Le Mutuz, thread zako huwa ni burdani sana kutoka kwa wachingiaji.
Kitu kimoja ninacho appreciate kutoka kwako ni kuwa calm and composed. Huna jazba na hakika mwingine dhaifu awaye angeshakimbia. Nakutakia heri katika harakati zako, mtafutaji hachoki akichoka kapata
Ninakusihi usiondoke JF na kwenda kujificha katika blog. JF ni kisima cha maarifa na jiko la kupika watu mbali mbali.
Haya unayoyaona ni sehemu ya mafunzo na mwisho wa yote utaiva. Hao viongozi akina Zitto, Mnyika, Kigwangalla n.k wamepitia tanuru hili ndiyo maana unaona wapo wima kama ulivyosema.
FYI, kuwepo JF tu imekuwa bonge la Ad kwako. Kila mtu anajua Le Mutuz ni nani anafanya nini. Na usitegemee watu wote wakawa na mtazamo sawa na hivyo ndivyo jamii ilivyo na inavyopaswa kuwa.