Lema asikitishwa uandikishaji kuahirishwa.

chakii

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
19,710
22,776
MBUNGE wa Arusha Mjini, Godbless Lema amesema uandikishaji wapigakura katika Daftari la Kudumula Wapigakura, uliokuwa uanze jana na kuahirishwa, umewasikitisha kama chama kwa kuwa wananchi hawakupewa taarifa za usitishwaji wa uandikishaji huo.



Licha ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kutoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu kusitishwa huko, wananchi walijitokeza jana kwenye vituo vyao kwa ajili ya kujiandikisha.



Lema alisema hayo jana jijini hapa wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari na kulalamika kuwa wananchi hawajaelezwa sababu ya kuahirishwa kwa uandikishaji huo, ambao awali ulikuwa ufanyike Juni 12 na kutangazwa tena kuwa utafanyika Juni 9 na juzi NEC ilitangaza kuwa utafanyika Juni 15 mwaka huu.




Alisema NEC wameahirishwa bila kutoa taarifa kwa viongozi wa vyamambalimbali vya siasa, ambao walijipanga vyema kuhakikisha zoezi hilo linafanyika na wananchi wanajiandikisha ili waweze kuwa na vitambulisho hivyo kwa ajili ya kupiga kura katika uchaguzi mkuu mwaka huu.“Kuahirishwa kwa zoezi hili ni hujuma zinazofanywa na NEC, maana wametangaza kuahirisha zoezi wakati wananchi leo walikuwa wamejitokeza katika vituo vilivyopangwa kuanza zoezi hili la uandikishaji, lakini tunasema hizi ni hujuma za makusudi za kuhakikisha wannachi hawaandikishwi, lakini na sisi tunasema tutaendelea na uhamasishaji wa kuajiandikisha kwa wananchi ili tarehe hiyo nyingine wajitokeze kwa wingi”.



Pia, ingawa kuna ongezeko la idadi ya kata za jiji hilo, ongezeko hilo si kigezo cha kuahirisha uandikishwaji, lakini na sisi tutaendelea na kampenizetu za kata kwa kata, kuhamasisha uandikishaji hadi zoezi hilo litakapoanza la uandikishwaji kwa mfumo wa BVR.




Mratibu wa Uchaguzi Mkoa wa Arusha, Richard Kitwega aliomba radhi kwa wananchi wa Mkoa wa Arusha, kutokana na tume kusitisha zoezi hilo na kutaja sababu zilizofanya uandikishwaji huo kutofanyika jana kuwa ni ongezeko lakata, vifaa vya kuandikisha kutokamilika ikiwemo wino na kuahidi kuwa zoezi hilo litafanyika Juni 15 mwaka huu.



Awali, juzi Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Juma Idd alisema zoezi hilo lilitakiwa kuanza jana kwa kata sita na baada ya siku saba zoezi hilo litaendelea katika kata nyingine za jiji la Arusha.


Chanzo : Habari Leo
 
Back
Top Bottom