Lema amvizia Makinda, Je atamtega na nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lema amvizia Makinda, Je atamtega na nini?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by JOHN MADIBA, Jul 1, 2011.

 1. JOHN MADIBA

  JOHN MADIBA JF-Expert Member

  #1
  Jul 1, 2011
  Joined: Jan 30, 2011
  Messages: 251
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  MBUNGE wa Arusha Mjini, Godbless Lema (CHADEMA), amemtaka Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anne Makinda, kumpa nafasi ya kutoa ushahidi wake bungeni juu ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda, kusema uongo bungeni kabla ya hukumu ya mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe (CHADEMA).Katika mkutano wa pili wa Bunge uliofanyika Februari mwaka huu, Lema alipewa muda wa kuthibitisha tuhuma alizozitoa bungeni kuwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, hakusema ukweli juu ya vurugu, vifo na majeruhi waliopatikana baada ya polisi kuingilia maandamano ya CHADEMA Januari 5 mwaka huu mkoani Arusha.

  Lema, alisema baada ya kupewa agizo hilo, aliwasilisha vielelezo vyake kuthibitisha uongo wa Pinda, lakini alidai mpaka sasa hajaona jitihada zozote za Spika Makinda kumpa nafasi kuueleza.

  Alibainisha kuwa ameshangazwa na uharaka wa Spika Makinda, kumpa nafasi Zitto, kuthibitisha kauli yake ya Juni 23, mwaka huu kuwa Baraza la Mawaziri lilishawishiwa na baadhi ya watu ili kuliongezea muda wa miaka mitatu Shirika Hodhi la Mali za Mashirika ya Umma (CHC).

  Lema alisema kuwa anamtaka Spika kutoa nafasi kwanza kwake ili aweze kutoa ushahidi wake bungeni ambao unathibitisha kuwa Waziri Mkuu alisema uongo bungeni na kuwadanganya wananchi juu ya mauaji yaliyofanywa na Jeshi la Polisi jijini Arusha.

  “Kama kweli Spika amekuwa na ujasiri wa kuharakisha kesi basi mimi naomba nipewe nafasi ya kutoa ushahidi wangu bungeni juu ya Waziri Mkuu kusema uongo wakati wa kipindi cha maswali ya Waziri Mkuu ya Papo kwa Papo, kwa sasa ni zaidi ya miezi minne sijapewa nafasi ya kuwasilisha ushahidi wangu bungeni, na nazidi kusisitiza kuwa Waziri Mkuu alisema uongo bungeni kwa nini mimi sijapewa nafasi na kwa muda mfupi Zito anatakiwa kuwasilisha ushahdi wake mapema hivyo, hizo ni dalili za makusudi kwa Spika kutowatendea haki wabunge anaowaongoza,” alisema Lema.

  Lema alihoji ni kwa nini baadhi ya wabunge ambao walionekana kusema uongo bungeni bado hakuna hatua zozote ambazo zimeshachukuliwa na ni muda mrefu sasa lakini iweje kwa Zitto ambaye kesi yake ni ya muda mfupi adaiwe kutoa ushahidi siku ya Jumatatau wakati wabunge waliotangulia hawajapewa nafasi ya kutoa ushahidi.

  Aidha Lema alisema kuwa Mbunge wa Kigoma Kusini David Kafulila (NCCR-Mageuzi), aliwatuhumu wabunge wa CCM kwa kula rushwa na Spika Makinda, alimtaka kutoa ushahidi lakini jambo la kushangaza bado hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa mpaka sasa.

  Aliongeza kuwa hivi karibuni mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa, alimtuhumu Waziri Mkuu kutumia vibaya magari ya serikali, ndege na kutakiwa kutoa ushahidi bungeni lakini bado hajapewa nafasi ya kutoa ushahidi wake juu ya ukweli kuwa Waziri Mkuu alitumia vibaya magari hayo ya anasa kwa msafara mrefu jambo ambalo alitakiwa kupewa muda wa kuthibitisha maneno ya mbunge huyo.

  Hata hivyo alisema kuwa majibu yaliyotolewa kuwa Waziri Mkuu alikuwa anatumia VX badala ya V8 ni utoto kwa kuwa matumizi ya magari hao ni sawa bali kinachotofautiana kuwa VX kutokuwa naa TV ndani na V8 ina video ndani mbele ya dash Board na viti vya vyuma ambapo VX haina lakini matumizi ya mafuta ni sawa.

  Lema alisema kabla Zito hajapewa nafasi ya kupeleka ushahudi wake bungeni siku ya Jumatatu ni bora Spika akatoa nasasi kwa wale ambao walitangulia kutakiwa kutoa ushahidi juu ya kauli zao bungeni kama zilivyotangulia na wala siyo kuharakisha kesi ya Zitto jambo ambalo alisema linaonyesha wazi kuwa Spika anashindwa kutoa fursa za wabunge katika kutoa ushahidi pindi wanapokuwa wakitoa hoja zao na wakalazimishwa kutoa ushahidi.

  Mbunge alisisitiza kuwa Waziri Mkuu alisema uongo bungeni hivyo, anamtaka Spika kutoa nafasi ya kutoa ushahidi bungeni ili kuweza kuelezea jinsi jeshi la polisi lilivyoweza kufanya mauaji kwa wananchi wa Arusha wasiokuwa na hatia na serikali ikapindisha ukweli kwa kisingizio kuwa chanzo cha mauaji kilisababishwa na maandamano yaliyofanywa na CHADEMA.
   
 2. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #2
  Jul 1, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,224
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  Kinachoniuma ni kuwa hoja za msingi hazitiliwi manani badala yake ni kutafuta umaarufu tu.
   
 3. JOHN MADIBA

  JOHN MADIBA JF-Expert Member

  #3
  Jul 1, 2011
  Joined: Jan 30, 2011
  Messages: 251
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  kwanini makinda hajamruhusu lema atowe ushahidikuhusu waziri mkuu kuongea uongo bungeni. Kwaninianataka kumruhusu zitto kutoa ushahidi huu mchezo unasiri ndani. Je wajua nini makind anataka kufanya???///
   
 4. Kimilidzo

  Kimilidzo JF-Expert Member

  #4
  Jul 1, 2011
  Joined: Jan 3, 2011
  Messages: 1,346
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 135
  Hoja muhimu ni zipi sasa, toa ufafanuzi sio kuongea kijumla jumla. hoja inaweza kuwa sio muhimu kwako lakini muhimu kwa mtu mwingine... Perception.. Madam Spika tenda haki, Lema, Zitto yote makinda yako usiweke double standards... Tumia FIFO na sio LIFO.
   
Loading...