Ladies Love The Idea Of Average Joe's Not The Real Deal. Ile Package Ya Average Joe Kiboko

lara 1

JF-Expert Member
Jun 10, 2012
15,700
29,160
Igweeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee!!

Its such a shame sijawaletea ujumbe toka kwenye bible ila nawaahidi sio mwisho hazikuwa kiki za Mako wa Masogange. Nipo home recording is tough, watoto kila dakika wanaingilia instrumental. Ila nikirudi tu maskani nawaletea kitu.

For now tuendelee kumpa Kaisari yaliyo yake kaisari.

Wanawake wengi hususani sisi born town, born here watoto wa Kino, Migomigo, Ilala, Mikocheni, Sinza, Tabata kitambo hiko watoto wa mujini ni issue sanaa. We are facing real life struggle. Tumelelewa kimayai mayai malezi flani amazing. Kama mimi fikiria malezi gani i say anything to anyone, hata humu siogopi mtu, ofisini ndo kabisaaa, mtaani nimeshindikana. Watoto wa Mwinyi ni jipuuuuuuu.

Sasa kuna kaka zangu Average Joes, amabo ni kaka zetu wengi wetu, ndugu zetu, familia zetu, wapo wana hustle life halijakaa poa bado. They are hardworking and all ila bado kwa level za mwanamke. Hakuna kipimo cha average Joe, kwangu a well accomplished man kwa regina mengi ni average joe wa mwishooo kabisaaa. Average Joe kwangu kwa wanawake wa kitaa ni big fish catch.

Sasa shoga angu wa damuuuuu, ni Dr, na single mom, akaja kjniambia Lara time is oveeeer, like really over, tusichague sanaa, we should make it work na hawa hawa average Joe. They are the real dela sijui nini. Heheheeeeeee! Uzee mbaya sanaaaa. Si unaona wenye hela tunatumikaaa tu, mwisho wa siku hela zinafata hela kama baba J. Mi nimechoka, na down grade namkubalia Average Joe mmoja anashamba sijui la green house sijui analima mboga mboga was working in a bank ila akaachishwa. Long long story. Hahhaaaaa. Mi nikamwambia Mwili wako chaguo lako ukijitoa sadaka haya ukigawa sandakalawe haya. Mimi kama kawaida GET RICH OR DIE TRYING sina option ingine.

Akaanza oooh kwanza mama zetu waliwakubali averageJoe. We baba ako alikuwa na nini, unajua tunawakaidi wazazi. Hahaaaa. She just couldnt do it alone alihitaji approval japo moja tu. Nikamwambia that was the 80s plus hawakuzaliwa Kinondoni to know any better. Mama alitoka mgombani sawa alikuja mjini lwa dada mdogo form 1, kasoma mzizima jangwani, still she is from the bush, jembe anashika vizuri, anafuga, you cant take the bush out of a girl. Yeye alikuwa ahana option, either akae kwa shemeji au average Joe mdingi. Sasa we are born in better times, we have options, we should thank God.

Huku na huku akasema nimeamua i am going out with him, sihitaji approval wala explanation to do. Akawa kaja mdada mwingine mdogo tu, tukamwambia WE ARE HAPPY FOR YOU. Sasa the plot aliokuwa anatupa was very easy. Like AVERAGE JOES ARE NOT MEN BUT SAINTS. Analeta Akapelaaa za kitaaa.

Hadija huyo dogo akaniuliza sister Lara, hivi Dr. Hawajui wanaume wa uswazii hukuuuu, heheheeeee. Anacheza na mito. Nikamwambia tulia mtoto akililia wembe mpe, mwache achezeee FREE P wiki tu akili zitamkaa. Yule maisha boraa wamekaa sanaa Botswana huko kala bataaa, ashamaliza raha za dunia mwache achezee libolo Fc. Hadija akawa is she serious nikamwambia itafahamika.

Tukaitwa kumfahamu shemela, mimi tenaa sura ya mtu roho ya shetani. Shemela akaona shem si ndo mimi navompamba, nikaenda mpaka shamba na Dr, nikaomba na nyanya. Sasa Dr kuanza kupost picha za Shamba Man, Muhaya baby dady kakata fungu la matumizi by 80%. Walikuwa wanapasha kiporo. Muhaya was loaded from way back when. Japo ana matatizo yake ila hajajutia kuzaa nae. Kama seriali hakaukiwi mafunguuu.

Akaniambia napambana na mhaya atakataje fungu, Nikampa tu live shamba boy akijua hakuoiii ngooo, kwanza atastuka kujua bado mnapeana mafungu, come on you are a Dr, unafanya part time kwenye miradi, unauza nguo, your dad is loaded, you can make it work. Kumbuka uliamua mwenyeweee bila kushinikizwa. You can make it work, give Shamba man a chance. Mpe fair chance, cause mkioana Muhaya hatoleta hela. After all bado madolla ya kutosha hio shule ya mtaala wa cambriage, be appreciative. It was okay to push the limits before cause si ulikuwa unampa mzigo, sahivi dont try it kabisaa, just let it go.

