Uchaguzi 2020 Lala Salama Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura

Juakalee

Member
Oct 3, 2018
69
17
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kesho inaanza siku tatu za lala salama kwenye zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na Uwekaji wazi wa Daftari la Awali Tanzania Zanzibar na Mikoa 14 ya Tanzania Bara.

Hii ndio kusema kwamba Tume ipo kwenye maandalizi ya mwisho kuelekea Uchaguzi Mkuu.

Video iliyopostiwa kwenye IG page ya Tume hiyo inamnukuu Mkurugenzi wa Uchaguzi, Dkt. Wilson Mahera akisema kwamba tahadhari zote zimechukuliwa kujikinga na Covid- 19 wakati wa zoezi hilo.



Screenshot_20200501-143312_Instagram.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dodoma watu wamejiandikisha wachahche sana ! Juzi Mamlaka zililazimika kupeleka Waandikishaji amaeneo ya Wizaraili watumishi wajiandikishe huko!
 
Uchaguzi chini ya awamu ya tano ni kipimo halisi cha ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura. Hakuna mtu mwenye akili timamu ataweza kushiriki huo upuuzi bila tume huru ya uchaguzi.
Hivi mzee unaona dalili za kuwa na tume huru ya uchaguzi . ?
 
chama tawala kina thibitisha kwa umma kuwa hakina haja ya kuleta maendeleo ya kudumu kwa wananchi wa Tanzania. Jitihada zote za kutaka amani ya kudumu katika taifa hili zimegonga mwamba. CCM, wanalazimisha machafuko katika nchi. kila wakionyeshwa njia ya amani wao wana jigamba na vyombo vya usalama. Wananchi wamechoka na kama tahadhari ya kukataa demokrasia kuchukua mkondo wake, maafa yatakayo tokea nchi hii itakuwa balaa. Tunawanasihi viongozi watawala waone imani juu ya wananchi wao na kufanya yalio sawa. wanachodai wapinzani ndio haswa wanayo yataka wananchi. Tume huru ya uchaguzi, uwazi wa mijadala bungeni, kupotea wananchi na watu wasiojulikana, ukandamizwaji wa vyombo vya habari na wana habari, kuvunjiwa biashara na majumba pasi na sabau au fidia. etc.etc.
 
Back
Top Bottom