Lawyers tusaidieni; Kwa hiyo kanisa langu likifungiwa sitakiwi kuabudu kabisa hata nikikodi ukumbi?

Kitchener

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2019
Posts
13,823
Reaction score
27,694
Ni hoja niliyojiuliza, kwamba watu hawatakiwi kuabudu hata sehemu zingine, walau hata kukodi ukumbi ili kujifunza Neno la Mungu bila kwenda maeneo waliyozungushia utepe, kwa hiyo ile haki yao ya kuabudu imesimamishwa hadi kesi itakapoisha hata kama ni miaka 10? ndivyo katiba inavyotaka ilipotoa uhuru wa kuabudu?

Pia najua uhuru wako unaopewa na katiba hautakiwi kuvunja haki za watu wengine, nikawa najiuliza hawa watu wanaoenda kupigwa virungu leo baada ya msando kuwafukuza na kwenye ukumbi waliokodi kukusanyika kwa amani tu, vitendo vyao vimevunja haki ya nani ili pengine tuseme wasikusanyike kwani watadhuru haki za wengine?
 
Write your reply...kama wanatumia usajili wa kanisa la gwajima hawaruhusiwi cha msingi wasajili upya na jina jipya
 
Kwahiyo Kila anayeabudu lazima awe na kanisa?

Empty set!! Una fuvu tu ndani kuko wazi hakuna ubongo Bora ufugie kuku tu.
 
Ni hoja niliyojiuliza, kwamba watu hawatakiwi kuabudu hata sehemu zingine, walau hata kukodi ukumbi ili kujifunza Neno la Mungu bila kwenda maeneo waliyozungushia utepe, kwa hiyo ile haki yao ya kuabudu imesimamishwa hadi kesi itakapoisha hata kama ni miaka 10? ndivyo katiba inavyotaka ilipotoa uhuru wa kuabudu?

pia najua uhuru wako unaopewa na katiba hautakiwi kuvunja haki za watu wengine, nikawa najiuliza hawa watu wanaoenda kupigwa virungu leo baada ya msando kuwafukuza na kwenye ukumbi waliokodi kukusanyika kwa amani tu, vitendo vyao vimevunja haki ya nani ili pengine tuseme wasikusanyike kwani watadhuru haki za wengine?
Haki ya kuabudu wanayo, wanqweza kuabudu mahali popote watakapo ili mradi tu wasivunje sheria za nchi. Hata hivyo wanatakiwa kuitekeleza haki hiyo ya kuabudu kwa kuzingatia sheria za nchi, yaani kuabudu katika kanisa lililosajiliwa.

Ni kama vile haki ya mwananchi kupiga kura, unakuwa nayo lakini unaitumia haki hiyo kwa kufuata sheria, kujiandikisha kwenye daftari la mpiga kura, kwenda kwenye kituo sahihi ulichojiandikishia, kuwa na kitambulisho cha kupigia kura na kupiga kura wakati wa uchaguzi siku ya uchaguzi tu, sio muda wowote.

Kwa sasa hao waumini wanapigwa na kufurushwa kwa kuwa wanakusanyika pasipo kuwa na usajili, na ukisema ni waumini wa kanisa la ufufuo na uzima basi hapo tena wanakosa kibali kwa kuwa kanisa lao limefungiwa. Bora wajitambulishe kama wakristo tu wasio na dhehebu

Sema hizi mambo ni siasa tu. Unaweza kuta hata Gwajima anafurahi hivi kanisa lake linavyozinguliwa kwa kuwa kwake ni mtaji kisiasa na karata ya muhimu dhidi ya hasimu wake.
 
hawatumii usajili wa gwajima, wanatumia usajili wa wengine. kwa hiyo, ile haki ya kuabudu hapo, imeporwa kiwepesi namna hiyo.
 
Kwahiyo Kila anayeabudu lazima awe na kanisa?

Empty set!! Una fuvu tu ndani kuko wazi hakuna ubongo Bora ufugie kuku tu.
leo hii mimi nikiamua kuondoka na mke wangu kwenda mlimani kuomba, wanaweza kutufunga? kwamba tumekusanyika bila usajili wa kanisa? hii serikali inatakiwa iondoke ili tupate serikali itakayotupatia haki za kuabudu.
 
