La katiba nawapa credit tuongozeni tena kudai Tanganyika... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

La katiba nawapa credit tuongozeni tena kudai Tanganyika...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Luteni, Dec 1, 2011.

 1. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #1
  Dec 1, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Ni ukweli usiopingika Chadema imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kwenye suala la katiba, ingawa mchakato bado uko kwenye hatua za mwanzo lakini jitihada zao zimeonekana hakuna mtu atabisha kuwa bila wao tusingekuwa hapa leo, hii imezidisha imani ya watu kwao na kukomaa kwao katika masuala ya kitaifa kabla hawajawakabidhi nchi.

  Kwa hiyo basi, kwa nguvu ile ile na mapenzi yale yale waliyotumia kufanikisha hilo naomba waanze kupiga kelele tena kuanzishwa kwa serikali ya Tanganyika Insallah watafanikiwa. Msiogope sera yenu kutekwa na wapinzani wenu kama walivyoteka sera ya katiba kwa vile mwisho wa siku watakaofaidika ni wananchi wote wa Tanzania kama tukavyofaidika na kuanzishwa kwa katiba mpya.

  Nawasilisha.
   
Loading...