Tarehe 21 Novemba, 21
CNN kupitia mwandishi wake
Larry Madowo ilitoa taarifa ya kiuchunguzi kuhusu matukio yaliyotokea kuanzia Oktoba 29, 2025 kufuatia maandamano yaliyotokea katika mikoa mbalimbali na kusababisha vifo vya raia huku baadhi ya watu wakieleza kutokuwapata ndugu zao. Taarifa hiyo inaeleza na kufafanua kwa kina kuhusu video za wahanga wa maandamano waliofariki kwa kupigwa risasi, madai uwepo wa kaburi la halaiki na kadhalika.
Kumekuwapo
taarifa inayosambazwa mtandaoni inayodai kuwa Larry Madowo, mwandishi aliyeandaa ripoti hiyo amekiri kuwa alipokea malipo makubwa ya kifedha ili kuchapisha taarifa za kuchafua tawira ya Tanzania kwenye mitandao.
Vilevile taarifa hiyo imeambatanisha kuwa ni nukuu Larry akisema
“Nilikubali kushawishiwa na maslahi ya kifedha,” alisema. “Ninajutia madhara ambayo huenda nimesababisha kwa watu na kwa taswira ya Tanzania.”
Je, ni upi uhalisia wa taarifa hiyo?
Ufuatiliaji wa JamiiCheck kupitia nyenzo za kidigitali umejirirdhsisha kuwa taarifa hiyo si ya kweli.
Kupitia utafutaji wa maneno muhimu, JamiiCheck imebaini kuwa taarifa hiyo haijachapishwa na
African folder kama ilivyonukuliwa bali ni taarifa iliyotengenezwa na wapotoshaji.
Aidha muundo wa grafiki haufanani na
grafiki rasmi ambazo hutumiwa na African Folder. Kutofautiana kwa mwandiko (fonts) inadhihirisha kuwa taarifa hiyo ni ya kutengenezwa na wapotoshaji.