Ni hoja niliyojiuliza, kwamba watu hawatakiwi kuabudu hata sehemu zingine, walau hata kukodi ukumbi ili kujifunza Neno la Mungu bila kwenda maeneo waliyozungushia utepe, kwa hiyo ile haki yao ya kuabudu imesimamishwa hadi kesi itakapoisha hata kama ni miaka 10? ndivyo katiba inavyotaka ilipotoa uhuru wa kuabudu?

pia najua uhuru wako unaopewa na katiba hautakiwi kuvunja haki za watu wengine, nikawa najiuliza hawa watu wanaoenda kupigwa virungu leo baada ya msando kuwafukuza na kwenye ukumbi waliokodi kukusanyika kwa amani tu, vitendo vyao vimevunja haki ya nani ili pengine tuseme wasikusanyike kwani watadhuru haki za wengine?
Mkusanyiko wowote usio na kibali ni haramu. Hapo ukumbini mkianza kupigana na kujeruhiana nani atawajibika? Pambaneni haki yenu ya kuabudu mrudishiwe lakini sio kwa style hiyo.
 
Haki ya kuabudu wanayo, wanqweza kuabudu mahali popote watakapo ili mradi tu wasivunje sheria za nchi. Hata hivyo wanatakiwa kuitekeleza haki hiyo ya kuabudu kwa kuzingatia sheria za nchi, yaani kuabudu katika kanisa lililosajiliwa.

Ni kama vile haki ya mwananchi kupiga kura, unakuwa nayo lakini unaitumia haki hiyo kwa kufuata sheria, kujiandikisha kwenye daftari la mpiga kura, kwenda kwenye kituo sahihi ulichojiandikishia, kuwa na kitambulisho cha kupigia kura na kupiga kura wakati wa uchaguzi siku ya uchaguzi tu, sio muda wowote.

Kwa sasa hao waumini wanapigwa na kufurushwa kwa kuwa wanakusanyika pasipo kuwa na usajili, na ukisema ni waumini wa kanisa la ufufuo na uzima basi hapo tena wanakosa kibali kwa kuwa kanisa lao limefungiwa. Bora wajitambulishe kama wakristo tu wasio na dhehebu

Sema hizi mambo ni siasa tu. Unaweza kuta hata Gwajima anafurahi hivi kanisa lake linavyozinguliwa kwa kuwa kwake ni mtaji kisiasa na karata ya muhimu dhidi ya hasimu wake.
mwakasege anapozunguka kwenye semina, ana kanisa gani? amesajili kanisa? mimi kama mchungaji na mwalimu kama mwakasege, siwezi kukodi ukumbi na kuita watu waje niwafundishe Neno la Mungu au tuabudu pamoja kisa tu sijasajili kanisa? au ni kwa hao waumini wa ufufuo na uzima tu?

kwa kifupi, serikali hii imejaa watu wanaowachukia wakristo na ukristo, ila walikuwa wanakosa tu pa kuwapigia na kuwatesea ila mioyo yao ina chuki kubwa sana na wakristo. hili halijaanzia kwa gwajima tu, wala kwa padre kitima tu, wala kwa mengi yaliyopita. sidhani kama kungekuwa na rais mkristo waislam wangenyanyaswa kama wanavyonyanyaswa wakristo.
 
mwakasege anapozunguka kwenye semina, ana kanisa gani? amesajili kanisa? mimi kama mchungaji na mwalimu kama mwakasege, siwezi kukodi ukumbi na kuita watu waje niwafundishe Neno la Mungu au tuabudu pamoja kisa tu sijasajili kanisa? au ni kwa hao waumini wa ufufuo na uzima tu?
Mwakasege amesajili huduma inaitwa MANA. Yeye hajaisajili kama kanisa (church) bali ni huduma (ministry), na anapofanya mkutano ni kwa mawili, ama amealikwa na huduma nyingine mahali hapo au ameandaa yeye kwa huduma yake ya MANA. Huwezi fanya mikutano au makongamano bila kibali wala usajili.
 
