Lazima akuvulie chu..

Lazima akuvulie chu..

mkurugenzi1

Senior Member
Joined
Mar 22, 2009
Posts
122
Reaction score
28
Jamaa: Hello mrembo, samahani, una mpenzi?
Binti: Hapana. Sina mpenzi.
Jamaa: Kitabu cha Mwanzo 2: 18 "Bwana Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye."
Binti: Lakini mimi sikupendi jamani.
Jamaa: Waraka wa kwanza wa Yohana 4:8 "Yeye asiyependa, hakumjua Mungu, kwa maana Mungu ni upendo."
Binti: Mh! Mi ntajuaje kwamba na wewe unamaanisha hayo maneno?
Jamaa: Injili ya Mathayo 12:34b "Maana, kinywa cha mtu huyanena yaujazayo moyo wake."
Binti: Jamani leo kazi. Mi ntajuaje kwamba we ni mkweli na mwaminifu?
Jamaa: Injili ya Marko 13:31 "Mbingu na nchi zitapita; lakini maneno yangu hayatapita kamwe."
Binti: Wewe! Na kwanini umekuja kwangu? Wasichana mbona wako wengi tu!
Jamaa: Mithali 31:29 "Binti za watu wengi wamefanya mema, Lakini wewe umewapita wote."
Binti: We una mambo wewe! Sasa mimi kwangu umependa kitu gani?
Jamaa: Wimbo Ulio Bora 4:7 "Mpenzi wangu, u mzuri pia pia, Wala ndani yako hamna ila."
Binti: Mh! Huo uongo, mbona mimi hata sio mzuri kihivyo. Unaongeza chumvi tu!
Jamaa: Mithali 31:30 "Upendeleo hudanganya, na uzuri ni ubatili; Bali mwanamke amchaye Bwana, ndiye atakayesifiwa."
Binti: Nikisema nimekukubalia itakuaje?
Jamaa: Mwanzo 2:24 " Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja."
Binti: Jamani we mkaka. Inakuaje unajua maandiko kiasi hicho?
Jamaa: Yoshua 1:8 "Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana."
Binti: Wowwww! Naona unampenda sana Mungu.
Jamaa: Zaburi 34:8 "Onjeni mwone ya kuwa Bwana yu mwema; Heri mtu yule anayemtumaini."
Binti: Mh! Haya bwana. Basi nipe muda nifikirie ombi lako.
Jamaa: Wafilipi 4:8 "Hatimaye, nduguzangu, mambo yo yote yaliyo ya kweli, yoyote yaliyo ya staha, yo yote yaliyo ya haki, yo yote yaliyo safi, yo yote yenye kupendeza, yo yote yenye sifa njema; ukiwapo wema wo wote, ikiwapo sifa nzuri yo yote, yatafakarini hayo."
Binti: Mh! Jamani wewe, haya, nimekubali. Mpaka hapo nakupenda tayari!!
Jamaa: Ufunuo wa Yohana 22:21b "Amina"
 
Sasa huku ni kutafuta laana,maandiko matakatifu yanageuka mistar ya kutongozea.hii ni hatariiii
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom