Lara1 ndio sababu ya kuachana na mpenzi wangu

St Lunatics

JF-Expert Member
Aug 29, 2015
6,644
11,173
Leo ni siku ya Valentine's day nikiwa namsubiri mpenzi wangu amalize kuoga, Nikasema wacha nifungue computer niangalie jf. Katika kuangalia habari za hapa na pale mara nikauwona uzi wa Lara1 unaosema:-
Valentine Story! Guess Who Is Getting Married? Marriage games.
Sasa nikaona wacha niusome mpaka my gf amalize kuoga na mambo yake ya make up nitakuwa nishaumaliza kuusoma ubuyu wa Lara1. Hee kumbe uzi wake ulikuwa mrefu hatari utasema story za tamthilia fulani na kila nikiusoma unazidi utamu. Na mimi sababu ya kujiunga hapa jf kiukweli story za huyu dada, ingawa pia akina General Galadudu,Nifah na Mshana jr na wengine wengi lakini Lara1 ndio sababu kuu. Mpenzi akamaliza akaja ukumbini akanipa hug na kiss cha shavuni akaniambia kuwa yupo tayari kutoka na kufurahia siku. Mara namsikia anaguna kooni nikamuuliza nini mpenzi mbona unakwaruza koo au una sore throat? Alichonijibu kuwa yupo tayari kwa kutoka nikasema sawa lakini ngoja nimalizie hii story kidogo ya lara1 manake ipo so interesting kwa kweli. Ama kusema jina la lara1 ilikuwa kama kuweka petroli kwenye mkaa wa moto. Nikaanza kuambiwa mpaka nikilala hutaja hilo jina la huyo malaya sijui mchepuko wako, kama ndio mchepuko wako basi toka nae yeye manake mie sitoki tena. Nikatupiwa flowers,chocolate na teddy bear wangu wa uso isipokuwa Samsung galaxy s6 edge hajanirejeshea akarudi chumbani nikasema wacha nikambembeleze ili tutoke. Sijui nini kilitokea kwa kweli hapa najiona nipo kitandani Hospitali ya Aga khan, Naangalia pembeni namuona mpenzi wangu anatoka machozi. Namuuliza nimefikaje hapa ananipa kioo najiangalia nimekaa kama kaka jambazi.
 
unaweza tunga stori nyengine ya kijambazi...? maana hizi mm huwa spendagi...!:):(
 
Usisahau kwenda choo kabla ya kulala ee usije lowesha godoro sawa eee
 
Tangu umejiunga jf 29 august 2015, leo ndio naona umejikakamua kuanzisha uzi aiseeee.....
Haya hongera mkuu
 
coz umekosea yaani mpenzi wako yupo tayari kutoka we unamsubirisha kwa kusoma story toka kwa mwanadada ambapo uwezekano wa kupata mawasiliano yake upo. unapokuwa na mpenzi wako ni kosa kubwa kuonyesha upo interested na mwanamke hadi tena hadi unaonyesha kuchanganyikiwa kabisa na huyo mtu
 
Back
Top Bottom