NewDawnTz
JF-Expert Member
- Nov 15, 2010
- 1,667
- 362
Kwanza niwaombe kabla ya kuchangia vitu vifuatavyo mviweke pembeni...
(i) U-CCM na U-CHADEMA wenu na ule u-CUF sijui na Udovutwa n.k
(ii) Ubongo wa kunyanyaswa kibeijing kwa kuletewa thread ya kujijadili; na tofauti nyingine zote
Leo nilikuwa nasoma gazeti la MwanaHalisi na katika habari zilizonisisimua ni ile iliyobeba kichwa cha juu cha gazeti iliyoandikwa na mkulu mwenyewe Kubenea na nyingine mbili za Wanadada kama sio wana mama Jes Katunda na Evetha Swai wa kule UDOM.
Katika makala hizi kumekuwa na mitazamo tofauti kama vile kumuona mama huyu kama kielelezo cha uwezo wa mwanamke (Evetha Swai) wakati makala ya Kubenea na kidogo ile ya Jes ikiwa na mtazamo tofauti wa kuona kuteuliwa mama huyu kama njia ya wajanja wachache kuendelea kuhodhi taifa hili kama vile ni la kwao wao peke yao.
Nina mambo matatu nimeweza kuyaona katika waandishi hawa watatu;-
(i) Kuteuliwa kwa Makinda kuna msukumo wa Rostam ambae alienda Iringa kumshawishi achukue kiti na kwa mujibu wa Makala ya Kubenea, mwandani wa mama Makinda amekiri ya kuwa mheshimiwa kakiri ni kweli
(ii) Kama la hapo juu ni sahihi, basi ni sahihi pia ya kuwa lengo kuu lililoongoza CCM kutafuta speaker halikuwa kwenye nani anachaguliwa bali nani anaondolewa uspika (kwa Mujibu wa Jes Katund) na kwa mantiki hii huu sio uteuzi unaozingatia kuwa mama huyu anathibitisha uwezo wa wanawake bali huenda ni kuthibitisha udhaifu wake ambao utaweza kutumiwa na wajinga wachache kujinufaisha (labda tofauti na ilivyokuwa kwa Sita)
(iii) Kuteuliwa kwake kunamaanisha kuwa CCM imetambua ya kuwa wanawake wana uwezo mkubwa sana katika kuenddesha nchi katika ngazi ya bunge jambo ambalo pia linatufungulia kuamini kuwa kama wanaaminika kuweza kuendesha bunge (yaani wananchi) basi hata nchi inaweza
Kufuatia haya nimeshawishika kusikia je ni nini mtazamo wa great thinkers wakina dada na kina mama juu ya uteuzi wa mwenzao (bila kuathiriwa na mawazo ya hao juu niliyoyatoa kama mwongozo wa mjadala).
Wakina baba mnaweza kutupakulia pia mitazamo ya wake zenu katika uteuzi huu wa CCM
Nawasilisha