Kwenye watu kumi binadamu mmoja | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwenye watu kumi binadamu mmoja

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Bujibuji, Aug 17, 2009.

 1. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #1
  Aug 17, 2009
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,265
  Likes Received: 22,010
  Trophy Points: 280
  'Wanawake Watakaowanyima Unyumba Waume Zao Kunyimwa Chakula'
  [​IMG]
  Rais wa Afghanistan Hamid Karzai




























  Sheria mpya inayowaruhusu wanaume wa madhehebu ya Shia kuwanyima wake zao chakula na matumizi mengine iwapo watagoma kuwapa unyumba imepitishwa nchini Afghanistan pamoja na mataifa mbali mbali ya magharibi kupinga muswada wa sheria hiyo.

  Sheria hiyo mpya imetiwa sahihi na rais wa Afghanistan Hamid Karzai anayepewa msaada na Marekani pamoja na kwamba awali aliahidi kuiangalia upya sheria hiyo.

  Kwa mujibu wa shirika la kutetea haki za binamu la Human Rights Watch-HRW lenye makazi yake New York, Marekani, sheria hiyo mpya iliyofanyiwa marekebisho ilitangazwa kwenye gazeti la serikali julai 27 mwaka huu na sheria hiyo imeishaanza kutumika.

  Waislamu wa madhehebu ya Shia wanachukua asilimia ndogo sana ya waislamu wa Afghanistan wakikadiriwa kufikia asilimia 15 tu ya waislamu wote nchini Afghanistan.

  Mbali na sheria hiyo kuwaruhusu wanaume wa shia kuwanyima chakula wake zao wanapokataa kuwapa unyumba, pia inawataka wanawake waombe ruhusa kwanza kwa waume zao kabla ya kuanza kufanya kazi.

  Sheria hiyo ilikuwa ikipigiwa debe na kiongozi wa shia nchini humo,Ayatollah Mohseni, ambaye kauli zake zinaaminika kusikilizwa na zinaweza zikabadilisha mwelekeo wa waumini wa shia katika upigaji kura katika uchaguzi mkuu utakaofanyika wiki ijayo.

  Matokeo ya kura za maoni kabla ya uchaguzi huo yalionyesha kuwa rais Karzai alikuwa akiongoza kwa asilimia 44 akifuatiwa na mpinzani wake wa karibu Abdullah Abdullah aliyepata asilimia 26 ya kura hizo za maoni.

  SOUCE:- NIFAHAMISHE.COM
   
 2. Wa mmoja

  Wa mmoja Member

  #2
  Aug 17, 2009
  Joined: Aug 4, 2009
  Messages: 99
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Duh!ni noma!
   
Loading...