They were going strong for about 3 month, the guy is good, very humble, very down to earth, anajua. Kumtreat mdada but blantantly LAZY. Sio hustler, wa kufosi kingi. Ana hio green house yake basi. Hafanyi chochoteee like it pays that much. Mtu wa kuridhikaaa na vitu vidogo sanaa. Akikusimulia kuhusu hio green house sasa weeeee utapenda, he can never be more proud na hio bustani sijui shamba. Hahahaaaa. Living the life of his dream, heheeheeee.

Muhaya akaacha kutoa ada kabisaa, madai kayumba kiuchumi ila mi namjua hustler yule kaka sijapata ona, the guy anafanya kazi 6 sio wa kufilisika wala kuyumba. Dr. Kapaniki, nikamwambia you can make it make it work, remember wewe ni Dr. (MD) Usijichukulie poa, piga Over time za kutosha hapo, komaa dukani, pesa karatasi. Wapiiii. Usicheche na ada ya $3000 chupi inaweza ikubane watu wahisi K kubwa chupi ndogo. Heheeeee.

Akaanza kusandaaa sasa. Nikamwambia mwambie shemelaaa, si mko wote for better, for worse. Ongea nae uone atakusaidia vipi. Usiconclude bila kumpa fair chance we mwambie msikize atasemaje, anachangia nini kwenye ada ya mtoto wenu. Akamwambia. Guess what alichomjibu. Shule ghali sanaa hio, mambo ya kuishi nje ya uwezo hayaweziii. Msaada ataompa ni kumpeleka Canosa na shule zingine affordable watafute nafasi. Heheehehee. Dr was furious, burning, kidogo amwambie ITS OVER. Eti anasema hivo cause sio mtoto wake.

Nikamwambia ofcourse sio mtoto wake hio ni FACT na the guy hana mtoto so hajui uchungu wa mtoto, still unaweza kulipa hio ada alone, mbona hela ndogo for your childs education, come on. You can always ask your dad his pension is larger than life, cut the guy some slack hajakunyima ila HANA to be fair. Muhaya ndo kakunyima. Fight kuipata kwanza ndo uombe uombe kwa watu. Akauliza HOW, HOW. Au niweke kwa mtu temporary naadhirika. Heheheeeeeee. Nikamwambia ziko legit jobs za kupata hio hela swala ni JE UTAZIWEZAAA.

Nawezaaaaaa. Nikamwambia anza kuuza vitafunwa maofisini, i was being sarcastic hahaaaa. Luckly akaona ni wazo zuri. Tukamtafutia tenda 4 za vitafunwa ofisini kwangu na kwa shoga zangu wa 2 na kwao. She is too lazy kukanda ule unga, akapika chapati kama ngumiiii, heheheee, nikamwambia you cant be serious huwezi kuuza this shit, watu wataharishaa after all nimekupigia debe, my reputation is at stake. Shoga jiko huliwezi, ushazoea enjoface fanya uwe unaamka saa 9 wahi magomeni nunu 100, 100 uza 500 faida 400 yote. Akapata mwanga. Average Joe anamwamsha mke mtarajiwa heheeeee. Siku 3 tu Hoiiiiiiiiii. Heheheeeee. Ananiambia si ninunu vya siku 2, nisiamke kila siku. Nikamwambia ukianza kutulisha lulala mie mwenyewe nitakuwa siliiii. Heheee. 2 weeks gig ya vitafunwa ikamshindaaa.

INAENDELEA





INAENDELEA LIVE KUTOKA KITAAA.
 
Siku zimeisha muhaya anadai kayumba kiuchumi, na yeye yuko tayari mtoto ahamishwe shule. Dr kakondaa, finacial stress ikaanza kuwatibuliaaa humo ndani. Akawa ana flirt na pastor mmoja, pastor ana mke, i dont why, ila pastror mwenye ushuzi wa hio $3000 hataaaa. Nikawmabia sasa wewe unaruka mkojo unaenda kutua kwenye nnya. Kama you are out of options cut the shamba guy loose ukamlambe miguu muhaya that will get you 3000 fatser sasa pastor atakupa nini, mwenyewe njaa tu. Ama sivo get to work.

Uza nyanya za shemela, cause ana nyanya na ma vegetable na matunda kuwa unatusambazia maofisini, tutanunua tu u shoga kaziiii japo haina pension. Bi dada akaona kero kuuza yeye, akamwambia Shemela awe anakuja na gari kutuuzia. Like kama mimi namkusanyia oda, jioni anakuja na kirikuu tunanunua. Si mnajua kazi za shamba hazitaki u smart.

