acha chuki , Lavalava anajua sana mbona mimi binafsi namkubali kuliko hata hao unaowaona wewe wazuri labda... wimbo wake wa bora tuachane ni mzuri sana sana, anajua kutumia lafudhi ya Kiswahili vizuri
yaani wimbo ule na wa somo wa kassim mganga nikiusikia najiskia kama kweli niko pwani ya africa mashariki
Kwa mlioona show ya Jana mtakuwa mashahidi.
Wasanii wa WCB wote walifanya kazi nzuri sana kasoro Lavalava.
Kwanza alivaa kishamba pia hakupokea shangwe za maana kutoka kwa mashabiki kutokana na ukweli kwamba alikuwa anaboa mashabiki tu badala ya kuwaburudisha.
Hakika Simba (Diamond) hapa kwenye usajili wa haka kajamaa ulikosea sana nitazidi kukulaumu milele na milele.
Vijana bwana eti 'Label yetu ya WCB' [emoji23][emoji23] pambana upate mkate wako wa kila siku uyo mwenzio yuko jikoni tayari na anakaa meza moja na hao wenye label wakati wewe unalalama mitandaoni.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.