Mimi kama nilimsikia vizuri mkuu wa ule mkoa nadhani alisema kuwa Msiba ule ni wa kitaifa, hivyo Serekali yake tukufu ndiyo iliamua iuweke pale uanjani na ni hiyo Serekali ingelichukua gharama yote. Ndo maana viongozi wakuu wakaitwa pale. Sasa mambo yalikobadilikia na kuja kuambiwa kuwa zile rambi rambi ndo hizo tena zitumike kuwa entertain viongozi na kupamba jukwaa, nimechoka. Nadhani serekali ijifunze kitu hapo, isiingilie mambo mengine. Ihudhurie tu kama waalikwa. Watu hawaielewi hivyo isizidi kujipaka uchafu hata usio wahusu yaani kuokota rambirambi. Tuna mfuko wa maafa sio wa kuweka rambirambi