Law School Of Tanzania

Kitang'wa1

JF-Expert Member
Dec 4, 2014
460
285
Hello! Wadau wa sheria humu, naombeni kuuliza jambo, kuhusiana na title hapo juu, maana napata shida kujua.

Nauliza, Law School Ya Tanzania, ipo chini ya Wizara ya Katiba na Sheria ama ipo chini ya Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam (UDSM)?!

Nitafurahi Nikijuzwa. Natanguliza Shukurani.

Ahsante!
 
SHERIA NA KATIBA. IPO CHINI YA WIZARA HIYO TANGU IMEANZA. ISIPOKUWA TU NI KWAMBA, WAKATI INAANZA HAIKUWA NA MAJENGO YAKE, HIVYO ILIBIDI IBEBWE KWA MUDA NA UDSM. KWA SASA IPO KWENYE ENEO LAKE CHINI YA WIZARA HIYO HIYO.
 
Nikiangalia kama sijakosea, naona sheria ya kuianzisha Law School, ya nchi hii, ilipitishwa mwaka 2008 na hiyo ni Revised Edition. Sasa nauliza tena, mniwie radhi katika hili, wale mawakili / wanasheria wa zamani 1970s na kuja juu hadi 1993 labda tuseme hivyo, kulikuwa na Law School, miaka hiyo?

Nitashukuru mkinidadavulia.

Ahsante!
 
Hata hivyo, nazidi kuwashukuru wale wote mlionijibu na mtakaonijibu vema.

Ahsante!
 
hakukuwa na law school badala yake kulikuwa na mitihani ya Bar mara nyingi ilikuwa ikifanywa Arusha ikiendeshwa na Tanganyika Law society
 
Nakushukuru ndugu hapo juu MASEETO, kwa jibu lako. Nisikuchoshe ama nisiwachoshe tu, nia ni kujua, maana naipenda sana kozi ya Sheria.

Kwa hiyo, wale waliofanya Bar Exam's, ilipoanzishwa hii Law School, walilazimika kwenda tena kusomea hiyo kozi ya Shule ya Sheria, ama kozi zinalingana tu na Bar Exam's, kimantiki hiyo?!

Nauliza hilo, maana kila aliyesomea sheria miaka hii, ili apate kazi (hasa Serikalini), na sasa lipo zaidi Sekta / Taasisi binafsi, lazima awe kasomea na Shule ya Sheria (Law School).

Natanguliza Shukurani Mkinijibu vema, lengo kuu nielewe. Nilipokosea mnirekebishe.

Ahsante!
 
Nilivyokuwa naisikia na kuielewa mwenyewe, hiyo mitihani ya Bar, niliamini inafanywa mwisho wa masomo ya Law School, yaani ndiyo final exam's, kwa maana hiyo.

Miaka hiyo iliyopita, mahakimu na wanasheria wa Serikali (nilivyoaminishwa), walikuwa wanaajiriwa tu baada ya kumaliza Bachelor zao za Sheria, kinyume na ukitaka kuwa wakili binafsi, ndiyo ukafanye hiyo Bar Exam's (by then, kama nilivyojibiwa hapo juu), tofauti na sasa, lazima nao wakasome Law School, ili uupate huo U-Hakimu ama Mwanasheria wa Serikali.

Naruhusu kwa Moyo safi kabisa, kukosolewa, lengo langu kuelewa.

Ahsante!
 
Jamani msinichoke kunielewesha, tugawane hiyo elimu kidogo ninayouliza, maana NATAMANI KUJUA NA KUELEWA.

Ahsante!
 
Nakushukuru ndugu hapo juu MASEETO, kwa jibu lako. Nisikuchoshe ama nisiwachoshe tu, nia ni kujua, maana naipenda sana kozi ya Sheria.

Kwa hiyo, wale waliofanya Bar Exam's, ilipoanzishwa hii Law School, walilazimika kwenda tena kusomea hiyo kozi ya Shule ya Sheria, ama kozi zinalingana tu na Bar Exam's, kimantiki hiyo?!

Nauliza hilo, maana kila aliyesomea sheria miaka hii, ili apate kazi (hasa Serikalini), na sasa lipo zaidi Sekta / Taasisi binafsi, lazima awe kasomea na Shule ya Sheria (Law School).

Natanguliza Shukurani Mkinijibu vema, lengo kuu nielewe. Nilipokosea mnirekebishe.

Ahsante!
kama umeshafanya Bar exams hakuna haja tena ya kusoma law school ni tofauti tu kwamba zamani hapakuwa na law school kwaiyo kimantiki ni kitu kimoja
 
Back
Top Bottom