Laana:

Laana:

kelao

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2012
Posts
8,132
Reaction score
5,811
Ndugu wanajukwaa nimekuwa nikijiuliza nini maana ya neno laana na anaelaaniwa huwa anapata madhara gani? Tulishuhudia tukio la kuvamiwa na kujeruhiwa dr.Steven Ulimboka,serikali na viongozi mbalimbali wa ccm walitoa matamko ya kuwalaani wahusika wa tukio hilo.hali kadhalika tulishuhudia matukio kama ya kutekwa kwa A.Kibanda,kuuwawa kwa D.Mwangosi,kuuwawa kwa padre E.Mushi,kujeruhiwa kwa padre A.Mkenda,kumwagiwa tindikali kwa Masheikhe,kulipuliwa bomu kanisani Huko Arusha Olassiti na hivi karibuni kulipuliwa kwa bumu kwenye mkutano wa CDM huko Soweto Arusha.Tumesikia matamko mbalimbali kutoka kwa viongozi wote wakuu wa serikali wakilaani matukio hayo.Je,nini mdhara ambayo yamewapata wahusika wa matukio hayo?Je,inatosha kwa serikali kutoa tamko la KULAANI tukio moja au jingine bila kuchukua hatua stahiki za kuzuia majanga kama haya?
 
Laana huwa inamrudia yule anayeitoa pasipo haki, au anayejifanya kulaani kumbe moyoni anachekelea. Hivyo viongozi wetu wanapotoa laana za kinafiki, hizo laana zinawarudia wenyewe na familia zao. Haya mambo tunayoyashuhudia nchini kama siyo laana ni nini? Wamejilaani na laana zimewakamata.
 
Hata mimi sijui maana ya laana ila nasikia mzee Mkapa uzito umemzidi hadi anatembelea fimbo sijui ni yale ya Pemba 2007?
 
Back
Top Bottom