Lakisihela village | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lakisihela village

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by STABLE GIRL, Jul 1, 2011.

 1. S

  STABLE GIRL Member

  #1
  Jul 1, 2011
  Joined: Feb 7, 2011
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kweli usilolijua ni sawa na usiku wa giza. Wakati wengine wakifa njaa wengine wanaona laki si hela. Hapo chanika kuna kijiji kinaitwa lakisihela kwa maana kwamba mtu anayeishi hapo kutoa rushwa ya laki moja kwa afisa wa polisi au mheshimiwa fulani si tatizo.
  Kijiji hicho kimejificha sana kiko ndani ya hifadhi moja ya msitu wa asili karibu na mahandaki ya jeshi yaliyochimbwa kwa tahadhari ya vita. Watu wake wanajishughulisha na uvunaji wa miti na uchomaji wa mkaa kinyume cha sheria, pia wanachimba mchanga, wanawinda kwa kutumia silaha wanazopewa na askari wanaolinda handaki hilo au wanaoziuza kwa laki au pungufu, pia wanavuna mbolea ya popo inayopatikana katika handaki hilo. Kazi yao ambayo inawapa au kuwaletea migogoro wanakijiji hao ni biashara ya pombe haramu ya gongo.
  Waungwana tunakwenda wapi?
   
 2. S

  Sweetlove Member

  #2
  Jul 2, 2011
  Joined: Apr 18, 2011
  Messages: 56
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tanzania is among nchi sizojua zinakoelekea but racing to reach there.
   
Loading...