Lady Jadee afanyiwe maombi

Lady Jadee afanyiwe maombi

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
16,281
Reaction score
16,242
Kutokana na mashairi ya nyimbo zake na matukio yanayomtokea mwimbaji Judith Wambura (Lady Jaydee) vinaonyesha kuwa binti huyu ana shiida ya mahusiano mwanzo mwisho. Anaonekana kuwa ni binti ambaye hajawahi kuonja raha maishani kwake tangu utotoni.

Kwani msanii huyu ni nani? ametoka kwenye familia ya aina gani? alipata malezi gani akiwa mtoto? Mwenye majibu ya maswali haya hebu ajitokeze atusaidie kumfahamu msanii huyu mahiri wa Kitanzania. Vinginevyo mashabiki zake tujikusanye tumfanyie maombi ili na kwake mambo mazuri yatokee, maana siku zote pesa haiwezi kununua furaha hata kama ukiwa nazo nyingi.
 
Aliwahi kuwaita mashekhe nyumbani kwake wakamfanyia dua yakumtoa jini mahaba, sasa huenda halijatoka na ndo linammiliki
 
Si rahisi kutenganisha muziki na ushetani;na ndio maana matunda au matokeo yake yanaonekana hata kwa wanamuziki injili.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom