Kamanda
Senior Member
- Dec 5, 2007
- 150
- 176
Nimesikia na kusoma malalamiko mengi sana, tena kwa muda mrefu sasa, kuhusu mfuko wa pensheni wa LAPF.
Kinachoonekana kulalamikiwa na ndiyo ukweli, baada ya kuwa nimethibitisha, ni hatari kwa mfuko huo, kupoteza nguvu yake kiuchumi na kifedha baada ya kuamua kugeuka benki.
Ndiyo, mfuko unajifanya kuwa benki kwa kuanza kukopesha pesa za wanachama wake kwa wanafunzi wa vyuo vikuu na taasisi za elimu ya juu, kwa lengo la kujiongezea mapato. Lakini, amini naaambieni, hawa sasa wanakaribia kuanguka.
Inakuwaje LAPF itoe fedha moja kwa moja kwa wanafunzi hao, eti mdhamini akiwa mwajiri? Hawaoni kuwa huko ni kuweka fedha zetu mdomoni mwa choo cha shimo? Kwamba lazima zitatumbukia.
Iweje hawa wanashindwa kuiga wenzao kama PSPF ambao wamejiwekea utaratibu mzuri wa kutoa fedha za wanachama kupitia benki?
Chondechonde jamani LAPF, acheni kukopesha fedha zetu moja kwa moja kwa wanachama wenu wapya. Mtatuuuaaaa.
Sikieni malalamiko ya sie wanachama wengi, tena wa siku nyingi, kwamba hilo fao lenu halifaiiii