Nimesoma Comment zote za wadau, achana na hizo za utani, ninachojua komputa yako bado nzima, kulingana na maelezo ya wadau, wanaokushauri ununue nyingine siyo veeema saaana, ila waweza kununua kama una pesa nyingine. Cha kufanya;
1. Hakikisha hutumiii computer yako ikiwa juu ya kitambaa, kapeti au nylon na hata kwenye mapaja unatakiwa kuhakikisha sehemu ya cooling system haizibwi. Weka laptop kwenye plain table isiyona kitambaa. kitambaa kinaiziuia kupumua vizuri hivyo kuifanya ichemke, hust imajini mtu akisikia baridi hujifunika nguo, sasa huoni kama kitambaa chako kinaziba upozaji wa computer yako. hakikisha chini ya laptop yako kuna nafasi unapoitumia.
2. Nenda kanunue feni za laptop, zipo za aina mbalimbali, unaiweka chini ya laptop kisha unachomeka USB plug yake kwenye moja ya tundu la komputer yako, inapoza vizuri sana na itaokoa garama ya kununua computer mpya. Waweza ku Google ukaona image ya feni za laptop, kisha uchague inayokupendeza.
Kimsingi, inashauliwa kutumia kila laptop ikiwa kwenye feni yake hasa mikoa ile yenye joto. Hii inasaidia komputer kudumu muda mrefu. Kwa wale wanaonunua vi-Note book bila feni, huwa havidumu. Laptop au computer zinahitaji ubaridi ili ziweze kudumu. Na ndiyo maana inashauliwa chumba cha computer kiwe na cooling sytem, kiyoyozi nk ili kuzifanya zipate cooling ya kutosha. Tembelea taasisi za serikali zote- zenye Public Komputer utakuta zina cooling system, hii ni moja ya requirement ya chumba cha computer. Usipofanya hivyo computer hazidumu.