Haki ya kuabudu wanayo, wanqweza kuabudu mahali popote watakapo ili mradi tu wasivunje sheria za nchi. Hata hivyo wanatakiwa kuitekeleza haki hiyo ya kuabudu kwa kuzingatia sheria za nchi, yaani kuabudu katika kanisa lililosajiliwa.

Ni kama vile haki ya mwananchi kupiga kura, unakuwa nayo lakini unaitumia haki hiyo kwa kufuata sheria, kujiandikisha kwenye daftari la mpiga kura, kwenda kwenye kituo sahihi ulichojiandikishia, kuwa na kitambulisho cha kupigia kura na kupiga kura wakati wa uchaguzi siku ya uchaguzi tu, sio muda wowote.

Kwa sasa hao waumini wanapigwa na kufurushwa kwa kuwa wanakusanyika pasipo kuwa na usajili, na ukisema ni waumini wa kanisa la ufufuo na uzima basi hapo tena wanakosa kibali kwa kuwa kanisa lao limefungiwa. Bora wajitambulishe kama wakristo tu wasio na dhehebu

Sema hizi mambo ni siasa tu. Unaweza kuta hata Gwajima anafurahi hivi kanisa lake linavyozinguliwa kwa kuwa kwake ni mtaji kisiasa na karata ya muhimu dhidi ya hasimu wake.
Lakini lile kanisa walilokwenda kuabudu mara ya kwanza lilikuwa tofauti na lao na bado walikwenda kulivunja hilo kanisa huoni hapo kuna kitu kingine kabisa
 
sidhani kama kungekuwa na rais mkristo waislam wangenyanyaswa kama wanavyonyanyaswa wakristo.
Na Wakristo hatujaelekezwa kulia lia au kupambana kimwili hivi dhidi ya watesi wetu, tumeelekezwa kuomba na kusali. Kwa hiyo kama unaona unaonewa na mamlaka za dunia, njia za kisheria hazijakusaidia, rudi magotini kwa Mungu lia. Unaweza kuiangusha serikali nzima kwa maombi badala ya kulialia wakati unajua haitasaidia chochote
 
Lakini lile kanisa walilokwenda kuabudu mara ya kwanza lilikuwa tofauti na lao na bado walikwenda kulivunja hilo kanisa huoni hapo kuna kitu kingine kabisa
Sasa hapo walalamikaji ni kanisa lililovunjwa, waumini wa hilo kanisa lililovunjwa au waumini wa Gwajima? Maana nimesema, popote watakapojitambulisha kuwa ni waumini wa Gwajima tayari wanakua wamejitambulisha kama wakosaji.
 
Jamaa wanaogopa kusanyiko wanahisi kutakuwa na maagizo ya gwajiboy.
 
Haki ya kuabudu wanayo, wanqweza kuabudu mahali popote watakapo ili mradi tu wasivunje sheria za nchi. Hata hivyo wanatakiwa kuitekeleza haki hiyo ya kuabudu kwa kuzingatia sheria za nchi, yaani kuabudu katika kanisa lililosajiliwa.

Ni kama vile haki ya mwananchi kupiga kura, unakuwa nayo lakini unaitumia haki hiyo kwa kufuata sheria, kujiandikisha kwenye daftari la mpiga kura, kwenda kwenye kituo sahihi ulichojiandikishia, kuwa na kitambulisho cha kupigia kura na kupiga kura wakati wa uchaguzi siku ya uchaguzi tu, sio muda wowote.

Kwa sasa hao waumini wanapigwa na kufurushwa kwa kuwa wanakusanyika pasipo kuwa na usajili, na ukisema ni waumini wa kanisa la ufufuo na uzima basi hapo tena wanakosa kibali kwa kuwa kanisa lao limefungiwa. Bora wajitambulishe kama wakristo tu wasio na dhehebu

Sema hizi mambo ni siasa tu. Unaweza kuta hata Gwajima anafurahi hivi kanisa lake linavyozinguliwa kwa kuwa kwake ni mtaji kisiasa na karata ya muhimu dhidi ya hasimu wake.
Sasa mbona jamii zingine zinafanya ibada zao za kijadi kwa kukusanyika na wanakua hawana vibali na polisi wapo tu wanaangalia?
 
Back
Top Bottom