Shida yangu kubwa ni neno "was" ukitaka kulitumia na verb unatumia verb gan Kat ya irregular verb, past au partipaticiple mfano juz boss aliniambia I was not seen you in an office hpo ilo neno seen ni past participle ya verb je ni sawa hpo naomben ufafanuzi wa kina
Japo kwa uchache na kwa kuchanganya lugha (si vizuri kujifunza lugha kwa kuchanganya)
WAS/WERE inatokana na kitenzi TO BE
PRESENT (Wakati wa Sasa/uliopo)
I
am
You
are
He/she/it
is
We
are
They
are
PAST (Wakati Uliopita)
I
was
You
were
He/She/It
was
We
were
They
were
I was at the office yesterday (Nilikuwa ofisini jana)
They were playing with the children last weekend (walikuwa wanacheza na watoto wikiendi iliyopita)
Hivyo am/is/are na was/were hutumika kama kitenzi kikuu (main verb) --angali sentensi ya kwanza-- au kitenzi kishirikishi (helping verb)--angalia sentensi ya pili.
Japo kuna wakati 'I' huendana na 'were'; ukitumia Conditional Clauses/If Clauses
Kwa mfano: If
I were you, I would not go outside ( Ningekuwa wewe, nisingeenda nje)
HAVE/HAS hutumika kuonyesha wakati mtimilifu au utimilifu wa tendo; aidha kwa wakati uliopo au wakati uliopita
I have done my work (Ni
mefanya kazi yangu)
She has gone to the shop (A
meenda dukani)
Have they stayed long? (Wa
mekaa muda mrefu?)
The car had left early (Gari lilishaondoka mapema)
We had already eaten at the hotel (Tulishakula hotelini)
Had you gone swimming at that beach? (Ulishaogelea katika ufukwe huo?)