Ladies wa jf..mnauzungumziaje uteuzi wa mwanamama mwenzenu kuongoza bunge????? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ladies wa jf..mnauzungumziaje uteuzi wa mwanamama mwenzenu kuongoza bunge?????

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by NewDawnTz, Nov 17, 2010.

 1. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #1
  Nov 17, 2010
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kwanza niwaombe kabla ya kuchangia vitu vifuatavyo mviweke pembeni...

  (i) U-CCM na U-CHADEMA wenu na ule u-CUF sijui na Udovutwa n.k
  (ii) Ubongo wa kunyanyaswa kibeijing kwa kuletewa thread ya kujijadili; na tofauti nyingine zote

  Leo nilikuwa nasoma gazeti la MwanaHalisi na katika habari zilizonisisimua ni ile iliyobeba kichwa cha juu cha gazeti iliyoandikwa na mkulu mwenyewe Kubenea na nyingine mbili za Wanadada kama sio wana mama Jes Katunda na Evetha Swai wa kule UDOM.

  Katika makala hizi kumekuwa na mitazamo tofauti kama vile kumuona mama huyu kama kielelezo cha uwezo wa mwanamke (Evetha Swai) wakati makala ya Kubenea na kidogo ile ya Jes ikiwa na mtazamo tofauti wa kuona kuteuliwa mama huyu kama njia ya wajanja wachache kuendelea kuhodhi taifa hili kama vile ni la kwao wao peke yao.

  Nina mambo matatu nimeweza kuyaona katika waandishi hawa watatu;-
  (i) Kuteuliwa kwa Makinda kuna msukumo wa Rostam ambae alienda Iringa kumshawishi achukue kiti na kwa mujibu wa Makala ya Kubenea, mwandani wa mama Makinda amekiri ya kuwa mheshimiwa kakiri ni kweli

  (ii) Kama la hapo juu ni sahihi, basi ni sahihi pia ya kuwa lengo kuu lililoongoza CCM kutafuta speaker halikuwa kwenye nani anachaguliwa bali nani anaondolewa uspika (kwa Mujibu wa Jes Katund) na kwa mantiki hii huu sio uteuzi unaozingatia kuwa mama huyu anathibitisha uwezo wa wanawake bali huenda ni kuthibitisha udhaifu wake ambao utaweza kutumiwa na wajinga wachache kujinufaisha (labda tofauti na ilivyokuwa kwa Sita)

  (iii) Kuteuliwa kwake kunamaanisha kuwa CCM imetambua ya kuwa wanawake wana uwezo mkubwa sana katika kuenddesha nchi katika ngazi ya bunge jambo ambalo pia linatufungulia kuamini kuwa kama wanaaminika kuweza kuendesha bunge (yaani wananchi) basi hata nchi inaweza

  Kufuatia haya nimeshawishika kusikia je ni nini mtazamo wa great thinkers wakina dada na kina mama juu ya uteuzi wa mwenzao (bila kuathiriwa na mawazo ya hao juu niliyoyatoa kama mwongozo wa mjadala).

  Wakina baba mnaweza kutupakulia pia mitazamo ya wake zenu katika uteuzi huu wa CCM

  Nawasilisha
   
 2. s

  seniorita JF-Expert Member

  #2
  Nov 17, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 674
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  I think it is a mockery of both educational institutional and gender aspect in this country. If it was a gender concern, basi angewekwa mwyenawake ata=prove to Tanzanian society kwamba wanawake nao wapo, na wanaweza kuaminiwa kupewa nafasi za juu katika nchii hii. Sasa kama dada yetu AM with her advanced diploma of those centuries, plus mood swings, will that not prove that "women" are not ready to lead in this country? Nchi hii ina wanawake waliokubuhu kitaaluma, kwanini asitafutwe mwanamke ambaye kweli anaweza kuleta sifa kwa wanawake wa Tanzania na kwa wabongo wote kwa ujumla, na hata sifa kwa Afrika na dunia? A woman who will make our country proud!!! Ah...jamani....yatosha kwa sasa maana na kichwa kinauma nikifikiri haya......
   
