kwikwi ya nondozzzzz za CBE ( by Michuzi)

Kottler Masoko

Senior Member
May 28, 2010
193
28
Ankal pole na kazi za kuelimisha jamii. Tunaomba utuwekee katika glob yetu ya jamii ili maombi yetu yasikike kwa wahusika, maana tunajua haakosi kutupia jicho humu.

Sisi tulikuwa wanafunzi wa chuo cha elimu ya biashara CBE Dar es Salaam
tumemaliza mwaka 2006 wengine mwaka 2007 na tulifaulu katika masomo tuliochukuwa Ajabu mpaka leo huu mwaka wa nne hatujapata vyeti vyetu muda tuliosoma ni miaka mitatu ni ajabu muda wa kusubiri vyeti unazidi muda wa masomo na kila kukicha ni sababu tuu, mara printer hajapatikana, mara vinachapishwa nje ya nchi ili mradi siku zinakwenda ikiwa na ada tulishalipa tukamaliza tena kwa wakati.

Hii inatupa shida hata tunapoomba kazi wanakuwa na wasiwasi kama kweli tulisoma hapo maana tunatumia transcript ambazo wengine hawazikubali na hata iwapo unatakiwa upande cheo mwajiri anasema lete cheti chako kama huna unabaki palepale ulivoajiriwa na cheti cha awali.

WADAU WA CBE HUMU JAMVINI,HIVI WAHUSIKA WANATAMBUA UMUHIMU WA HAYA MAKAVA????
 
sio cbe peke yao jamani ndo maana tunasema serikali hii imetuchoshaaaaaa watumishi gani wasojali kazi tulizowakabidhi
 
nafikiri mko karibu sana na DIT,hembu mshaurini huyo mkuu wenu akajifunze kwa Prof J Kondoro,nafikiri hatatoka bure!
 
Binafsi nilimaliza elimu yangu ya chuo hapo CBE Dsm campus mwaka 2006 na mnamo October,2007 nilifika hapo chuoni na kuchukua cheti changu.Sasa hii habari yenu inanipa walakini!
 
Back
Top Bottom