La David Mattaka: Kwenye Hili simwelewi Kikwete!

Ngereja,

Mkuu samahani mbona mimi nakumbuka PPF ipo toka miaka ya 80 kama sio 70s!.... naomba somo mkuu wangu..

Heshima mbele mkuu,kumbuka PPF ilikuwa ni kitengo ndani ya NIC mpaka kilipoaanza kujitegemea rasmi mwaka 1992.PPF ilianzishwa mwaka 1978 chini ya sekretarieti ya shirika la bima la taifa,hadi kufikia mwaka 1992,ilipojitenga na kuwa shirika linalojitegemea.

Ni hivyo tu mkuu,nafikiri huo ufafanuzi unakuweka mahali pazuri.
 

Mzee naona unapiga remix ya bongo flava!!
New songs please!!!
 
Hahaa, hahaa.. What JK is doing at ATCL, is like "Kwenda kuazima jamvi Msibani" He should let Mattaka solve his mess at ATCL...
 
Sijui tusema na wenye wanatafuta Perdiem?, haiingii akilini hata kama anauona Mataka yuko fiti kwa mtazamo wake alitakiwa amwache arekebishe mambo kule ATCL. Hapa JF tunatakiwa tuwe na mwanasaikologia wengine tunaweza pata presha na ujinga unaoendelea
 
Kwa nini hawa viongozi wote wasipimwe akili?

Mbona sipati majibu ya haya madudu wanayofanya?
 
ATCL siyo kipaumbele cha JK, ATCL imeachwa kama mtoto yatima nobody ambaye anataka kuiinua na kuiimarisha.
Ni vema serikali ikahakikisha kuwa wafanyakazi hawapotezi tena haki zao kwa mwekezaji wa Kichina. Ninafahamu vizuri kabisa mchakato wa kuwapa wa China ATCL haukuwashirikisha wafanyakazi kwa makusudi kabisa ili iwe rahisi kwa serikali kuwatoa kafara wafanyakazi pale ambapo itatakiwa kuwajibika kwao katika utekelezaji wa mkataba mzima.
Sioni uwekezaji mpya kwenye shirika ambalo halijaimarika kama utaleta tija, tujitayarishe kwa yajayo
 
sielewi mkulu wetu anamatatizo gani maana kazi yake ni kuchekacheka tu,kuzurura na huku watu wanateketea kwa maisha magumu,kuchagua mabest wake ambao wanazidi kuleta hasara kila leo.sielewiii!!nisaidieni
 

Mheshimiwa Dr. Slaa, natanguliza heshima kubwa.

Naomba ufafanuzi kidogo kuhusu liabilities za NIC na athari za uteuzi huu kwa wenye Bima za Maisha. Nadhani waTanzania wengi wanaotumia Bima hii wanatakiwa wajue madhara yanayoweza kuwapata, ili waanze kuchukua taadhari zinazotakiwa/zinazostahili.

Inashangaza sana kusikia mtu anashindwa kutekeleza wajibu wake sehemu moja na kupelekwa sehemu nyingine, tena yenye matatizo makubwa vile vile. Sijui tutafika wapi na teuzi kama hizi.

Nadhani umefika wakati ambapo maslahi ya nchi yawekwe mbele, kuoneana haya na kupendeleana kuwekwe pembeni kama kweli tunataka kufikia malengo tuliyoyaweka.

Rais anayo mamlaka ya kufanya uteuzi alioufanya, ila swali ni je, amefanya kwa maslahi ya nani? Ni kweli anaamini kuwa uteuzi wake ni sahihi? Na analipa fadhila gani kwa waTanzania waliomchagua? Maana kila mtu anashangazwa na mambo kama haya.
 
Duh! This is too much now. The only plausible explanation is that Kikwete is purposely irritating wananchi.
 
Duh! This is too much now. The only plausible explanation is that Kikwete is purposely irritating wananchi.
Mimi najiuliza wakati Kikwete anam-appoint David Mattaka ina maana alikuwa hajui inside out of this guy.
 
tukielekea kuona cinema ya kituko tuijiulize walioiba billion wako wapi na KIBO PALACE ZAO/NMC ZA ARUSHA MMH NAIPENDA NCHI YANGU
 
pamoja ya kuwa huyu bana mataka kakamatwa hivi kunauwezekano wa mahakama kutenda haki kweli kwani jamaa ni schoolmate wa Raisi,ngoja tuone
 
He!!! Kikwete ni honest,wise,dedicated!! Mama Mia!!!!! Cronyism at its best.
 
david mattaka ni moja kati ya 'majembe' ya JK, kwa hyo muacheni mjomba alitumie jembe lake! maadam bado lina makali sion sababu za kuponda uteuzi wake!
nashangaa mnachoshangaa kwan ni kawaida ya mjomba kumhamishia sehemu nyingine mtu aliyeboronga sehem fulani...! kama aliweza kwenda kulitetea jembe lake la Rombo atashindwa kwa Mattaka ambaye ni watu wachache wanaomfahamu?
 
mimi nadhani tupige kampeni ya kutuma SMS kwa ajili ya JK ili aingie katika maajabu saba ya dunia baadala ya mlima Kilimanjaro!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…