana na Tanzania katika dunia hii kwa kufanya mamvo yake kiholela. Kitu cha ajabu zaidi ni kuwa, pamoja na kuona jinsi viongozi wa serikali wanavyotupeleka jehanamu, bado kuna wananchi kama ritz wanaendelea kuunga mkono upuuzi kama huu. Pole ritz kwa sababu unapenda uwekezaji huu wa Kitanzania. Ila tunajua kuwa "ukipenda chongo huita kengeza". Sii furaha ya Watanzania kuona kuwa mji umejengeka vizuri na hivyo kuwa kama mapambo kwao wakati wao wanashindwa kumudu maisha na wao wakiutazama kutoka pembeni kule ambako watakuwa wamehamishwa bila hata fidia ya maana.
Watanzania tupiganie haki zetu na wala tusikatishwe tamaa na kina ritz ambao wamekubali kula makombo na matapishi ya Wawekezaji.
Gurtu,
Nadhani ufahamu chochote unacholeta wewe ni upambe kwa Lema tu.
Huo mradi utaleta manufaa makubwa kwa wana Arusha, watajenga Shule, Hospitali, Maduka makubwa, Maengesho ya magari, hayo sio maendeleo?
Hata kuamia Vijiji vya Ujamaa ilikuwa nia njema kabisa ya Mwl. Nyerere, lakini implementation yake ilileta madhara makubwa sana kwa wananchi hata kupelekea wengine kuliwa na simba. Huyu anayejiita Meya naona hakujifunza kitu kupitia mradi ule wa Vijiji vya Ujamaa. Wananchi lazima washirikishwe na waandaliwe, wao si maboga unayoweza kuyabeba tu na kuyapeleka unapotaka wewe pasi na ridhaa yao wenyewe.
Gurtu,
Nadhani ufahamu chochote unacholeta wewe ni upambe kwa Lema tu.
Huo mradi utaleta manufaa makubwa kwa wana Arusha, watajenga Shule, Hospitali, Maduka makubwa, Maengesho ya magari, hayo sio maendeleo?
Usipende kujiangalia umasikini wako uka-Generalize kwa watu wooote!!!Mimi na wewe tukishirikishwa tuna akiba yoyote ya kuwekeza kwenye huo mradi? Ni kweli Mh. Lema anaposema wananchi hawajashirikishwa anazungumzia wale wafuasi ambao huwa wanaandamana naye au kuna kundi la wafanyabiashara wachache (wale wenye hardwares) anawazungumzia kwa mgongo wa walalahoi? .......changanya na za kwako
wewe kichaa, unaposema huo mradi ni kwa mnufaa ya wana Arusha unamaanisha nini? kwani watu wa kaloleni watakaopomolewa vibanda vyao bila fidia sio wana Arusha? Watanzania na wana Arusha kwa ujumla wanahitaji maendeleo ya watu na sio maendeleo ya vitu.Juzi nilileta thread humu JF kuhusu huo mradi nakauliza Lema, naye anahusika sikupata jibu sahihi..
Leo ndio nimepata jibu, hivi huo mradi ni wa Chadema au CCM? huo mradi ni kwa manufaa ya wana Arusha.
Nashangaa Lema kujipa majukumu ya Shekh Yahaya utabiri
wameanza dar sasa arusha inayofuata ni mwanza then moshi then kitakachoendelea ni kutawaliwakama kingamboni kama arusha!