 3. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #3
  Nov 17, 2010
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0

  Pole sana Seniorita...hawa wakina RA hawana hata heshima kwa waliowaleta duniani. Cha msingi ni kumfunda mwanamama mwenzenu kujipanga na kuchomoa meno kuwarudi wale wote waliompitishia mlango wa nyuma kwa kigezo cha jinsia ili wajue WOMEN CAN HAVE A STAND THAT MAN CAN NEVER MOVE A STEP ONCE THEY DECIDE like what my mother taught my about women psychology

  MPELEKENI KITCHEN PARTY HUYU MAMA
   
 4. S

  Singo JF-Expert Member

  #4
  Nov 17, 2010
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 1,073
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  upande wangu, siamini kama huyo new speaker ataweza stahimili mikiki. jana tu kayumbishwa sana na Mheshimiwa Tindu Lisu kwa MASWALA YA KANUNI ZA BUINGE, ALIZODAI ANAZIFAHAMU
   
 5. s

  seniorita JF-Expert Member

  #5
  Nov 17, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 674
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mwenzangu NewDawnTZ, can you possibly teach old do a new trick? Haiwezekani kwa huyo dadetu; too late;
   
 6. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #6
  Nov 18, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Kama mwanzo tu kaanza kutingishika huko mbeleni itakuaje???:nono:Kama kanuni za bunge zinamsumbua ataliendeshaje bunge?Kwa maoni yangu wangemchagua mtu ambae yuko ''up to date'' kitaaluma...mwenye mawazo na uelewa wa kutosha kuhimili mitikisiko ya bungeni!
   
 7. f

  furahi JF-Expert Member

  #7
  Nov 18, 2010
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 947
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Huyu mama hakuchaguliwa kwa sababu ya gender, everybody knows. Coz ingekuwa ni hivyo , wanaume wote wa sisiem wangeambiwa wasichukue form. Mbona walichukua? Wametudhalilisha sana wanawake coz wamemuweka mtu ambaye ni full of stress, short tempered, mbishi na kitakachofuata sasa ni dharau na aibu kubwa itakayotuangukia wanawake coz tutaonekana hatuwezi hata tukiwezeshwa! Kwanza nimempenda sana First lady we2 Mrs Josephine alivyozungumza jana kwenye 5 Connect ya EATV kwamba mambo ya gender si ya kukurupukia. Mwanamke aplay part yake kama mwanamke na mwanaume vile vile. Tusiforce mambo kisa ubeijing jamani. Ona sasa huyu mama anavyodhihakiwa kila sehemu kwa kutaka mambo makubwa asiyoyaweza. Aibu tupu kwa wanawake.!
   
 8. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #8
  Nov 18, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Upande wangu simwamini hata kidogo ,najua atateteleka hasa nikifuatilia misimamo ya uendeshaji wake wa vikao vya Bunge lililopita wakati spika Sitta akiwa hayupo.
  1. Hajiamini hata wakati wa kuongea ukimwangalia tu hana Confidence
  2. Alikuwa anakatisha hoja muhimu zilipokuwa zikiongelewa hasa kutoka upande wa upinzani.
  3. Alikuwa anacheka hata katika vitu visivyochekesha ambavyo vinatakiwa kuwa serious na
  kuhitaji Discussion ya kina

  Kwa kifupi yuko pale kimaslahi ya watu,hasa kifisadi zaidi...
   
 9. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #9
  Nov 18, 2010
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0

  Hahhaaa, Seniorita bana...unamaanisha mbwa mzee hafundishwi kuwindaaa......Poleni maana ninawasiwasi atawaabisha sana na kuonekana hamna uwezo. Kama akifanya hivyo atakuwa amewaangusha wakinamama na wakinadada wenye mauwezo yenu ya kufanya mambo kiasi wakina RA na EL hawawezi watumia
   
 10. MADAM T

  MADAM T JF-Expert Member

  #10
  Nov 18, 2010
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 3,672
  Likes Received: 941
  Trophy Points: 280
  ETI NILISIKIA WAMESEMA KIGEZO CHA KUMTOA SAMWEL SITTA NI KWAMBA WALITAKA SPIKA MWANAMKE, SASA KAMA UANAMKE NDIO KIGEZO NA SI UWEZO NINA WASIWASI HAPO, HE! KUMBE KUZALIWA MWANAMKE DILI SANA, NAJIPONGEZA KWA HILI ILA NAOGOPA!!:hippie::A S 109:
   
Loading...