Tecno Spark 4 air yangu inapata moto sana na kuishiwa na chaji hovyo

toplemon

JF-Expert Member
Mar 26, 2017
4,581
4,631
Tecno Spark 4 air yangu inapata moto sana na kuishiwa na chaji hovyo

Hii simu inapata moto kila saa utashangaa inakwambia eti battery ipo na high temperature so remove battery na pia uchomoe chaja

Pia haikai na chaji vizuri mfano nilichaji ikajaa asilimia 100 saa moja jioni inafika saa 5 usiku kitu ipo asilimia 14 tu nashindwa kuelewa kwanini

Na ni mpya ina miezi 3 tu nilishauriwa niweke battery nyingine labda itakua sawa maana battery yake ni mah 3000 nikanunua ya itel mpya yenye mah 3500 maana watu wanasifu itel kwamba zinakaa na chaj nikaweka kitu kikawa ni kile kile tu siku hiyo hiyo nikaitoa nikarudisha battery yake ya mwanzo ni full majanga
 
Umesema simu mpya, hujui kwamba Tecno wana warrant ya miezi 13? umeifungua tayari warrant haifanyi kazi, hiyo simu ina short ndio maana inachemka na kula charge, tafuta fundi mzuri wa hardware aitafute hiyo short aitoe
 
Kuifungua kvp
Umesema simu mpya,hujui kwamba Tecno wana warrant ya miezi 13?,umeifungua tayari warrant haifanyi kazi,hiyo simu ina short ndio maana inachemka na kula charge,tafuta fundi mzuri wa hardware aitafute hiyo short aitoe
 
Oneni
Screenshot_20200620-011414.jpeg
 
Back
Top Bottom