Laki sita zataka kumkatisha uhai mweka hazina wa kikundi cha kukopeshana Njombe

kilagalila

JF-Expert Member
Nov 8, 2018
320
154
1548503043125.jpeg
Mkazi mmoja wa mtaa wa Kihesa mjini Njombe aliyefahamika kwa jina la Maria mgeni (26) amenusurika kifo mara baada ya kujaribu kujiua kwa kunywa sumu kutokana na kushindwa kuwasilisha baadhi ya michango ya wanachama inayokaribia kiasi cha shiringi laki sita

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Rashid Ngonyani,alisema kuwa binti huyo mfanyabiashara ndogo ndogo wa mboga mboga alijaribu kujiua kwa kunywa sumu ambayo bado haijajulikana pamoja na kujichana maeneo ya kitovuni na kitu chenye ncha kali.

“Mnamo tarehe 25 mwezi wa kwanza 2019 majira ya saa saba mchana huko mtaa wa kihesa Njombe mjini mfanyabiashara huyo alijaribu kujiua kwa kunywa sumu na kujichana maeneo ya tumbo na kitu chenye ncha kali na baadaye aliweza kukimbizwa katika hospital ya kibena na kushonwa nyuzi mbili”alisema kamanda

Kamanda ngonyani alisema kuwa binti huyo ambaye ni mweka hazina aliamua kufanya hivyo kwa nia ya kukwepa kulipa deni ambalo alikuwa anadaiwa ili aweze kuwasilishwa kwa katika kikundi chake.

“huyu mwanadada anacheza mchezo wa kupeana shiringi 2000 kila siku na huu mchezo una wanachama takribani 90 kwa hiyo yeye alikuwa ni mweka hazina wa hicho chama chao na tarehe hiyo aligundulika hajawasilisha baadhi ya michango ya wanachama wake inayokaribia laki sita kwa hiyo alifanya hivyo kwa nia ya kukwepa kulipa deni ambalo alikuwa akidaiwa ili aweze kuwasilisha,na mtuhumiwa mpaka sasa ameshikiliwa na polisi na upelelezi unaendelea”aliongeza kusema kamanda Ngonyani

Katika hatua nyingine kamanda Ngonyani alisema kuwa jeshi la polisi mkoa wa Njombe linamshikilia mkazi mmoja wa mtaa wa matalawe aliyefahamika kwa jina la Zebedayo mgulunde (23) fundi ujenzi kwa kosa la kujaribu kujiteka.

“mnamo tarehe 14 mwezi wa kwanza mwaka huu huko mtaa wa matalawe kata ya Njombe mjini kijana huyo alikopeshwa kiasi cha shiringi laki mbili na nusu na ndugu Abel kitenge kwenda kununua mananasi na baada ya kukopeshwa pesa hiyo aliondoka na rafiki yake aliyefahamika kwa jina la Baba Frola kwenda Makambako kununua hayo mananasi na alipofika huko alizitumia kwa matumizi mengine”

“kwa hiyo mnamo tarehe 17 mwezi wa kwanza 2019 aliweza kumdanaganya Yule ambaye alimkopesha hizo fedha kwamba ametekwa na wakati anasema hivyo alikuwa akitumia simu ya baba Frola na baba Frola aliigiza kwamba ndiyo mtekaji wa huyu bwana aliyekopeshwa hizo fedha na alifanya hivyo ili kutoa taarifa za uongo asiweze kulipa fedha ambazo alikuwa amekopeshwa”alisema Ngonyani

Aidha Ngonyani alisema kuwa watuhumiwa wote wawili wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa ajili ya upelelezi.

Kuhusu matukio ya mauaji ya watoto wadogo yanayoendelea mkoani Njombe kamanda Ngonyani alisema kuwa jeshi hilo mpaka sasa linawashikilia watuhumiwa wawili wanaojihusisha na matukio hayo huku akimtaja Joel Joseph Nziku (35) ambaye ni dereva huko Magegere mjini Makambo pamoja na Alphonce Edward Danda (51) mbena mkristu na mkulima wa kijiji cha Ibumila halmashauri ya mji wa Makambako wote wakihusika na matukio ya utekaji na mauaji ya watoto.

mc.amiri/mr.mtaani
 
Hahaa...wamekula pesa ya kununua mananasi then wanajiteka. Wasiojulikana wametufundisha maujanja fulani hivi.
 
Back
Top Bottom