Lami ya kimataifa

Hii lazima itakuwa contractor wa Tanzania!! Chakushangaza sasa ni hiyo gharama ya kujenga hiyo rami; utaambiwa billion of shillings!!! Nchi haiwezi kuendelea namna hiyo.
 
Si mmewapa wiki 2 wamalize barabara
Mnategemea nini tena!
Tulieni mkabidhiwe barabara
[emoji23][emoji23]

Ova
 
..surface dressing.. In layman's world ni aina ya utandazaji tabaka gumu la uji uji lami "bitumen" na kugundisha kokoto ndogo ndogo..namna ya utandazaji sasa ndio hapo wananchi tunashangazwa ila lengo ni barabara ipitike kipindi chote cha mwaka kwa urahisi.
 
Watanzania kama vitu hatuvijui tuwe tunauliza kwa ustaarabu kuliko mtu ana comment kwa kejeli kwenye kitu ambacho hana utalaamu nacho.

Hiyo lami mnayoiona hapo sio lami ya mwisho yaani kwamba baada ya hiyo lami kumwagwa basi traffic itaruhusiwa kupita.
Lengo la kumwaga hiyo lami ni
(1) kama huo udongo ulikuwa umechanganywa na cement basi hiyo lami humwagwa ili kuilinda hiyo layer isipigwe na jua moja kwa moja ili kutopoteza unyevu nyevu( moisture) ambao unahitaji na cement ili kutengeneza nguvu iliokusudiwa.
(2) Kazi nyingine ya hiyo lami ni kuilinda layer isiharibike yaani iwe tough na vile vile hiyo lami inasaidia kuweka bond kati layer inayokuja.

Kuna lami za aina nyingi na kila moja ina kazi yake, kwa hiyo sio kila unapo ona lami inamwagwa basi unajua barabara imeisha kumbe inakuwa bado hata layer tatu.
 
Barabara ipitike mwaka mzima!!!
 
#Tunatekelezakwakishindo
Hii lazima itakuwa contractor wa Tanzania!! Chakushangaza sasa ni hiyo gharama ya kujenga hiyo rami; utaambiwa billion of shillings!!! Nchi haiwezi kuendelea namna hiyo.
 
Sawa tumekusikia "mkandarasi" kutoka TARURA
 

Mkuu, kwa jibu lako ndio sababu siichoki Jf. Ila wapo baadhi hulifanya kila jukwaa ni utani na vichekesho. Mleta mada aidha ni mmoja wao au alikuwa na lengo lake tofauti na utani akapata wafuasi. "Sio lazima ujue kila kitu, ila busara na hekima ni kukaa kimya kwenye vitu usivyovielewa", kupitia ukimya wako utajifunza zaidi.
 
Mleta mada yawezekana alitaka aone mitambo mikubwa mikubwa na watu wenye asili ya ulaya ndio aamini ujenzi wa barabara unafanyika. Of course wakandarasi wa ndani walio wengi hawana equipments za kutosha na zenye viwango vya kimataifa ( tushajionea huko njiani lami inachemshwa kwa kuni) kwa hiyo wanajikongoja but angalau wanaojitahidi kinamna kufikia lengo ...ni kawaida yetu kukosoa zaidi kuliko kuangalia uboreshaji.
 
Ahsante sana mkuu.
Tatizo wabongo tumejaa ujuaji na kejeli za kishamba.
 
Lea gani wakati hawajac himba na kijaza kifusi mbona tunaona huku Mbezi hadi kufikia hatua hiyo kuna leya kadhaa za udongo kulingana na soil profile ya eneo husika au na wewe fundi mchundo
 
Wakandarasi wanafanya kazi masaa 24/7.View attachment 1765932
Hiyo ni Prime coat...

Layer inayowekwa baada ya stabilization layer (udongo uliochanganywa na cement) na pia hua inawekwa kwenye crr(layer ya kokoto)...


Kazi yake ni kui"seal layer husika (Inasaidia maji kutokupenya kutokea juu).

Hua inasambazwa kwenye barabara kwa njia kadhaa.. unaeza kutumia yale magari special au pia unaeza tumia pipes kama hizo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…