Naomba ufafanuzi kuhusu gari aina ya Land Rover Discovery TD5

Mzee Kigogo

JF-Expert Member
Jun 3, 2018
8,324
13,634
Heshima kwenu Wakuu! Hapa kati nimejichanga kama $ 13000 hivi nikaona sio mbaya nitafute SUV kwa ajili ya Safari za Porini hasa siku nimeamua kutembelea mbuga za wanyama.

Katika Pita pita zangu mitandaoni nikaona hizi gari Land Rover Discovery 2. Kuanzia mwaka 1999 mpaka 2004 kama sikosei nyingi zinatumia engine ya TD5.

Kwa wenye experience ya hizi gari naomba tushare mawili matatu kuhusu fuel consumption, Uimara wa gari hasa off-road na pia kuhusu upatikanaji wa spare parts na matengenezo yake kwa ujumla.

Karibuni Wadau wa haya magari.
3BAEBA74-9D8F-4670-99AD-BDC6BDDB74FC.jpeg
 
Mkuu hiyo gari nzuri kwa matumizi ya safari ndefu na mjini.Mafuta inatumia kawaida na inataka matunzo kama mtoto. Kwa safari za porini iko vizuri ila haikupi uhakika ikisumbua kidogo unalala porini.

Kama umri umesogea chukua hii, ila kama ni kijana usichukue hiyo pesa tafuta Land Cruiser series 80.
 
Mkuu hiyo gari nzuri kwa matumizi ya safari ndefu na mjini.Mafuta inatumia kawaida na inataka matunzo kama mtoto.
Kwa safari za porini iko vizuri ila haikupi uhakika ikisumbua kidogo unalala porini.

Kama umri umesogea chukua hii, ila kama ni kijana usichukue hiyo pesa tafuta Land Cruiser series 80.
Tunashukuru sana kwa mchango wako mzuri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu hiyo gari nzuri kwa matumizi ya safari ndefu na mjini.Mafuta inatumia kawaida na inataka matunzo kama mtoto.
Kwa safari za porini iko vizuri ila haikupi uhakika ikisumbua kidogo unalala porini.

Kama umri umesogea chukua hii, ila kama ni kijana usichukue hiyo pesa tafuta Land Cruiser series 80.
YEs mkuu! Land Cruiser 80 series ni gari ya ndoto yangu hasa upate Manual Turbo Diesel ila sasa hazipatikani now days na hata ukiipata bei yake imechangamka kidogo compare to Discovery.
Land Cruiser 80 or even 60 Series Ilikua chaguo langu ila kuzipata kwa bei hiyo ni nadra sana
 
Kupata landcruiser sio mchezo hasa kwa bei hiyo. Ila hiyo Discovery sio mbaya lakini inataka matunzo na service nzuri (kwa hiyo engine TD5). Za petrol ni nzuri zaidi ila zinakula mafuta sana. Kama unatafuta gari ya porini unaweza kuifikiria hiyo ika wenye uzoefu nazo watasema zaidi

Duh! Nyingi za Petrol ni V8 hapo ndio tatizo
I prefer TD 5 engine sababu wameshare na Land Rover defender. Nilifikiri TD5 ni engine imara kumbe sio mkuu?!
 
Td5 kuipeleka porini inabidi uwe unaenda nayo kistaarabu, hiyo haitaki shurba.
Kama safari zako ni za porini sana na njia mbovu inabidi uje uvue hiyo injini uweke TD200(mzee wa porini) ingawa ni ya kizamani na ina unguruma vibaya.
Sawa mkuu! Itabidi nijipange tena nitafute Land Cruiser hasa 60 series or 80 maana hizo ndio gari pekee za uhakika wa safari ukitoa LC hard top na Nissan Safari
 
Mk
YEs mkuu! Land Cruiser 80 series ni gari ya ndoto yangu hasa upate Manual Turbo Diesel ila sasa hazipatikani now days na hata ukiipata bei yake imechangamka kidogo compare to Discovery.
Land Cruiser 80 or even 60 Series Ilikua chaguo langu ila kuzipata kwa bei hiyo ni nadra sana
Mkuu kwa dau lako hilo la dola 13,000 za Mmarekani amini nakwambia unapata Land Cruiser series 80 kutoka South Africa na inalipiwa vibali vyote ila kwa engine ya 1hz iliyotembea sana na ipo katika hali nzuri.

Au ukinunua za kutoka Malawi na ukiilipia kila kitu hiyo pesa inabaki.
Kwa kuagiza kutoka Japan itakuwa ngumu hizi gari zimekuwa adimu na bei ipo juu.
 
Series 60 achana nayo sogea kwenye series 70.
Kwa dau lako ukitafuta zinazotoka Malawi unapata na pesa inabaki.
I
Series 60 achana nayo sogea kwenye series 70.
Kwa dau lako ukitafuta zinazotoka Malawi unapata na pesa inabaki.
60 series ukipata yenye good condition sio mbaya sana! Hasa upate Turbo Diesel. 70 series zina bei sana alafu nyingi hazina Turbo. I prefer 80 series zenye Turbo. Hizo unaweza kupata South Africa kweli?!
 
Mzee Kigogo, Kwa matumizi na porini Discovery 2 ni nzuri zaidi kuliko Discovery 3 &4 hasa ukiipata ya Diesel..ulaji wa mafuta ni mdogo..Ingine ina nguvu..speed 220km
Iko juu kiasi kwamba kwa porini si rahisi ku buruza chini ..Ni Gari imekaa kikazi na ya kiume. Hutajutia uamuzi wako..kuhusu spares..mara nyingi si magari ya kuharibikaharibika ovyo ila kama zilivyo landrover zingine spares zake ni kwa dealers au maduka maalumu na ni original spares zitakazokupa life span ya landrover yako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kiletza,
Ni kweli imekaa kiume hasa upata standard stick shift ila sasa uimara wake ndio tatizo hasa engine yake TD5 kumbe kimeo kama wadau walivyoelezea hapo juu.
 
Mkuu hiyo gari nzuri kwa matumizi ya safari ndefu na mjini.Mafuta inatumia kawaida na inataka matunzo kama mtoto.
Kwa safari za porini iko vizuri ila haikupi uhakika ikisumbua kidogo unalala porini.

Kama umri umesogea chukua hii, ila kama ni kijana usichukue hiyo pesa tafuta Land Cruiser series 80.

Nafikiria kuchukua Patrol Y60 Td42 manual,kuna mwana analiuza bei ya kawaida sana,nataka nilifungie trailer ya 2 tonnes kwa ajili ya kuingia nayo kwny mishe mishe mkuu.

Hio machine unaionaje?
 
Nafikiria kuchukua Patrol Y60 Td42 manual,kuna mwana analiuza bei ya kawaida sana,nataka nilifungie trailer ya 2 tonnes kwa ajili ya kuingia nayo kwny mishe mishe mkuu.

Hio machine unaionaje?
Hiyo chukua mkuu, kama ni jamaa yako muulize kama amewahi gusa injini au kuichezea fuel injector pump.

Hiyo ni gari ya uhakika kwa safari yoyote na unavuta tela vizuri.
 
Kama Iko kwenye hali nzuri ichukue mkuu! Sio gari ya kuuliza mara mbili.
Thnxs mkuu,ngoja nilifanyie makeke nina ka project huko porini nahitaji gari ya kazi na pia nitaitumia onroad pia kwa sana.

Khs Td5 way bay kuna bro wetu alikua nayo na ni ilitumia kipindi flani changamoto zake zilikua:

Ilikuja na air susepension(especially zile zenye seat 7 tairi zake za nyuma ndio zina hio air suspension),zinazingua mara kwa mara na ni expensive ku-zimaintain akazitoa akaweka coil.

Kufeli kwa EGR valve kama ambavyo ilikua ni ugonjwa wa magari mengi ya diesel ya miaka hio.

Pia ilikua na tabia ya Window Powers ku-fail/milango kugoma kufunguka kuna muda ilibaki mlango mmoja tu ndio unafanya kazi.

Kufeli kwa Fuel Pump mara kwa mara(at least kila baada ya mwaka 1 na miezi 4 alikua anaibadilisha)

Head Gasket pia ilikua kimeo sana.

Ilikua na shida sana ya ku-overheat.

Kama utanunua kwa mtu,fungua oil samp ukikuta kuna dalili zozote zile za diesel kwny ile Sump run away my friend.

Roof ilikua ina-leak wkt wa mvua hatari.

Ni gari zuri likiwa liko zima,lkn likianza magonjwa yake ambayo sometimes ki-ukweli hua hayaeleweki vzr na linataka attention sana yaani sio haya magari yetu tuliozoea kuyaburuza tu,Disco ukiona limewasha taa tu chap chap lipeleke likafanyiwe diagnosis la sivyo inaweza ikawa story nyingine na ujue hizi OBD-2 reader hazisomi kwny disco mkuu mpk upeleke kwa wale ma-specialist wake.

Na nadhani Td5 hua ina addiction wamiliki wake wengi hua hawayauzi ovyo ovyo.
 
Back
Top Bottom