Kama mjuavyo wateja hatukosi maneno heheheee. Mara Dr. Kaishaaaa lazima akondee wewe bwana muuza nyanya heheeheeee. Wengine Dr akamuombe mzazi mwenzie radhi sio kwa nyanya hizi, mmemuona shemela alivopaukaaaa na yebo zake heheheee, mapenzi upofuuuu. Japo mtua kishasema an kindoo cha nyanya kashanunua. Sasa ile status hospital ikashukaa. Utasikia aaaah mke wa muuza nyanya, mwambie Mr. Aniletee nyanya kesho. Heheheheeeee. Makazini humu ni JUNGU KUU. Akampiga marufuku shemela kuleta nyanya. Namwambia watu wanataka nyanya anadai zimeisha kumbe anamwambia bw. Shamba oda hamna. Heheheeeeee. Masikiniii.

Nguo mtaji alikataa fremu akarudishaaa. Sasa hadija akala bingo mume wa mtu anaenda nae South, akaja kuniomba ushauri. Mi nikamshauri ni waoz zuri ila asiende pekw yake aende na mimi kumbe je mlitegwmea nimshauri nini, nchi ya watu, nishahesabu mtu 3 kilo za kutosha, nauli ya bure. Aaaah. Mme wa mtu kakubali lazima akubali Hadija is only 23 yuko at the peak. Mi ndo dada wa Hadija, mme wa mtu nilijua kijana babu mzeee, sio mzee ila mtu mzimaa bwana. Tukamwambia Dr. Oooh na mimi naenda. Nikamwambia afu shamba boy utamwambia unaenda wapi, mwenzio mtu wangu nimemformat haniulizi maswali mengi na hata akiniuliza sikosi jibu isitoshe unadaiwa ada, mashauzi ya nini. Tafuta ada bembeleza ndoa hapo, wacha si tukale maisha. Alisikitika anamkumbuka muhaya hatari, baba J angenipa hio hela fastaaa, baba J, baba J mwisho kabakia. Ndiwoooo.

Alivona haendi anamshauri Hadija, Lara anakuponza sio vizuri kutembea na wanaume kama baba zako, South kitu gani uuze utu wako? Muache huyo baba, tafuta mume mdogo wangu. For a minute she had her. Akaja kuniambia Hadija like she is having second thoughts. Nikampanga acha kuzembea acha uboyaaa. We huyu baba ushamvulia nguo sanaa, what is ut one more time south huko? We kama unaona kuuza vitumbua Dr. Mzimaa ndo maisha shauri yako. Sasa mwenzio Dr yuko kwenye payrollwe hujasomaa, the only thing you have is Age. Tumia umri vizuri ukulipe ujijengee msingi. Kuuza nyanya yale sio maisha mahangaiko. Umetoka mkoani ukicheza utarudi huko huko. Mmmmhhhh! Akaenda kumwambia Dr vile vile mimi nimesema kuuza nyanya sio maisha, kuuza vitumbua sio maisha nad we are going bondeni baby.

Dr akaja kunisuta kwa uchunguuu mkubwaaa. Hahahaaaaaa! Nikajitetea tu mi nimeongea vile trip tu ilisababisha niuze utu wangu, but i dont mean what i said, and i am proud of her hehehee. Ila aliniona very bad friend indeed. Kama gundu tu ile trip ikawa cancelled sema the damage was done. In the end akaja kumuomba baba yake hela ya ada akapewa akalipa.

Ila they grew apart and apart na Shamba man, Alishindwa ku adapt mazingiraaa. Akaja kuniuliza one more time baada ya engagement na mahari will it be worth it. Nikamwambia sijui. Follow your heart. Basi ananiuliza inamaana baba atamsomesha J mpaka lini, nikamwambia fikiria mtakao zaa na shamba man, J has his dad who is supper loaded, harusi ikifungwa anchukua full custody atapewa maisha kule.

Akawa anawazaaa, anakondaaa kila siku. Ananiambia i thought i will be the happiest women ever, now i am finally marrying shamba man, mi namjibu you should be happy. Ananiambia tu i am not. Even mom is not. Mi namwambia Is he treating you bad low key, maybe something i dont know? Anasema hapana. Sasa nini tatizo mumy? Anadai i am not sure this is how i want to end. Nampa moyo, you will be fine, hela zinatafutwa tu.mimi tena kwa unafikiii na uzandikiii. We si ulisema unataka kuishi maisha ya mama zetu. Sio ndo hayo ya kufuga kuku, kuuza mikate, kulima bustani za matembele, you just got your wish! Hehheheheeee.

