Leading Without a Title: Zitto Zuberi Kabwe si wa Kubezwa

Status
Not open for further replies.

busar

JF-Expert Member
Dec 22, 2011
1,068
1,061
Ndugu!

Utangulizi

Nimetafakari sana juu ya Siasa za Tanzania. Nimeangalia kwa upana siasa zetu za Sasa (za kileo). Nikatazama mustakabali wa huko tuendako. Kama tunataka mabadiliko basi TUNAHITAJI WANASIASA VIJANA WAJANJA.

Dhima

Tupate watu wafaao kwa kuangalia waliopo.

Kiini.

Tumempoteza Maalimu Seif. Mwanzo Hizbu, akajakuwa ASP, CCM, CUF, baadae ACT-Wazalendo.

Tunajifunza nini? Jenga Mvuto na Nguvu kwa jamii yako bila kujali ni ndogo kiasi gani. Pemba ilimjenga Maalimu.

Turudi bara kwa Sasa.

Katika wanasiasa wa nje ya CCM naona Zitto ana Nguvu kubwa sana ya kuamua mwelekeo wa Siasa yetu kutokea upinzani.

Kwa sasa lazima ZZK awe sehemu ya mjadala muhimu wa nani anajaza nafasi ya VP Zenji. TISS hawana namna ya kumkwepa. ZZK katika hilo. Anaweza kutaka lolote. Liwe la kifedha, vitu au heshima. Lakini pongezi kwako ZZK. Nitajiunga na ACT Wazalendo.
 
..nadhani angekuwa CCM angekuwa mbali sana.

..mazingira ya siasa za nchi yetu yanawabeba zaidi wana-ccm kuliko walioko ktk vyama mbadala.
Naona CCM angekua neutralized kma Nape,Kafulila,Bashe, au Filikunjombe Yaani makali yasingeonekana.

Mara zote naamini kma angebaki CHADEMA akiwa na uvumilivu kma Mnyika then leo hii angekua mwenyekiti.

Kupitia uenyekiti CHADEMA angekua na nguvu sana na influence kuliko hata Peak-Dr Slaa otherwise mabadiliko ya katiba yakiwa agenda ya kudumu ya upinzani then ''kufika mbali'' kutakuwa more realistic kwa pande zote za kisiasa.
 
..nadhani angekuwa CCM angekuwa mbali sana.

..mazingira ya siasa za nchi yetu yanawabeba zaidi wana-ccm kuliko walioko ktk vyama mbadala.

CCM inalea vijana na kuwapa miongozo, kila hatua inayopiga kuna mzee au wazee wa kukuweka sawa na kukupa mawaidha. Kitu ambacho ni hadimu sana kwenye upinzani. Na hii sio kwamba CCM ni chama dola au kina hazina ya wazee, ni vyama vya upinzani kushindwa kujenga programu ya kulea vijana. (Kitu ambacho kinarekebishwa.)

Wote kina Kikwete, Magufuli mpaka kina Januari, Polepole nk.. Wakati wa kipindi chao walikuwa na waangalizi au wao wamekuwa waangalizi wa wengine.
 
Mwanasiasa inconsistent na anaebadilika kirahisi sana

Unakumbuka statement ya pamoja baada ya Uchaguzi mkuu ilikuwaje na yeye akafanyaje Zanzibar?
Unakumbuka kauli ya kubadili gia angani ilitolewa na nani? Kwa taarifa yako kuamzia kipindi hicho mambo hayajawa rahisi kwa wapinzani na kwamuktadha huo wote wapimzani wote hubadilikabadilika
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom