Land rover discovery v8 - (1999 model) - bei tafadhali

Kaduguda

JF-Expert Member
Aug 1, 2008
724
641
Heshima mbele!

Nahitaji ushauri wa wataalamu wa biashara ya magari. Kuna mdau anataka kuniuzia gari hiyo - Land Rover Discovery V8i (model ya mwaka 1999). Gari ni nzima, nimeijaribu kwa kuendesha masafa marefu iko very comfortable na stable sana barabarani. Inatumia Petrol na ulaji wake wa mafuta sio mbaya sana. Ni kama lita moja kwa Km 8 - 9 hivi kwa kukadiria. Tatizo langu sijajua hii gari yaweza kununuliwa kwa kiasi gani kwa bei za hapa kwetu Bongo baada ya huyu mtu kuwa ameitumia kwa muda wa miaka mitatu tangu ameileta toka Japan. Odometer yake inasoma Km 95,000. Naombeni mnisaidie Bei ili nisiingizwe mjini! Nikauziwa bei ya magari mawili kwa gari moja! Wabongo siku hizi hawaaminiki!
 
Ndiyo umekuja huku ili unilangue eh, basi sikuuzii

Tafadhali mkuu! Niko serious mwenzio naogopa kulizwa! Hope hukuwa na nia mbaya ya kuniliza! Maana unaweza ingia kichwa kichwa ukatoka povu bure baada ya kugundua ushaingizwa mjini!
 
Back
Top Bottom