ASIWAJU
JF-Expert Member
- Nov 18, 2022
- 1,939
- 1,625
Habari za saa nyote natumai ni njema, moja kwa moja wacha niende katika jambo lililonifanya niandike lalamimiko langu.
Lalamiko langu linaenda kwa shule za msingi na upili katika taifa letu la Tanzania kuhusu suala la ulazimishaji wa vipindi vya dini kwa wanafunzi tena kwa kuwachapa viboko wale wote waliogoma kuhudhuria vipindi hivyo.
Imefika wakati dini kuonekana ni jambo la lazima kwa mwanafunzi wakati katiba ya taifa letu haielezi hilo.
: Kwanini uongozi wa shule mbalimbali za misingi na upili kwa hapa nchini zimefanya dini kuwa kipindi cha lazima pasipo kujali uhuru wa mtu kuwa muumini wa dini au la ?
Dini ni suala la hiari lakini hapa taifani kwetu katika shule za misingi na upili dini imechukuliwa kama ni suala lazima.
: Kwanini uhuru wa kimaamuzi wa wenye dini umezingatiwa lakini wa wasio na dini umefunikwa kwa viboko vikali na adhabu kali kutoka katika viongozi/ walimu wa shule ?
Mimi mwenyewe mleta lalamiko nilipata kuwa muathirika wa hili swala wakati wa uanafunzi wangu jambo lililo niletea kero kubwa kwangu.
: Kwanini wanafunzi wasiotaka kujishughulisha na masuala ya kidini wasipewe uhuru wao wa kufanya hivyo ? Kwanini iwe ni lazima kwa wanafunzi wote kushiriki vipindi hivyo ?
Ni hilo tu lalamiko langu kwa shule za Tanzania kuhusu lazimisho la kushiriki vipindi vya dini kwa wanafunzi pasipo kuzingatia uhuru wao wa kimaamuzi, ningependa kuona shule zote za taifa letu zikiji rekebisha kuhusu hili swala.