Akaniambia i think nampenda Baba J zaidi. Nikaona lazima cause the nigga gave you good life utaachaje kumpenda sasa. Huku namwambia hamnaa hata huyu ukikaa nae utaanza kumpendaa. Baba J is almost 8 yrs mnajuana huyu hata miaka 2 bado. Trust me give him a chance utampendaa. We kumkubali na hii hali yake si ndo True love yenyeweee. Hahahaaa haloooo.

Siku ya siku ananiambia SHOGA ANGU NIMERUDIIIII RASMIIIII. Namuuliza ulisafiri eeeh bila kuniaga. Nimerudi chamani chama cha GET RICH OR DIE TRYING. Ooooooooh! Nikaweka mikono kichwani, baaasi tenaaa ndugu wasomaji. Bwana yule bwana shamba nimemtupia hukooo. Nimerudiana na baba J shoga angu. Mkae mkao wa kuchapika bakora za machooo. Kwanza kashanipa mtaji wa kusafiri. Fremu tumelipa juzi hapo. Ada akniambia nisiwazeeee kabisaaa, tena antaka mtoto wa 2. Tobaaaaaaaa.Navokwambia kama tumependana janaa, full machat.

Nikaona algebraaa tupu. Nikamuuliza same old baba J.? Akasema THE ONE AND ONLY BABA J. Nikamjulisha Hadija. Hadija yuko nyoo alikuwa ananichuuza mimi, mbona yeye huyo mzazi mwenzie muhuni, malaya mbwa, kitombi hatariii hamuachiiii? Nikamwambia embu mchimbe Bwana Shamba yuko wapi sahivi, mimi nikakabe nafasi hahaaaaaa.

Akaja kunipa mrejesho masikinii Bwana Shamba, stress za kuachwa kaenda chuo kusomea uchungaji. Jamani mtu mwenye BAFF yake. Nikamwambia Hadija muongo. Yupo kweliiii na shamba kauzilia mbaliiii. Mmmmmmmmhhhh! Nikamuuliza bi dada wanasalimiana.? Yuko wapi kisa cha kuacha si alifumwa na sms za baba J, walichepukaaa. Nikamwambia basi YAMENITOSHAAAA.
 
I ask the the lord for everything i lack n more


Women loves u for free n Niggaz will hate u for nothing
 
Lara 1 ...true definition ya talent ila simulizi zako zinafanya niogope ndoa zaidi kuliko nnavoiogopa
 
Wanawake wengi wapo after money hawana mapenzi ya kweli.
 
Hivi hii habari ya utegemezi wa mwanamke kwa mwanaume ni kubwa kiasi hiki au Lara unayakuza? MD hawezi kulipia ada ya mwanae? Inabidi aendeleze mahusiano na mwanaume aliyemuacha ili mtoto asomeshwe??? Na mwanamke wa kiswahili anayechoma vitumbua au kusuka mikeka afanye nini? Tulipelekwa shule ili iweje kama hatuwezi kujisimamia na kujitetea?

Na baba wa mtoto akijaribu kuni-black mail na mtoto tena kwenye swala la elimu hakika ataujua upande wangu ambao hakuwahi kuufikiria. Ningekuwa mtamu hivyo asingeniacha.
 
Karma is a bitch! that time when we happen to make enough cash to splash, true love will be long gone! It's gon be payback time! And there's gon be no mercy for you ladies. We just have to start from the bottom, and we need someone to support us!
Hahahahahhaha jina lako tuu lol...mada imepata mwenyewee
 
Hivi hii habari ya utegemezi wa mwanamke kwa mwanaume ni kubwa kiasi hiki au Lara unayakuza? MD hawezi kulipia ada ya mwanae? Inabidi aendeleze mahusiano na mwanaume aliyemuacha ili mtoto asomeshwe??? Na mwanamke wa kiswahili anayechoma vitumbua au kusuka mikeka afanye nini? Tulipelekwa shule ili iweje kama hatuwezi kujisimamia na kujitetea?

Na baba wa mtoto akijaribu kuni-black mail na mtoto tena kwenye swala la elimu hakika ataujua upande wangu ambao hakuwahi kuufikiria. Ningekuwa mtamu hivyo asingeniacha.
Nimesoma kimya kimya. Nilisikitika na kushangaa MD anazunguka kuomba ada,mara aende kwa ex,mara kwa baba! Au ndio yale yale hela unayo lskini huoni raha hadi mwanaume akulipie au akununulie kitu?! Where the hell are independent ladies?!
 
Nimesoma kimya kimya. Nilisikitika na kushangaa MD anazunguka kuomba ada,mara aende kwa ex,mara kwa baba! Au ndio yale yale hela unayo lskini huoni raha hadi mwanaume akulipie au akununulie kitu?! Where the hell are independent ladies?!
Asking for genuine support from baba or anyone else is understandable, but this MD and women of her like are mental slaves. They are like kuku wa kisasa - you open a door for them to get out, but instead they enjoy the breeze and stay inside.

NB: I don't support lazy average Joes though.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom