Lema ang'aka kuhusu Zanzibar, Amwambia Chenge asijione Mungu mdogo

Kibo10

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
11,277
8,850
Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema amesema leo bungeni suala la Zanzibar si la kichama,Ni suala la nchi na lisipotafutiwa ufumbuzi lina athari kwa kila mtu.

Lema amewaambia wabunge wa CCM hii nchi ikiharibika hata watoto wao wataharibikiwa na hawawezi kukaa madarakani kwa maisha yao yote.

Lema amemtolea mfano mbunge Marry Nagu na kumwambia akumbuke serakali iliyopita alikuwa waziri,Lakini leo naye anauliza maswali ya nyongeza.

Lema alienda mbali zaidi na kumwambia Mwenyekiti wa bunge Chenge asijione ni mdogo wake Mungu kwa kukalia kiti cha spika.

Godbless Lema nimegundua ni mbunge bora wa muda wote,Viva Chaliii
 
Huku akinukuu maandiko kadhaa matakatifu Mh Lema ametamka wazi wazi na kumtaja Maalim Seif kama mshindi halali wa uchaguzi halali uliofanyika oct 25 ,

Hakika Mh Lema harembi ! amemnukuu bwana Yesu kristo pale alipotahadharisha kuhusiana na kuzima uhuru wa maoni na kuzuia TBC kuonyesha matangazo ya bunge , amesema ukizuia wanadamu basi mawe yataimba badala yao .

Kiukweli Mh huyu ameongea kwa uchungu na uzalendo wa hali ya juu sana !

Wito wangu kwa viongozi wa nchi hili suala la Zanzibar lisifanyiwe mchezo , ni bomu la hatari sana !
 
Mbunge wa arusha mjini Godbless lema amesema leo bungeni swala la Zanzibar si la kichama,Ni swala la nchi na lisipotafutiwa ufumbuzi lina athari kwa kila mtu,
Lema ameenda mbali zaidi na kuwaambia wabunge wa Ccm hii nchi ikiharibika hata watoto wao wataharibikiwa na hawawezi kukaa madarakani kwa maisha yao yote.
Lema amemtolea mafano mbunge Marry Nagu na kumwambia akumbuke serakali iliyopita alikuwa waziri,Lakini leo naye anauliza maswali ya nyongeza.
Lema alienda mbali zaidi na kumwambia Mwenyekiti wa bunge Chenge asijione ni mdogo wake mungu kwa kukalia kiti cha spika.
Godbless Lema nimegundua ni mbunge bora wa muda wote,Viva Chaliii
Hivi mkuu bado ulikuwa hujui kuwa mheshimiwa lema kuwa ni lulu ktk siasa za tanzania?
 
Mbunge wa arusha mjini Godbless lema amesema leo bungeni swala la Zanzibar si la kichama,Ni swala la nchi na lisipotafutiwa ufumbuzi lina athari kwa kila mtu,
Lema ameenda mbali zaidi na kuwaambia wabunge wa Ccm hii nchi ikiharibika hata watoto wao wataharibikiwa na hawawezi kukaa madarakani kwa maisha yao yote.
Lema amemtolea mafano mbunge Marry Nagu na kumwambia akumbuke serakali iliyopita alikuwa waziri,Lakini leo naye anauliza maswali ya nyongeza.
Lema alienda mbali zaidi na kumwambia Mwenyekiti wa bunge Chenge asijione ni mdogo wake mungu kwa kukalia kiti cha spika.
Godbless Lema nimegundua ni mbunge bora wa muda wote,Viva Chaliii
Chadema ni matapeli hawaaminiki tena,,mpaka june,2015 walikua wanamwita lowassa fisadi mkuu,na lema alifikia kusema ni thawabu kwa mungu kumwita lowassa fisadi,leo anambeza Nagu?
 
Tatizo la ccm wanasubiri mpaka wakose tonge, ndiyo waanze muongea ukweli, mfano :- Msekwa, Sitta, Membe etc, lakini wakiwa kwenye kijani & njano zao, daaaaaaah! Unaweza sema labda wao hawana mpango wa kuja kuishi kwenye hii Nchi yetu ya TZ.
 
Chadema ni matapeli hawaaminiki tena,,mpaka june,2015 walikua wanamwita lowassa fisadi mkuu,na lema alifikia kusema ni thawabu kwa mungu kumwita lowassa fisadi,leo anambeza Nagu?
Endelea kubakia ktk historia ya vita ya kagera
 
Back
Top Bottom