Kwenye politics .chama kuwa na political bases ni jambo la kawaida mf ccm ina bases mikoa ya pwani hususan Tanga. Political bases hazijengwi kwa fitina japo kwa mipango na mikakati mahususi. Binafsi namfahamu zitto tangu tukiwa UDSM japo alinitangulia. Siasa za zitto na mwigulu kama zinatofautiana ni kidogo sana. Wawili hawa waligawana njia tu lakini ni watumishi watiifu wa kitengo . Mwigulu yupo kwenye baraza kwasababu kumuacha nje ni hatari kuliko kuwa nae ndani ya baraza. Haya nilielezwa na veteran mkongwe kabisa wa ccm. Hembu jaribu kufikiria kwa kadhia ile ya kariakoo jana wale waliokuwa wanamshangilia bwana mwigulu ni kina nani haswa na walikuwa wanashangilia nn? Wale ni watu walipangwa na mwigulu ili kumpumbaza mama . Hizi ni siasa ambazo mwigulu alizifanya tangu akiwa mwanafunzi wa uchumi pale UDSM. Ilifikia wakati watu wanaenda kwenye mgomo mwigulu anapanda jukwaani bila kuonesha upande zaidi ya kuonesha mikono yake juu kwamba anaunga mkono kinachoendelea.